Simba Vs Yanga; Timu Ya Tatu iliharibu Mchezo!
Ndugu zangu,
Katika soka kuna timu tatu zinazocheza. Mojawapo ni timu ya waamuzi. Niliangalia kwenye runinga mechi ya leo. Nilichokiona; Waamuzi walichangia kuharibu mchezo. Nilichokiona-
1. Penalty waliyopewa Yanga haikuwa penalty. Beki yule hakukusudia. Mpira haukipigwa na mchezaji wa Yanga. Hata ungempita haukuwa ukielekea kwa mchezaji wa Yanga. Kama mimi ningekuwa refa, basi, ile haikuwa penalty.
2. Haruna Moshi Boban alipaswa kupewa kadi nyekundu moja kwa moja kwa rafu ile mbaya ambayo hata mlevi wa kilabuni hawezi kumfanyia mlevi mwenzake. Katika nchi za wenzetu, hata kama refa hakutoa kadi nyekundu, lakini, chama cha soka kingeweza kumpa adhabu ya kufungiwa zaidi ya mechi tatu.
3. Striker wa yanga, Bahanuzi alicheza kandanda safi sana. Alistahili kuwa Man of the Match. Nimependa uchezaji wake.
4. Mrisho Ngasa ni mchezaji mahiri, lakini, anahitaji kutumia misuli pia kukabiliana na mabeki kama akina Mbuyi Twite.
5. Juma Kaseja ni Juma Kaseja, Tanzania One, a World Class goalie. Nakumkubali Juma Kaseja. Cha kushangaza; Kocha wa Simba kumwingiza Boban uwanjani. Hata kama Yanga walibaki na wachezaji tisa uwanjani, na Simba nao walikuwa na wachezaji tisa uwanjani. Mpaka sasa najiuliza; Haruna Moshi aliingizwa uwanjani kufanya nini? Hakyamungu.
Maggid Mjengwa,
No comments:
Post a Comment