WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Tuesday, May 7, 2013

Rais Shein aeleza faida za Mwenge wa Uhuru

 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein, amesema ipo haja ya Mwenge wa Uhuru  kurithiwa kizazi hadi kizazi kutokokana na falsafa safi aliyoileta raisi wa kwanza wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Nyerere.
Alisema falsafa hiyo ilieleza kwamba Mwenge unawashwa ili ulete matumaini palipojaa dharau na chuki; na kudumisha umoja na mshikamano miongoni mwa Watanzania   

Dk. Sheni alitasema hayo alipokuwa akiwahutubia umati mkubwa wa wananchi waliofika katika viwanja vya Chokocho katika sherehe za uwashaji wa mbio za mwenge wa uhuru.

Alisema Watanzania hawanabudi kuthamini mbio za Mwenge wa Uhuru kwani zimeleta heshima kubwa kwa Watanzania ndani na nje ya nchi na kwamba malengo na maudhui ya kuwashwa kwa Mwenge huo yana faida makubwa kwa Watanzania. 

Alisema kuwa mbio hizo zina historia na umuhimu mkubwa kwani zimeanzishwa na wasisi wa Taifa yaani hayati Nyerere na hayati Abeid Amani Karume.

Alifafanua kuwa tokea kuwashwa kwa Mwenge huo miaka kadhaa iliopita Tanzania imekuwa ni nchi ya historia kuwa ni nchi ya amani barani Afrika, kwa vile Mwenge umeacha maeneo ya hekima ambayo yalitolewa na hayati Mwalimu Nyerere, wakati alipoanza kuuwasha Mwenge huo mwaka 1967.
 
CHANZO: NIPASHE 
uchambuzi wa ukadirifu kuhusu mwenge wa uhuru
 
 http://2.bp.blogspot.com/-xiEl_FEB75M/UYiXdWnnv0I/AAAAAAAAqaY/Jh4cfwR71lE/s640/2-dr,+shein+akimkabidhi+mwenge+kiongozi.JPG


 

Mwalimu Julis Kambarage Nyerere  falsafa yake kuhusu mwenge ilikuwa kama ifuatavyo;, “Sisi Watanganyika, tunataka  kuuwasha mwenge na kuuweka juu ya mlima Kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini pale ambapo hakuna matumaini, upendo pale ambapo pana chuki, heshima ambapo pamejaa dharau”.Mwenge huo uliwashwa  Siku ya uhuru wa Tanganyika Desemba 9, 1961, Baba wa Taifa aliwasha Mwenge na baadaye ukapelekwa kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro

Je mwenge huu ulikuwa na maana gani kwa Taifa?
·  kwa ufupi, ulikuwa ni alama ya uhuru wetu kuona mapungufu yetu sisi wenyewe katika ujenzi wa Taifa letu

· Falsafa hiyo inalenga kuwaunganisha Watanzania, unatumika kukemea waovu, unatumiwa na serikali kupitisha ujumbe na kuzindua miradi ya maendeleo inayoleta matumaini kwa Watanzania

 

· mwenge ulikutumika kuhimiza uzalendo, kuhimiza uwajibikaji, kueneza ujumbe juu ya athari za rushwa, ukimwi, uzembe na kadhalika;
·       Mwenge ni ishara ya mshikamano wa udugu wa kitaifa 

· Mwenge ametumika kama chombo cha kuchochea maendeleo kupitia kauli mbio yake amabyo imekuwa ikitolewa kila mwaka  na tukizingatia kuwa mwenge unafika katika kila kona ya nchi yetu. JE MALENGO YA MWENGE WA UHURU YAMEONYESHA MAFANIKIO?

· Mwenge umekuwa ukitukumbusha kuhusu kuthamini uhuru wetu kama taifa ambalo tunatakiwa kusimama imara  kwa kuzingatia misingi ya imani upendo, amani na utulivu.·        Mwenge pamoja na tofauti zetu za makabila, dini na vyama vya siasa sisi kama Watanzania  katika kipindi hiki cha zaidi ya miaka 50 bado tunahimizwa  kusimama kama Taifa moja na kuhakikisha kuwa Taifa letu haliyumbishwi na  watendaji wabovu, wazembe, wala Rushwa, Mafisadi na wanaoeneza chuki za kuligawa Taifa kwa njia yeyote ile iwe ni Dini, Ukabila au Vyama vya siasa.

·  Katika kusherekea Mwenge wa Uhuru falfasa ya Mwenge inatakiwa ibaki imara ila utekelezaji wake unatakiwa kubadilika kulingana na hali  halisi ya vyama vingi, upana wa demokrasia, na uzembe wa uwajibikaji;
 


·Sheria inatakiwa iendelee kufuatwa na wale wote wanaovunja sheria wachukuliwe hatua kali bila kujali nafasi zao kwa kufanya hivyo tutafanikiwa kurejea   nuru yake ile ile tukapousimika tena tarehe 9 december 2011, kilele katika Mlima Kilimanjaro;

·   Mwenge kwa sasa uwamulike ; wabadhirifu, wazembe maofisini, wala rushwa magendo  uwajibikaji ni dhana ambayo kwa sasa kama Taifa tunaihitaji sana

· Mheshimiwa Rais wa Awamu ya Nne Dr. Jakaya Mrisho Kikwete sisi kama watanzania tutaendelea kukuhimiza wewe kama Rais wa nchi pamoja na Makamu wa Rais na Waziri Mkuu kuwapigania watanzania katika kufikia nchi ahadi ambayo itakuwa na falfasa ya maisha Bora kwa kila mtu yanawezekana kama serikali itafanikiwa kushinda vita dhidi ya mafisadi na wahujumu wa maendeleo ya wananchi wa Tanzania kupitia kodi zetu;

·  Kodi zetu na Misaada kutoka kwa wafadhili itumike kwa masilahi ya Wananchi na sio watu wachache ambao wanatumia nguvu kubwa katika kuhujumu;

SISI KAMA WATANZANIA TUNA

SABABU, 
NIA, 
NA UWEZO,
WA  KUPAMBANA NA WAHUJUMU wa AMANI, 


MAENDELEO NA UTULIVU AMBAO MWENGE WA UHURU UMEKUWA UKIENEZA KWA MIAKA HAMSINI (50) SASA;


TAZAMA RAMANI  kweli TANZANIA  ni NCHI NZURI lakini wajanya wachache wameanza kuhujumu amani na utulivu wetu kwa faida yao. Tunaendelea kuwaomba viongozi wetu msichukulie rahisi rahisi hii hali ya uvunjaji amani inayoendelea.


MUNGU IBARIKI TANZANIA
 

No comments:

Post a Comment