MZEE YUSUFU
MAKAMBA ASEMA -CCM IMESAJILI KIKOSI SUPA LIGI YA MWAKA 2015
KATIBU Mkuu mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Luteni
Yusufu Makamba, amesema Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), ya Chama Cha
Mapinduzi(CCM) imefanya kazi nzuri kwa kuwa imesajiri supa timu ya kucheza ligi
ya mwaka 2015.Makamba ametabiri kuwa kazi nzuri iliyofanywa na NEC mjini Dodoma
wiki iliyopita itakiwezesha chama hicho kushinda kwa kishindo katika uchaguzi
mkuu wa rais na wabunge mwaka 2015.
Kauli hiyo aliitoa jijini Dar es Salaam jana
wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuzindua kisima cha maji
kinachomilikiwa na Kanisa la Anglikana Low Church Parishi ya Ukonga
Mazizini ambapo alialikwa kuwa mgeni rasmi.
“Nasema kama mwanachama wa CCM, lakini pia kama Katibu
Mkuu Mstaafu wa chama, tumesajiri wachezaji wa super ligi ya mwaka 2015,
wanaosemaCCM itakufa watakufa wao,”alitamba Makamba.
Aliongeza“Naamnini kuwa sisi tumesajiri vizuri,maana
usajili ni mzuri, kila aliyesajiliwa akipata nafasi ya kushinda afanye
yale yanayotakiwa”.Alisema katika uchaguzi huo wao walizingatia zaidi kuunda
timu itayochochea ushindi mwaka 2015 na si vinginevyo.
Wakati huo huo Makamba alihimiza mshikamano miongoni mwa
waamini wa kanisa hilo akionya kujiepusha na majungu na fitina kwa kuwa sasa
tabia hiyo mbaya imejikita mpaka makanisani.
Alisema licha ya kuwepo maandiko yanayowataka waumini
kutii mamlaka lakini wapo watu wanayapiga teke maandiko hayo na hivyo
kuwadharau wapakwa mafuta wa Mungu hadi kufikia hatua ya kumvua kofia wakiwa
madhabahuni.
“Siku hizi majungu na fitina vimeingia mpaka kanisani,
maandiko yanasema kutii mamlaka lakini watu wanamvua kofia hata
askofu,”alisema Makamba.Makamba alialikwa katika uzinduzi wa kisima hicho
kilichogharimu zaidi ya sh. milioni 10 kutokana kanisa hilo kuthamini mchango
wake.
Katibu wa Kanisa hilo Keneth Elia alisema Februari
26, mwaka huu Makamba alikuwa mgeni rasmi katika harambee ya kuchangisha fedha
kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa kisima hicho.Alisema Makamba alichangia
matanki mawili kila moja lina lenye ujazo wa lita 5000 na mabomba yaliyosaidia
kusambaza maji hayo.
No comments:
Post a Comment