WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Wednesday, March 12, 2014

Werema, Jussa wamfagilia Lissu

Mwanasheria mkuu wa serikali,Jaji Fredrick Werema.
Mwanasheria mkuu wa serikali, Jaji Fredrick Werema, amemfagilia mjumbe Tundu Lissu, kuwa mahiri katika sheria na amefanyakazi nzuri kama ambayo angeifanya yeye (Werema) ndani ya Bunge.

Akizungumza na NIPASHE, Werema, alisema Lissu alikuwa akifanya sheria na kutoa elimu kwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kwa umahiri mkubwa sana na kuifanya kazi ya kanuni hizo kuwa nyepesi.

"Kuridhiana na kukubaliana kwa kufanya kazi kwa pamoja ni muhimu sana,  hata wakati sipo, lakini kutokana na kuelewana Lissu aliweza kufanya shughuli ambazo huwa nafanya ndani ya Bunge kawaelewesha wajumbe kuhusu sheria na amejibu maswali mengi vizuri,” alisema.

Lissu na Werema ni wajumbe wa Kamati ya Kanuni na Kumshauri Mwenyekiti ambayo ilikuwa na jukumu la kupitia, kujadili na kurekebisha kanuni zilizoletwa na Ofisi ya Bunge ili ziweze kutumika kuongoza Bunge Maalum la Katiba.

Mjumbe wa kanuni hiyo, Ismail Jussa Ladhu, alisema kukamilika kwa kanuni hizo kwa kiasi kikubwa kumewezeshwa na umahiri wa Lissu kwa kutumia elimu yake, kusoma sana, kutafiti na utundu alionao.

”Waheshimiwa wajumbe msione kanuni hizi zimekamilika kwa kiasi hiki, Lissu amefanya kazi kubwa sana ya kutumia taaluma yake kuhakikisha tunapata kanuni bora za kuongoza Bunge hili,” alisema Jussa.

 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment