Na Mwandishi
Wetu
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba
amesisitiza umumihu wa wananchi kutoa maoni maoni yao kuhusu Katiba Mpya badala
ya kukimbilia kuwasilisha maoni waliyolishwa na viongozi wa vyama vya siasa,
asasi za kiraia na kidini.
Jaji Warioba ameyasema hayo leo (Jumanne, Oktoba 16, 2012)
katika mkutano kati ya Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala na uongozi
wa Tume hiyo uliofanyika katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam.
Kwa
mujibu wa Waziri Mkuu Mstaafu huyo baadhi ya viongozi hao na wadau wengine
wanadhani maamuzi ya kazi ya kukusanya maoni inayofanywa kwa sasa na Tume
yatamuliwa kwa kura na hivyo kuwalisha wananchi maoni ili wayatoa kwa Tume kwa
wingi.
“Wengine
wanafikiri huu ni wakati wa kupiga kura…hapana, sisi tunatafuta hoja,” alisema
Mwenyekiti huyo na kuwataka wadau mbalimbali kuwaacha wananchi watoe maoni yao
binafsi.
Awali akiongea katika mkutano huo, Mjumbe wa kamati hiyo ambaye
pia ni Mbunge wa Muhambwe, Bw. Felix Mkosamali alipendekeza Tume iwe inagawa
kwa wananchi fomu maalum za kujaza maoni yao siku kadhaa kabla ya Tume kufika
ili kuwapa wananchi fursa ya kuandika maoni kwa kina tofauti na sasa ambapo
Tume hutoa karatasi hizo kabla ya kuanza mkutano.
Akifafanua kuhusu hilo, Jaji Warioba amesema uamuzi wa Tume
kugawa fomu hizo mkutanoni unalenga kupata maoni binafsi ya wananchi na
kuongeza kuwa fomu hizo zikigawiwa mapema kuna uwezekano mkubwa kwa wananchi
kujaziwa maoni na watu wengine.
“Uzoefu
wetu umeonyesha hili la watu kuelekezwa nini cha kusema ambacho kwa kwli hawavijui
kwa kina,” alisema katika mkutano huo uliohudhuriwa pia na Naibu Waziri wa
Katiba na Sheria Angellah Kairuki, Katibu wa Tume hiyo Bw. Assaa Rashid na
Naibu Katibu Bw. Casmir Kyuki.
Pamoja na ufafanuzi kuhusu utoaji maoni binafsi ya wananchi,
Mwenyekiti huyo pia aliwaeleza Wajumbe wa Kamati hiyo kuwa lengo la
Tume ni kuhakikisha kuwa mchakato wote wa uandikaji wa katiba unakuwa wazi na
wananchi wanashiriki kikamilifu.
“Tukimaliza kukusanya maoni, tutaingia hatua ya pili ya Mabaraza
ya Katiba katika kila wilaya na baadhi ya taasisi ambapo tunataka wananchi
wenyewe katika maeneo husika wachague nani awawakilishe katika mabaraza hayo,”
alisema Mwenyekiti huyo.
Ufafanuzi huu ulifuatia swali la Mjumbe wa Kamati hiyo ambaye
pia ni Mbunge wa Kawe, Bi. Halima Mdee aliyeomba ufafanuzi kuhusu upatikanaji
wa wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ambayo yanapitia rasimu ya Katiba
itakayowasilishwa na Tume.
Akifafanua
zaidi, Jaji Warioba alisema Tume imepanga kufanya mikutano miwili katika kila
wilaya ambapo wawakilishi wa wananchi watajadili rasimu ya Katiba
itakayowasilishwa na Tume baada ya kukusanya maoni yao katika awamu ya kwanza.
“Ni hatua ambayo tunadhani itahitaji fedha nyingi hasa katika
kuwasafirisha hao wawakilishi wa wananchi kuja katika mikutano…hatutaki kuona
wananchi wanapata sababu ya kutoshiriki hatua hii muhimu,” alisema na kuwaomba
Wajumbe wa Kamati kuzingatia hoja hizo pale Tume itakapoomba fedha zaidi.
Pamoja na maoni hayo, Wajumbe hao pia waliieleza Tume umuhimu wa
kuongeza utoaji elimu kwa umma kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu Tume na
Katiba.
Kwa upande wake, Naibu Waziri Kairuki alisema Serikali
itaendelea kuipa Tume hiyo kila aina ya ushirikiano ili itekeleze majukumu yake
kwa ufanisi na kuwaomba Wabunge hao kuendeleza ushirikiano wanaoipa Tume hiyo.
Mwenyekiti wa
Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (kulia) akizungumza na
wajumbe wa kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala wakati wa ziara
iliyoanywa na wajumbe hao leo jumanne tarehe 16.Oktoba, 2012 ya
kutembelea vitengo mbalimbali vilivyopo katika Makao Makuu ya Tume hiyo Jijiini
Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angellah Kairuki na
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Pindi Chana.
Mwenyekiti wa
Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, (kulia) akibadilishana
mawazo na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, Pindi
Chana (katikati) wakati kamati hiyo iliyofanywa leo jumanne tarehe 16. Oktoba,
2012 na kutembelea vitengo mbalimbali vilivyopo katika makao makuu
ya Tume hiyo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria,
Angellah Kairuki.
Katibu wa Tume
ya Mabadiliko ya Katiba akibadilishana mawazo na wajumbe wa kamati ya Bunge ya
Katiba, Sheria na Utawala wakati wa ziara ya wajumbe hao iliyofanywa leo
jumanne tarehe 16.Oktoba, 2012 na kutembela vitengo mbalimbali vilivyopo katika
Makao Makuu ya Tume hiyo, Jijini Dar es Salaam. Kutoka Kulia ni wajumbe wa
Kamati hiyo, Rashid Ali Abdalla, Deogratius Ntukamazina, Naibu Waziri wa Katiba
na Sheria, Angellah Kairuki na Felix Mkosamali
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala wakitazama
namna ya Sauti zenye maoni ya wananchi zinazokusanywa kutoka Mikoa mbalimbali
nchini namna zinavyoweza kupokelewa katika Makao makuu ya Tume hiyo, Jijini Dar
es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Pindi Chana na wa pili kulia ni
Katibu wa Tume, Assaa Rashid. (Picha na Tume ya Katiba)
Habari kwa hisani ya Michuzi blog
bookmarked!!, I love your web site!
ReplyDeletemy web blog