
Rais Jakaya Kikwete, akiwahutubia Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba leo katika ukumbi wa Bunge mjini Dodom, ambapo katika hotuba yake ametumia dakika 155:46, kwa kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali yahusuyo muundo wa Katiba mpya ikiwa ni pamoja na kufafanua kuhusu shinikizo la muundo wa Serikali tatu na mambo kadhaa ya Muungano.

Wajumbe wakinyanyuka kwa pamoja na kupiga makofi kumshangilia Rais Jakaya, baada ya kukonga kwa Speech yake.

Sehemu ya Wajumbe waliohudhuria .....

Sehemu ya Mabalozi waliohudhuria ufunguzi huo wa Bunge la Katiba katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo jioni.

Mama Maria Nyerere (katikati) Mama Siti Mwinyi (kushoto) na Mama Salma Kikwete, wakiwa ukumbi humo wakimsikiliza Rais Jakaya Kikwete.

Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal (kushoto) Mama Tunu Pinda na Mama Asha Seif Balozi, pia wakifuatilia hotuba hiyo kwa makini.

Rais Jakaya Kikwete, akikagua gwaride maalum kabla ya ufunguzi rasmi wa Bunge hilo.

Badhi ya waandishi wa habari wapiga picha wakiwa bize.

Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta na Makamu wake, Samiah Suluhu, wakijadiliana jambo wakati wakisubiri kuwapokea viongozi.

Waandishi na watu mbalimbali wakiwa nje ya ukumbi huo wakati wa maopokezi ya viongozi mbalimbali.

Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu, akiwasili kwenye viwanja vya bunge.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye viwanja vya Bunge.

Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Samuel Sitta, akiwasili kwenye viwanja vya Bunge.

Baadhi ya waandishi.....

James Mbatia akiwasili na mjumbe mwenzake....Picha zote na Ofisi ya Makamu wa Rais
source; mjengwa blog
No comments:
Post a Comment