WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Monday, May 6, 2013

Kauli ya BAKWATA kuhusu mlipuko uliotokea Kanisani Olasiti, ArushaMK/HB.VOL.6/013/1 

06/05/2013

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI    

TAMKO LA BARAZA KUU LA WAISLAMU WA TANZANIA BAKWATA JUU YA MLIPUKO WA BOMU - ARUSHA

Assalaam alaykum warahmatullahi wabarakaatuh.
Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania BAKWATA, limepokea kwa masikitiko makubwa tukio la kurushwa bomu Kanisani na kusababisha upotevu wa maisha na majeraha kwa watu wengi wakati wa sherehe ya uzinduzi wa jengo la Kanisa la Parokia ya Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Orasiti, Arusha.

Kimsingi hili ni jambo la kusikitisha, kukera na kufadhaisha sana kutokea hapa nchini. Watanzania kwa miaka mingi, tumezoea hali ya utulivu na amani na tukio kama hili ni changamoto kwa usalama wa Watanzania wote nchi nzima Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania BAKWATA linalaani kitendo hicho cha kikatili na inaviomba vyombo vya dola kufanya jitihada zote kuhakikisha wahusika wanakamatwa na wanachukuliwa hatua, kwani msiba huu ni wetu sote, Wakristo na Watanzania wote.

Kwa niaba ya Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania mimi Sheikh Issa Bin Shaaban Simba Mufti wa Tanzania nawapa pole wafiwa wote katika tukio hilo na kuwaombea dua majeruhi na Mwenyezi Mungu (SW) awape tahfif na wapone haraka na kurudi katika shughuli zao za kila siku.
Wabillahi Tawfiiq.

SHEIKH ISSA BIN SHAABAN SIMBA.
MUFTI NA SHEIKH MKUU WA TANZANIA BARA.

No comments:

Post a Comment