WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Thursday, March 13, 2014

MHESHIMIWA SAMIA SULUHU HASSAN AMECHAGULIWA KUWA MAKAMU WA MWENYEKITI WA BUNGE LA KATIBA



Waziri wa Nchi Ofisi ya MAKAMU wa Rais anayeshughulikia Muungano Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amechaguliwa kuwa MAKAMU wa Mwenyekiti wa Bunge la Katiba.

Mheshimiwa Samia anaingia katika kitabu cha historia kwa kuwa mwanamke wa kwanza kuwa makamu wa Mwenyekiti wa Bunge la kwanza la kuandaa KATIBA Mpya ya Tanzania baada ya kupata kura 390 sawa NA asilimia 74.6 ya kura zote 523 zilizopigwa NA wajumbe wa bunge hilo NA kumshinda mpinzani wake Mh. Amina Abdallah Amour wa Chama cha CUF aliyepata kura 126 sawa NA asilimia 24.1 ya kura zote. Kura 7 ziliharibika.

Mh. Samia Suluhu Hassan ni msomi mwenye Stashahada ya Uzamili (Masters Degree) ya Maendeleo ya Jamii katika Uchumi. Amekuwa Waziri katika WIZARA mbali mbali 3 katika kipindi cha miaka 14 Kama mjumbe wa Baraza la Wawakilishi na Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano .

Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameliambia bunge la KATIBA wakati akijibu maswali ya wajumbe kuwa Amekuwa Waziri katika Ofisi ya MAKAMU wa Rais anayeshughulikia Muungano kwa miaka 4 ambapo ameweza kushughulikia kero zote 13 za Muungano isipokuwa moja inayohusu uchumi.

SOURCE: A. HAMIS

No comments:

Post a Comment