WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Monday, March 31, 2014

Yanga, Simba aibu yetu, aibu yao...

Mshambuliaji wa Simba, Amis Tambwe (kushoto) akiwania mpira na beki wa Azam, Aggrey Morris wakati wa mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Azam ilishinda 2-1.
Dar es Salaam. Azam imezidi kunyemelea ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu baada ya kuichapa Simba 2-1, huku mabingwa watetezi Yanga wakichapwa 2-1 na wachezaji 10 wa Mgambo Shooting kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Mabao ya Hamisi Mcha na John Bocco yalitosha kuipa Azam pointi tatu muhimu na kuongoza ligi kwa pointi 53, huku beki Joseph Owino akifunga bao la kufutia machozi kwa Simba.
Nayo Mgambo wakicheza zaidi ya dakika 60 wakiwa pungufu waliwaduwaza Yanga kwa kuwachapa 2-1. Mgambo walikuwa pungufu baada ya beki wao Mohamed Netto kutolewa kwa kadi nyekundu katika dakika ya 30 na mwamuzi Alex Mahaji aliyehisi mchezaji huyo amevaa hirizi katika nguo yake ya ndani, lakini alipokaguliwa haikuonekana. Mabao ya Mgambo yalifungwa na Fully Maganga na Malima Busungu.
Wakati Yanga wakisuasusa na pointi 46, Mbeya City imejiimarisha katika nafasi ya tatu kwa kufikisha pointi 45, baada ya kuwafunga ndugu zao Prisons kwa bao 1-0.
Katika Uwanja wa Taifa; Mcha aliwainua mashabiki wa Azam dakika ya 16 akiunganisha krosi kutoka upande wa kushoto baada ya wachezaji wa Simba, Donald Musoti na Amis Tambwe kugongana walipokuwa wakijaribu kumzuia Tchetche na kutoa mwanya kwa mfungaji kupiga shuti lililomwacha kipa Mapunda asijue la kufanya.
Simba walisawazisha bao hilo dakika ya 45 baada ya mpira wa adhabu uliopigwa na William Lucian kutua kichwani kwa Joseph Owino na kuifungia Simba bao hivyo timu hizo kwenda mapumziko zikiwa 1-1 huku mashabiki wa Yanga waliojitokeza uwanjani wakiishangilia Simba kwa nguvu.
Kipindi cha pili, Azam walimtoa Mcha na kumwingiza Kelvin Friday dakika ya 52, mabadiliko yaliyokuwa na faida kubwa kwao kwani dakika mbili baadaye Bocco aliifungia bao la pili akiunganisha mpira uliopigwa na Tchetche na kugonga mwamba na kurudi uwanjani.
Mjini Tanga mshambuliaji Fully Maganga aliifungia Mgambo Shooting bao la kuongoza dakika ya kwanza kwa kichwa akiunganisha mpira uliokuwa umepigwa na kipa Juma Kaseja kwenda kwa Kelvin Yondani.
Hata hivyo, katika mechi hiyo, Mgambo walipata pigo baada ya Mohamed Netto kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 30 na mwamuzi Alex Mahaji aliyehisi mchezaji huyo amevaa hirizi katika nguo yake ya ndani, lakini haikuonekana.
Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub aliifungia timu yake bao la kusawazisha kwa mkwaju wa penalti dakika ya 51 baada ya beki wa Mgambo, Novart Lufunga kumchezea vibaya mshambuliaji wa Yanga kwenye eneo la hatari. Hii ni mara ya tatu kwa Yanga kushindwa kupata ushindi inapocheza dhidi ya timu pungufu, walitoka 0-0 na Mtibwa na sare 1-1 na Azam. Busungu aliipatia Mgambo bao la pili kwa mkwaju wa penalti dakika ya 66 baada ya Kelvin Yondani kumwangusha kwenye eneo la hatari.
Katika Uwanja wa Sokoine Mbeya mshambuliaji  Paul Nonga aliipatia Mbeya City bao la kuongoza dakika ya pili baada ya kuwazidi mbio mabeki wote wa Prisons na kufunga bao hilo lililoamsha shangwe.
Morogoro; Katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Manungu, wenyeji Mtibwa  Sugar walienda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 3-1, shukrani kwa mabao ya Jamal Mnyate dakika ya 14,  Mussa Hassan Mgosi (30), na Mohamed Mkopi (81), huku Behewa Behewa akiifungia Coastal Union dakika ya 16
Imeandaliwa na Sosthenes Nyoni (Dar), Yakubu Burhani (Tanga) Godfrey Kahango (Mbeya), Juma Mtanda (Morogoro).

source: Mjengwa blog 

No comments:

Post a Comment