WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Friday, October 5, 2012

Harakati Za Dijitali Zanzibar



Na Ali Issa-Maelezo Zanzibar 05/10/2012 

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Habari Utamaduni ,Utalii na Michezo imeiteuwa kampuni ya Agape Associates LTD kufanya kazi ya kuweka miundombinu ya matangazo ya mfumo wa Digitali ili kuwahi tarehe ya mwisho ya matangazo ya Analogi ambayo ni 31 Disemba mwaka huu kama ilivyokubaliwa kwa nchi za Maziwa makuu. Aidha wizara imemteuwa Hassan Katetei Mdachi kutoka Kampuni ya Thornhead Engineering System,kutoka nchini Kenya kuwa Mshauri elekezi katika kufanikisha shughuli hiyo. 

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Habari Utamaduni ,Utalii na Michezo Saidi Ali Mbaruok wakati alipokuwa akizindua Kikosi kazi kitakachosimamia uwekaji wa miundo mbinu wa mtambo wa DIJITAL-ZBC huko Ofisini kwake Kikwajuni Mjini Zanzibar. Katika uzinduzi huo amesema amelazimika kuunda kamati kwani mfumo wa dijital harakati zake ni kubwa na za muda mfupi kufikia lengo ,hivyo kamati hiyo itafuatilia kwa karibu mahitaji ya dijital ili wananchi waweze kufaidika na huduma zake kwa wakati. Kamati hiyo itakuwa na lengo la kufuatilia na kusimamia kwa karibu shughuli za uwekaji wa mitambo ya dijital katika vituo vyote vya unguja na Pemba.
 Waziri Said Mbarouk amesema majukumu mengine ni pamoja na kusimamia utaratibu utakao weza kupatikana Ving’amuzi pamoja na njia zitakazo weza kurahisisha wananchi kuvipata kwa wakati pamoja na kuanda na kusimamia upatikanaji wa mandhari kwakuzingatia misingi ya kibiashara ,mila ,silka na hali ya ushindani iliopo . 

Ameyataja majukumu mengine ya Kamati hiyo kuwa ni pamoja na kubuni njia bora zitakazo saidia mtandao wa dijital kufanya kazi kwa ufanisi na kujitegemea. Katika uzinduzi huo Katibu Mkuu wa Wizira ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Ali Saleh Mwinyikai aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa Kamati hiyo yenye wajumbe 13.
                               Imetolewa na Idara ya Habari Maelezo Zanzibar

No comments:

Post a Comment