WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Tuesday, October 2, 2012

Watoto Wa Wassira Kujiunga CHADEMA; Ufafanuzi




TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI UFAFANUZI KUHUSU SISI KUJIUNGA NA CHADEMA NA MALUMBANO KUHUSU MAJINA YETU 

 Tarehe 30/09/2012 mimi Esther Wasira na dada yangu Lilian Wasira tulijiunga na CHADEMA na kukabidhiwa kadi na Katibu Mkuu wa CHADEMA Mh. Dr Willibrod Slaa. Tulielezea kwa kirefu sababu za sisi kujiunga CHADEMA na tukasisitiza kuwa tumeridhika kuwa CHADEMA ni chama chenye dhamira safi ya kuiongoza Tanzania na kwamba ni chama kinacholeta matumaini mapya ya kuijenga Tanzania mpya yenye neema. Waandishi wa habari walijaribu sana kutudodosa kujua tuna uhusiano gani na Waziri Steven Wasira. Tulielezea wazi kuwa mahusiano yetu ya kifamilia hayahusiki na sababu na dhamira yetu ya kujiunga CHADEMA. Hata hivyo tulielezea kuwa Waziri Steven Wasira ni baba yetu mdogo ambaye alinyang'anyana ziwa na baba yetu mzazi, wakili George Wasira. Tulidhani hiyo ilitosha na lisingekuwa swala tena la kujadili na badala yake hoja ya kujadiliwa ingeweza kuwa sababu tulizozieleza za kujiunga CHADEMA. Tunasikitishwa sana na malumbano yaliyofuata baada ya hapo kuhusu kama sisi ni watoto wa Wasira au la. Kama tulivyoeleza, tumejiunga CHADEMA kwa sababu tulizozieleza hapo awali na wala si kwa sababu nyingine yeyote. Hatujajiunga CHADEMA kumdhalilisha mtu, kumfedhehesha mtu au kukipatia umaarufu CHADEMA kwa vile tu tunatumia jina la Wasira. CHADEMA ni chama cha siasa tena chenye wanachama na wafuasi wengi Tanzania hivyo si kashfa bali ni fahari kubwa mtu kujiunga CHADEMA na tena ni ushahidi wa mtu kujitambua. Pia CHADEMA ni Chama maarufu sana Tanzania kwa sasa hata pengine ni maarufu kuliko CCM hivyo hakihitaji kujipatia umaarufu kwa mgongo wetu. Sisi tunawaheshimu sana wazee wetu na tutaendelea kuwaheshimu ila linapokuja swala la chama cha kujiunga linabaki kuwa hiari yetu kwa kuzingatia sera za chama na uwezo wa chama husika katika kujenga Tanzania tunayoitaka na hilo ndilo lililotupeleka CHADEMA. Na hii ni haki yetu ya msingi kabisa inayolindwa na Katiba ya nchi hii chini ya ibara ya 20(1). Ikumbukwe kuwa mmoja wa Waanzilishi wa CHADEMA ni Mzee Wasira. Dhamira ya kuanzisha CHADEMA ilikuwa ni kushika dola na hili ndilo CHADEMA imekuwa siku zote inajaribu kuwashawishi Watanzania kuwa sasa wamekomaa na wanastahili kuchukua dola. Kwa vile kuchukua dola ilikuwa ndio ndoto ya baba yetu mzazi Mwanzilishi wa CHADEMA, sisi kama watoto tumejiunga na M4C ya CHADEMA ili tuweze kutimiza ndoto ya baba yetu kuwa CHADEMA siku moja ichukue jukumu la kuiongoza Tanzania.
 Kwa maelezo zaidi wasiliana na: Lilian Wasira 0719 604156 Esther Wasira 0655 048797
Reactions::

8 comments:

Kijijini Bariadi said...
Wajameni,

Media na wanasiasa wa 'bongo' bana. Mbona tunakuwa wavivu wa fikra na uchunguzi kiasi hiki.

Hivi hawa watoto wana meriti gani au tofauti gani na mtoto mwingine wa mkulima ambaye anajiunga na CHADEMA kila kukicha mpaka Chama Makao Makuu kinatoa presi rilizi na kualika media kushuhudia Katibu Mkuu wa CHADEMA akiwapatia kadi za Uanachama wa CHADEMA.

CHADEMA Makao Makuu imeingizwa 'mkenge'. Haya ndiyo matokeo ya 'gutter politics'. Walifikiri kwa kufanya hivi watakuwa wamemshika ' pabaya'  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Mahusiano na Uratibu), Mh. Stephen Masato Wasira.
Hawa watoto nao, kwa kutaka ujiko usiokuwa na tija, walichekelea na kukubali kulifuta au kuliondoa jina la Baba yao mzazi ili kupata atesheni isiyo na tija yoyote kwao wala kwa familia yao.

Hii statimenti yao inaonyesha kuna mfukuto mbaya wa 'kindugu'. Who kea?. 'Bingo', Walionufaika na wanaoendelea kunufaika na minyukano hii ya kifamilia ni magazeti.

Kama kawaida 'Wabongo' tunaweza kupata medali ya dhahabu kwa kufanya mambo hovyo hovyo.

Why make statement?. Maji mmeyavulia nguo, hamna budi kuyaoga.
Anonymous said...
Wewe mchangiaji wa kwanza unachokiandika wala haujui unakulupuka tu. Baba yao walikuwa wanamtaja siku zote na huyo Stevin Wasira walikuwa wanasema ni baba yao ,dogo. Nadhani unajua unajua kuwa baba mdogo ni baba ingiwa hajakutoa tumboni.
Anonymous said...
Mnalo hilo esta na lili na bado hizo rasharasha tu mvua inakuja
Na nyie chadomo mbona mie mlivyoniipa kadi hamkuita waandishi auu kwaviile miiie Kayumba?
FlyingObject said...
STEVEN WASSIRA WAKULAUMIWA KATIKA HILI KWA SABABU HAKUWA NA SABABU YA KUSEMA HAWA SIO WATOTO WANGU WAKUWAZAA,BALI NI WATOTO WA KAKA YAKO KATIKA UTAMADUNI WA KIAFRIKA NA TANZANIA KUNA BABA MKUBWA MDOGO MJOMBA,KAKA ,N.K SASA KITENDO CHA YEYE KUKANUSHA HALAFU ANASEMA NAWAFAHAMU NI WATOTO WA KAKA YANGU,HAWA MAWAZIRI WA TANZANIA WAMELOGWA JAMANI????
Anonymous said...
Hivi tatizo ni jina? Kwani Steven ndo ana hali miliki ya jina la Wasira? Sioni tatizo la kumfanya waziri apayuke
Anonymous said...
Naomba kutofautiana na mada. Esther na Lily mmeolewa? Nahitaji mke mwanasheria...!
Anonymous said...
Mtajiju!
Anonymous said...
Tumeona watoto wa familia ya Nyerere wakiingia upinzani,lakini hawajafanya mbwembwe zozote,nyie vipi?acheni ushamba.

No comments:

Post a Comment