WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Wednesday, October 10, 2012

Kwa nini Rais Park Chung Hee alifanikiwa baada ya kuingia madarakani?


MAENDELEO YA NCHI YANATEGEMEA SANA MAONO (VISION) YA KIONGOZI AMBAYE YUKO MADARAKANI.




Give a person a fish: you have fed the person for today.  Teach a person to fish: you have fed the person for a lifetime.”

Kumpa mtu samaki utakuwa umemlisha katika siku ya leo.ukiweza  Kumfundisha mtu  namna ya kuvua samaki  utakuwa umeweza kumsaidia kumlisha katika maisha yake yote.

Teach the person how to process and package fish for export and market it, and you have stimulated economic development.

Ukiweza kumfundisha mtu namna ya kutengeneza na kusafirisha na kuweza kuuza samaki katika masoko ya nje; utakuwa umefanikiwa kuchochea maendeleo ya kiuchumi

Park Chung Hee alikuwa kiongozi wa Korea ya Kusini kuanzia mwaka 1961-1970 alipo uwawa.Park Chung Hee alikuwa dikteta lakini alikuwa Rais ambaye alifanya Korea ya Kusini leo hii kuonekana tajiri. Alipoingia madarakani mwaka 1961 alikuwa na vision na vipaumbele ya maendeleo ya nchi yake kwa kutilia mkazo maendeleo ya  Elimu, kukuza technologia (ICT),Kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanakuwa na nidhamu ya kazi (dicpline) na kusimamia ukaaji wa Nishati.


Kwa taathimini ya kiuchumi wakati Park anaingia madarakani uchumi wa Korea ya Kusini ulikuwa sawa na  hali ya uchumi tunaoulaamikia sisi watanzania yaani uchumi duni na maisha magumu;

Kutokana vision na uzalendo wake kwa kujitoa kwa utendaji bora  na usimamiaji bora wa rasilimalia za taifa lake  leo hii Korea ya Kusini ni moja ya nchi zenye uchumi imara dunia na inashindana na hata kuogopewa na nchi ambazo ni tajiri duniani.

Ni takribani zaidi ya miaka 30 toka alipouwawa lakini tafiti zinaonyesha kuwa amebaki kuwa na rekodi bora ambayo imeisaidia nchi yake katika umaarufu ambao Korea ya Kusini inafurahia leo; Park alisaidia sana katika kusimamia ukuaji wa uchumi na usambazaji wa kasi  wa uwiano wa kipato, ikilinganishwa na mataifa mengine.  Kwa usimamiaji wake bora wa maendeleo kwa wote, Rais Park ilijulikana kama "unforgettable" miongoni mwa Wakorea kwa sababu ya ujuzi wake na nguvu ya usimamiaji wa maendeleo kwa wote.

Kwa nini alifanikiwa katika kuboresha uchumi wa nchi yake?

Rais Park alikuwa na tabia moja mimi naiona ni nzuri ambayo iliwashangaza waandishi wengi  ndani ya ofisi yake kuwa kuta zilitapakaa na michoro ya takwimu, ikiwa ambazo zilikuwa zikionyesha  mwenendo wa biashara, ukusanyaji wa kodi na taarifa za maendeleo ya viwanda ambayo katika nchi yeyote ile ni nguzo imara ya maendeleo. Kiongozi yeyote mwenye  maono ya  namna hii lazima awe kiongozi bora kwa maendeleo ya nchi yake.

Swali hapa viongozi wetu wanatumia muda wao mwingi wakiwa ofisini wanakuwa wanangalia data za aina gani? 
Kusoma magazeti

Je viongozi wetu wanakuwa na muda wowote wa kufuatilia ukuaji wa uchumi wa taifa kupitia ofisi zao?

Jambo jingine ambalo ni msingi sana ambalo pengine viongozi wetu wanatakiwa kulitilia mkazo wanapo yaangalia maendeleo ya kiuchumi kwa nchi yetu kwa  kuendelea kutilia mkazo katika kujenga uwezo wa kiufundi unaotokana na elimu ubora katika fani ya sayansi na teknolojia. Uwezo wetu wa kiufundi ni nguvu itakayo weza kutoa njia kadhaa za maendeleo ya kiuchumi na  mvuto wa makampuni ya kitaalam ya kimataifa kuwekeza ndani ya Taifa letu kwa faida ya Taifa:

Kama taifa “pengine” tuna tunatumia misaada vibaya, lengo la misaada ambayo nchi Hisani hutoa kwa taifa ni katika katika kutatua kero ya uchumi unaotusumbua na na kuyafanya maisha ya watanzania kuendelea kuwa duni. Matumizi bora ya misaada ya kigeni, katika miradi ya miundombinu sahihi ni suluhisho namba moja wa umasikini wetu.


Watendaji wetu kuanzia Kiongozi wa juu kabisa wa Serikali yaani Rais na wengine wote wanaomfuata wanatakiwa wawe na uwezo wa Kujenga kuboresha uchumi, kupitia sera za mitazamo yakimaendeleo kwa kukuza mifumo ya kiutawala na sera zinazolenga zaidi katika kusimamia maisha na ukuaji wa uchumi wa nchi.

Nimejaribu kueleza hayo yote ili kuonyesha kuwa bila kuwa na uongozi wenye maono usiotafuta faida yake wenyewe, usiokuwa tayari kuwawajibisha watendaji wabovu na wanaokiuka maadili uvunja sheria  hatuwezi kutoka hapa tulipo, tutaendelea kufurahia  kauli mbiu ambazo hazina maana wala msingi mkubwa kwa maendeleo ya Taifa. Kama historia inavyo onyesha kuwa  Rais Park aliingia madarakani kwa kupindua uongozi ulikuwa madarakani lakini lengo lake lilikuwa maendeleo ya Korea kusini katika hali yeyote na alifanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kipindi chake kama kiongozi wa nchi.

Je kwa nini sasa Nchi yetu tunafarijika ndani ya demokrasia lakini tunashindwa kuwaletea maendeleo wananchi wake?

Kama taifa viongozi wetu wangeweza kuiga namna bora ya usimamiaji katka kutekeleza majukumu yao:

Swali la msingi je kuna tija au mabadiliko yeyote yanayotokana na utaratibu huu wa usimamiaji?

Tofauti na Rais Park yeye alikuwa na wasiwasi mkubwa katika kupima matokeo,na alikuwa hana mchezo hata kidogo katika hili alikuwa hana msamaha kwa wale wote ambao hawakufikia malengo ambayo alikuwa amewapangia wengi waliathibiwa kwa kufukuzwa kazi bila huruma na hii ilikuwa inatoa changamoto kwa wale wote ambao walikuwa wamekabidhiwa madaraka kwa ajili ya Taifa kuwa wawajibikaji. kwani ufanisi ulukuwa unapimwa kwa uwajibikaji na sio propaganda za kisiasa.

Serikali yetu ina hili tatizo la ufuatiliaji na uwajibishaji wa mara moja; uwajibikaji na uwajibishaji hauko katika kamusi yaviongoziwetu. pengine hili linatokana na namna watendajiwanavyopatikana; Je watendaji wetu wanapatikanaje?kupitia elimu yao? utashi wa kisiasa wa chama kilicho madarakani? au kwa misingi ya urafiki na undugu?

kama majibu ya maswali hapo juu yatalenga zadi katika utashiwakisiasa, urafiki na undugu basi uwajibishai wowote utafanyika baada ya shinikizo kubwa kutoka kwa wananchi; na vision za viongozi wetu zitabaki zaidi za kwenye makaratasi ambazo zinakosa sana kipaumbele na kuthubutu.

Je baraza jipya litaleta ufumbuzi wa tatizo la umasikini?

 “watanzania wana matumaini makubwa na serikali yetu, tusiwaangushe. Njia pekee kwetu sisi ya kutowaangusha ni kufanya kazi kwa bidii”.

Nionavyo mimi Katika baraza la jipya tunao Mawaziri ambao wanaweza wakaivusha Tanzania  na kupeleka katika nchi ya ahadi iliyojaa maisha bora kwa kila mwananchi. mawaziri kama Dr.Mwakyembe, Prof. Tibaijuka, Sitta na kadhalika.

Ngoja nimchambue kidogo utendaji mzuri wa Dr. John Pombe Magufuri,   pamoja na mapungufu yake kama binadamu; Magufuri ni miongoni mwa viongozi wachache ambaye daima huwa anathubutu  na daima amekuwa akijielemisha ili kuzielewa zaidi sheria za nchi na wizara husika;  ni msimamiaji mzuri wa sheria katika utendaji wake  sio mnafiki katika utendaji wake hata kama wakati mwingine maamuzi yake yanakuwa kero kwa kwa watendaji wenzake na wananchi ambao wanakiuka sheria za nchi na zinasababisha utumiaji wa nguvu na ugumu wa utendaji na utoaji wa hudumu ya uhakika kulingana na sera au maagizo ya serikali kuu;

Kimsingi kama nilivyoainisha hapo juu inawezekana magufuli akawa na madhaifu yake lakini huwezi kuondoa ukweli kuwa ni miongoni mwa mawaziri wachache sana ambao tunao wanaofanya vizuri kazi za kusimamia hata kuchukua hatua kali kwa wakati. Hilo hata wananchi wa kawaida wanalijua na jamii ndio inayo msafisha daima.

Angalia jinsi anavyosimamia sheria namba 18 ya mwaka 2007 ambayo ilisainiwa na Rais mwenyewe ambayo inakataza watu kuingilia eneo la hifadhi ya barabara kwa kujenga makazi au kufanya biashara; pamoja na Mheshimiwa Rais na waziri Mkuu kumpunguza kasi lakini msimamo wake uko pale pale.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Sadiki aliwahi sema kuwa “Hatukatai hata kama ana upungufu wake, basi apewe sifa katika yale mazuri anayoyafanya, lakini ukweli ni wazi kuwa Magufuli ni kiongozi mchapakazi na msimamizi mzuri wa sheria na hilo halipingiki,” Akiendeleza sifa hizo Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka, alisema siku zote utendaji kazi wa Magufuli unafuata sheria na taratibu “Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, wengi tunamtambua Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya, tunakuomba uendelee kufanya hivyo hivyo wala hutofeli na ukiendelea na moyo huo sote hatutafeli,” aliongeza Kabaka.

Tunacho washauri Mawaziri katika baraza hili jipya wanatakiwa wachukue tahadhari mapema wasiendelee kufanya kazi na watendaji wabovu; Kumbuka, samaki mzuri akichanganyika na samaki waliooza lazima achafuke uvundo.Mawaziri wetu wanatakiwa wajipange upya waache porojo za kujitetea kwa maneno wajitete kwa vitendo ambavyo vina tija kwa wananchi kwa maendeleo ya Taifa; Tuna imani na nanyi kama mawaziri wapya  tunawatakieni kila la kheri na fanaka katika kumsaidia mheshimiwa Rais wetu katika  kutimiza kauli mbio ya maisha bora kwa wote.


Viva baraza letu la mawaziri tunaamini kuwa baraza hilo litakuwa la kiutendaji zaidi. Litachukua mazuri ambayo Rais Park wa korea ya kusini aliyatumia katika kuboresha uchumi wa nchi yake. Nafikiri inawezekana kuiga na kuleta katika tamaduni yetu kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu.

No comments:

Post a Comment