WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Friday, March 14, 2014

Wajumbe Bunge Maalum la Katiba waapishwa Mjini Dodoma



Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Samwel Sitta akila kiapo mbele ya  Katibu wa Bunge hilo Bw. Yahya Khamis Hamad, wakati wa hafla ya kuwaapisha wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mjini Dodoma.Kulia ni Naibu Katibu wa Bunge Hilo Thomas Kashilila.

>Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samia Suluhu Hassan akila kiapo mbele ya Naibu Katibu wa Bunge Hilo Thomas Kashilila, wakati wa hafla ya kuwaapisha wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba leo Mjini Dodoma.Kulia ni Katibu wa Bunge Hilo Yahya Khamis Hamad.

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambaye ni Mwanasheria Mkuu Frederick Werema akitoa hoja wakati wa hafla ya kuwaapisha wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mjini Dodoma.

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na aliyekuwa Mwenyekiti wa Muda wa Bunge hilo Pandu Ameir Kificho akila kiapo cha kuwa Mjumbe wa Bunge Hilo Mbele ya Mwenyekiti wa Bunge Hilo Samwel Sitta.

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda akila kiapo cha kuwa Mjumbe wa Bunge Hilo Mbele ya Mwenyekiti wa Bunge Hilo Samwel Sitta.

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Edward Lowassa akila kiapo cha kuwa Mjumbe wa Bunge Hilo Mbele ya Mwenyekiti wa Bunge Hilo Samwel Sitta.
 
source: mjengwa blog

No comments:

Post a Comment