SUNDAY, OCTOBER 14, 2012
(Katika kumkumbuka Mwalimu Nyerere,
naileta makala yangu, "Mwalimu Nyerere Aliiogopa CCM," ambayo
nimeshaichapisha katika hii blogu yangu mara kadhaa)
Ingawa alikuwa mwanzilishi wa CCM, kwa nia njema ya kuendeleza mapinduzi katika
nchi yetu, miaka ilivyozidi kwenda Mwalimu Nyerere alishuhudia jinsi CCM
ilivyobadilika na kuwa mzigo kwake na pia tishio kwa usalama wa Taifa.
Mwaka 1993 Mwalimu alichapisha kitabu kiitwacho Uongozi Wetu na Hatima ya
Tanzania (Harare: Zimbabwe Publishing House, 1993). Pamoja na mambo mengine
katika kitabu hiki, Mwalimu alisema kuwa kuna kansa katika uongozi wa CCM.
Nanukuu baadhi ya maneno yake:
Chama cha Mapinduzi, kwa sababu ya uzito wa historia yake, hadhi ya jina
lake, mfumo wa wavu wake, mazoea ya watu, na ubovu wa Vyama vya Upinzani,
kinaweza kuchaguliwa na Watanzania, pamoja na kansa ya uongozi wake. Au watu
wanaweza wakachoka, wakasema, "potelea mbali:" wakachagua Chama cho
chote, ilimradi tu watokane na kansa ya uongozi wa CCM. Hainifurahishi kuyasema
haya, lakini uhai wa Nchi yetu unataka yasemwe. (Ukurasa 61)
Mwalimu hakuishia hapo, bali aliongezea namna hii:
Nilisema awali kwamba kansa ya uongozi ndani ya Chama cha Mapinduzi
isingekuwa ni jambo la kutisha sana kama tungekuwa tumeanza kuona Chama kizuri
cha upinzani kinachoweza kuiongoza Nchi yetu badala ya CCM. Ubovu wa uongozi
ndani ya CCM ndio uliofanya nikapendekeza tuanzishe mfumo wa Vyama Vingi.
Nilitumaini kuwa tunaweza kupata Chama kingine kizuri ambacho kingeweza
kuiongoza Nchi yetu badala ya CCM; au ambacho kingekilazimisha Chama cha
Mapinduzi kusafisha uongozi wake, kwa kuhofia kuwa bila kufanya hivyo
kitashindwa katika uchaguzi ujao. Lakini bado sijakiona Chama makini cha
upinzani; na wala dalili zo zote za kuondoa kansa ya uongozi ndani ya CCM. Bila
upinzani mzuri wa nje, na bila demokrasia halisi ndani ya Chama cha Mapinduzi,
Chama hiki kitazidi kudidimia chini ya uzito wa uongozi mbovu. Kwa hali yetu ya
kisiasa ilivyo nchini hili si jambo la kutarajia bila hofu na wasi wasi! (Ukurasa 66)
Ni wa-Tanzania wangapi wenye utamaduni wa kusoma vitabu? Ni wangapi wanaosoma
vitabu vya Mwalimu Nyerere? Ni wazi kuwa umbumbumbu miongoni mwa wa-Tanzania ni
neema kwa CCM.
Nakala hii
kwa hisani ya Hapa kwetu Blog
Ingawa alikuwa mwanzilishi wa CCM, kwa nia njema ya kuendeleza mapinduzi katika nchi yetu, miaka ilivyozidi kwenda Mwalimu Nyerere alishuhudia jinsi CCM ilivyobadilika na kuwa mzigo kwake na pia tishio kwa usalama wa Taifa.
Mwaka 1993 Mwalimu alichapisha kitabu kiitwacho Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania (Harare: Zimbabwe Publishing House, 1993). Pamoja na mambo mengine katika kitabu hiki, Mwalimu alisema kuwa kuna kansa katika uongozi wa CCM. Nanukuu baadhi ya maneno yake:
Chama cha Mapinduzi, kwa sababu ya uzito wa historia yake, hadhi ya jina lake, mfumo wa wavu wake, mazoea ya watu, na ubovu wa Vyama vya Upinzani, kinaweza kuchaguliwa na Watanzania, pamoja na kansa ya uongozi wake. Au watu wanaweza wakachoka, wakasema, "potelea mbali:" wakachagua Chama cho chote, ilimradi tu watokane na kansa ya uongozi wa CCM. Hainifurahishi kuyasema haya, lakini uhai wa Nchi yetu unataka yasemwe. (Ukurasa 61)
Mwalimu hakuishia hapo, bali aliongezea namna hii:
Nilisema awali kwamba kansa ya uongozi ndani ya Chama cha Mapinduzi isingekuwa ni jambo la kutisha sana kama tungekuwa tumeanza kuona Chama kizuri cha upinzani kinachoweza kuiongoza Nchi yetu badala ya CCM. Ubovu wa uongozi ndani ya CCM ndio uliofanya nikapendekeza tuanzishe mfumo wa Vyama Vingi. Nilitumaini kuwa tunaweza kupata Chama kingine kizuri ambacho kingeweza kuiongoza Nchi yetu badala ya CCM; au ambacho kingekilazimisha Chama cha Mapinduzi kusafisha uongozi wake, kwa kuhofia kuwa bila kufanya hivyo kitashindwa katika uchaguzi ujao. Lakini bado sijakiona Chama makini cha upinzani; na wala dalili zo zote za kuondoa kansa ya uongozi ndani ya CCM. Bila upinzani mzuri wa nje, na bila demokrasia halisi ndani ya Chama cha Mapinduzi, Chama hiki kitazidi kudidimia chini ya uzito wa uongozi mbovu. Kwa hali yetu ya kisiasa ilivyo nchini hili si jambo la kutarajia bila hofu na wasi wasi! (Ukurasa 66)
Ni wa-Tanzania wangapi wenye utamaduni wa kusoma vitabu? Ni wangapi wanaosoma vitabu vya Mwalimu Nyerere? Ni wazi kuwa umbumbumbu miongoni mwa wa-Tanzania ni neema kwa CCM.
Prof.Mbele nimeifurahia hii makala lakini pengine unaweza kuifafanua zaidi ni kwa vipi Baba Wa Taifa ambaye ndiye mwanzilishi wa TANU na baadae CCM aliiogopa CCM yake mwenyewe? najua katika wakati tofauti aliweza kukemea na hata kufanikiwa kubadilisha mwelekeo wa siasa za chama chake na Serikali pia;
ReplyDeleteNitashukuru sana kwa uchambuzi zaidi wa makala yako.