WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Thursday, May 9, 2013

Simba yatuma salamu kwa Yanga mei 18, yaitwanga Mgambo 1-0

simba e9f0dWekundu wa Msimbazi

WEKUNDU wa msimbazi Simba leo hii wametoa dozi nyingine  kwa maafande wa Mgambo Shooting kutoka mkoani Pwani baada ya kuwatungua bao 1-0 sifuri katika mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara.

Mchezo huo uliotawaliwa na soka la ufundi umepigwa katika dimba la taifa jijini Dar es salaam na kushuhudiwa na mashabiki wengi wa Simba wenye matumaini makubwana kikosi chao kipya.
Mnyama sasa amefufua matumaini ya kucheza michuano ya Afrika mwakani, kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKT Mgambo  leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Katika mchezo huo, uliochezeshwa na refa Andrew Shamba, aliyesaidiwa na Abdallah Rashid na Abdallah Mkomwa wote kutoka Pwani, hadi mapumziko, Simba SC walikuwa mbele kwa bao 1-0.
Bao hilo lilifungwa na kiungo hatari wa pembeni, Haroun Athumani Chanongo dakika ya nane, ambaye aliombea mpira katikati ya Uwanja na kuanza kuwapangua mabeki wa Mgambo kabla ya kumchambua kipa Godson Mmasa.
Ushindi huo, unaifanya Simba SC itimize pointi 45, sasa ikizidiwa tatu na Azam FC inayoshika nafasi ya pili, ambayo Jumapili itamenyana na Mgambo kwenye Uwanja wake wa Azam Complex, Chamazi.
 Katika mchezo wa leo, kocha Mfaransa Patrick Liewig aliwapumzisha wachezaji kadhaa tegemeo, Mrisho Ngassa, Shomary Kapombe, Mwinyi Kazimoto, Felix Sunzu na Mussa Mudde kuelekea mchezo dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Yanga Mei 18.   
Kikosi cha Simba SC leo kilikuwa; Juma Kaseja, Nassor Masoud ‘Chollo’/Omary Salum, Haruna Shamte, Miraj Adam, Hassan Khatib, Jonas Mkude, Edward Christopher, William Lucian ‘Gallas’/Rashid Ismail, Amri Kiemba, Ramadhani Singano ‘Messi’/Salim Kinje na Haroun Chanongo.
JKT Mgambo; Godson Mmasa, Salum Mlima, Ramadhani Kambwili, Bashiru Chanacha, Bakari Mtama, Salum Kipanga, Chande Magoja/Mussa Gunda, Peter Mwalyanzi, Issa Kandulu, Fully Maganga na Nassor Gumbo. 

Chanzo: www.fullshangweblog.com

No comments:

Post a Comment