WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Friday, March 14, 2014

RAIS KIKWETE KUHUTUBIA BUNGE LA KATIBA WIKI IJAYO





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuhutubia bunge Maalum la KATIBA Kati ya Jumanne na Jumatano wiki ijayo.

Mwenyekiti wa bunge Maalum la KATIBA Mheshimiwa Samuel Sitta ameliambia bunge Mara baada ya kuapishwa na kukabidhiwa kiti chake leo jioni.

Amesema kazi ya kuwaapisha wabunge wote iliyoanza leo jioni itakuwa ikifanyika hadi saa 3 usiku na kukamilika Jumapili.

Jumatatu wiki ijayo saa 10 jioni bunge hilo litakabidhiwa rasmi rasimu ya katiba na mwenyekiti wa bunge la Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba.

Mheshimiwa Sitta ameliambia bunge Maalum la KATIBA kuwa wabunge watakuwa NA mjadala wa Jumla kwa siku Tatu kuhusu malengo NA muelekeo aw KATIBA mpya kabla ya kugawanyika katika Kamati mbali mbali kwa kazi rasmi.

Mwenyekiti Sitta amemshukuru na kumpongeza aliyekuwa Mwenyekiti wa muda wa bunge Hilo Mheshimiwa Pandu Ameir Kificho kwa ustahimilivu, busara, hekima NA uvumilivu aliouonyesha wakati akiliongoza bunge hilo kuandaa kanuni zake kwa kipindi cha wiki Tatu.

Amesema kazi ya kuandaa kanuni ilifanywa bila kanuni hivyo baadhi ya wabunge walitumia fursa hiyo kufanya vitendo visivyokubalika. 

Amewakumbusha wabunge kuwa kanuni zimepatikana NA hivyo wazifuate vinginevyo wasije wakamlaumu pale atakapochukua hatua kwa ukiukwaji aw kanuni hizo.

Akiwaaga wabunge aw bunge Hilo, Mheshimiwa Kificho amewaasa wabunge aw bunge Hilo kuwa na hekima, busara, subira NA hoja zenye mashiko wakati wakifanya kazi hiyo NA kuangalia zaidi maslahi ya taifa ili kuwapatia wananchi KATIBA ambayo haitawagawa bali itakayoimarisha umoja NA mshikamano wao.

Mheshimiwa Sitta na Makamu wake Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan wameapishwa leo jioni na Katibu wa Bunge la Katiba
Bw. Yahya Khamis Hamad aliyekuwa na Naibu wake Bw. Thomas Kashililla.

Imeandikwa na Zamaradi Kawawa, MAELEZO, Dodoma, Machi 14,2014.

No comments:

Post a Comment