WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Thursday, May 2, 2013

JK akubali ushauri kuhusu walimu



Mbeya. Rais  Jakaya Kikwete  amesema kuwa kuna haja ya kuruhusu  ajira za walimu kutoka katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kuweza  kupunguza tatizo la upungufu wa  walimu wa sayansi na kuboresha  kiwango cha Elimu ya Tanzania.

Kauli   hiyo ya Rais imekuja baada ya Shirikisho la Wamiliki, Mameneja wa shule na Wakuu wa vyuo Binafsi Tanzania (Tamongsco) kumweleza kuwa  walimu kutoka nchi za Afrika  Mashariki wamekuwa wakilazimika kulipia dola 1,500 kwa ajili ya kibali cha kuja kufanya kazi hapa nchini.

Kikwete alisema kuwa katika mambo  ambayo nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wamekubalina  katika suala la ajira ni pamoja na kila nchi kueleza ajira ambazo  inazifungua na ambazo itazifunga  nchini kwake.
“Katika  suala la  hili la gharama kubwa wanazolipa hawa walimu wanaotoka katika nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki litakwisha kwani tumekubaliana kuwa kila nchi itaeleza ni ajira zipi ambazo itazifungua  na  zipi itazifunga hivyo katika sekta ya elimu kuna haja ya kuachia ili tuweze kuwapata hao walimu” alisema.
“Kuna jambo ambalo  tumesema kuwa Tanzania tunahitaji walimu wa somo ya Sayansi, Kiingereza na Hisabati  ili kuweza kuboresha elimu katika nchi yetu kwa kumaliza tatizo hilo la upungufu wa hao walimu,”alisema.

source: mwananchi

No comments:

Post a Comment