WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Friday, March 7, 2014

Mbowe alaani utovu wa nidhamu bungeni

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba,Freeman Mbowe.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Freeman Mbowe, amelaani vitendo vinavyofanywa na baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo kwa kushindwa kuonyesha nidhamu ndani ya Bunge hilo.
Mbowe alitoa kauli hiyo jana muda mfupi mara baada ya Mwenyekiti wa Muda, Pandu Ameir Kificho kuahirisha semina ya kujadili kanuni kutokana na vurugu.

“Nasikitishwa na kiti kutoweza kufanya kazi yake kwa uzalendo na kuachia watu wafanye vile ambavyo wanavifanya ikiwa ni pamoja na kupinga hoja za wabunge ambao wanachangia kwa misingi ya vyama vyao.

“Siwezi kupongeza kabisa jinsi ambavyo vikao vinaendeshwa mbaya zaidi ndani ya vikao kuna watu wazima ambao wanapoteza heshima zao kwa kuwazomea wenzao na kuwapinga kwa kujenga taswira ya imani za vyama vyao,” alisema.

Alisema kinachomuumiza zaidi ni kuona muda unavyopotezwa badala ya kujadili mambo ya msingi watu wanajipanga kukwamisha mjadala huo.

“Kimsingi, mimi na watu wengine tulitegemea kuwapo kwa majadiliano ya kujidali ni jinsi gani ya kupiga kura na kuweza kumpata mwenyekiti wa kudumu kama tungemaliza ili kujadili wiki ijayo watu angeanza kuapa ili kazi za Bunge zianze rasmi, lakini kwa mtindo huu ni wazi kuwa tunapoteza muda katika mambo ambayo hayawezi kuwasaidia Watanzania,” alisema.  

Aidha, alisema kuna udhaifu mkubwa wa kiti kutokana na kushindwa kusimamia masuala mbalimbali ndani ya Bunge hilo.

“Kiti kinayumba kwa kiasi kikubwa na kinayumba kutokana na misingi ya upendeleo, lakini pamoja na kuyumba kwa kiti wajumbe tuna haki ya kuheshimiana na pale mjumbe anaposimama hututegemei kuona mjumbe mwenye sifa ya kuitwa mjumbe na kuanza kumzomea mwenzake,” alisema.

 Alisema jambo ambalo linafanyika ndani hata kama Mwenyekiti Kificho anakosema hakukutakiwa kuwa na sababu ya wajumbe kuzomea.

“Hakuna sababu ya kuzomea, sisi watu wazima na akili zetu tunasimama ndani ya Bunge tunazomeana halafu tunashindwa kufikia maamuzi yale ambayo tumeazimia ndani ya bunge letu hii ni kupoteza muda na fedha za walipa kodi,” alisema Mbowe.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment