WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Friday, May 10, 2013

Mazishi ya waliofariki katika mlipuko wa bomu, Olasiti, Arusha

 

Majeneza yaliyobeba mili ya marehemu waanga wa bomu.

Askofu Lebulu akiendesha shughuli za mazishi

Viongozi wa Kanisa, Serikali, Vyama na Asasi mbalimbali leo waliungana na Wazazi, Ndugu, Jamaa na Marafiki pamoja na wakazi wa mkoa wa Arusha na vitongoji vyake katika katika kuwaaga marehemu waliofariki baada ya kudhuriwa na bomu lililolipuka katika Kanisa la Mt. Joseph Mfanyakazi kwenye parokia teule ya Olasiti, mkoani Arusha.

Ibada ya mazishi ya watu hao watatu iliendeshwa na Kiongozi wa Kanisa Katolini nchini Tanzania, Mhashamu Polycarp Kadinali Pengo katika Kanisa hilo kabla ya miili kupumzishwa kwenye eneo la lililotengwa nje ya Kanisa.


Sehemu ya Mahubiri ya Kardinali Pengo 




Ndugu zangu,
Nafasi hii inaunganisha mawazo ya furaha na uchungu kutokana na kilichotukutanisha leo.

Mazingira haya yanaweka ugumu wa kupata cha kusema. Ila sisi ni watu wa imani. napenda kueleza imani yetu kama tunavyopaswa kuwa kwenye mazingira haya.

Tumejumuika ili kuwaweka kwenye nyumba ya milele hawa marehemu, lakini pia tunatumia nafasi hii kubariki Kanisa.

Kila mbatizwa ni kiungo cha mwili wa Kanisa. Kila kiungo cha mwili kinapaswa kuungana na kichwa cha Mwili ambaye ni Yesu Mwenyewe.

Kristo akipitia kwa mdomo wa mtume Paulo anatufundisha kuwa "Msijaribu kushindana na uovu kwa uovu, lakini shindeni uovu kwa wema."

Katika viongozi waanzilishi wa dini, ni Yesu peke yake aliyetolea uhai wake kujenga imani ya wafuasi wake. Viongozi wengine hawajikutoa sadaka wenyewe, na baadhi wametoa sadaka ya maisha ya watu wengine kwa ajili ya kueneza imani yao.

Sisi Wakristu Imani yetu inajengwa juu ya mwanzilishi wetu ambaye alitoa uhai wake ili kujenga imani yetu, na hakutoa uhai wa mtu yeyote kwa ajili ya kujenga imani yetu.

Katika masomo tuliyosikia leo, Somo la plili limetupa neno la Mtume Paulo, Rumi 12:17 inasisitiza hilo: usishinde uovu kwa uovu, bali shinda uovu kwa wema.

Soma la Kwanza limeeleza kuwa Paulo na Sila wanateswa kwa ubaya mkubwa sana na kuwekwa gerezani kwa ubaya. Na baada ya kufunguliwa kwa muujiza, askari wa magereza alitaka kujiua, lakini Paulo na Sila wakatenda lililo jema kuokoa maisha yake. Ni baada ya wema huo wokovu ulifika kwa askari huyo na jamaa yake yote wakaweza kumwamini Mungu.

Nawauliza waumini: "Wale waliotekeleza ubaya huu, akija mbele yetu akasema ni mimi ndiye, tungefanya nini kama waumini kwa kufuata mfano wa Yesu?"

Mimi nawaambia "Tujifunze kutoka kwa Bwana wetu Yesu Kristo: 'Tusidiriki kulipia uovu kwa uovu, lakini tutende mema ili kushinda uovu'."

Lakini haya hayaondoi majukumu ya serikali, ambayo yanabaki, na si mimi ninayepaswa kuyasema, wenye mamlaka wanayajua majukumu yao. Mimi nawaambia ninyi waumini.

Uovu si kitu kinachopendeza. Warumi waliwatesa wakristo kwa karne tatu, na haikusaidia chochote Himaya ya Warumi, ambayo baadaye ilisambaratika. Lakini imani yetu imebaki.

Amemalizia kwa kusema: Tukio hili na tukio la mauaji ya Padre Mushi, isiwe sababu ya kuacha amani ya nchi yetu isambaratike.

Lakini ni jukumu la wananchi wotte kuhakikisha nchi yetu haisambaratiki.

Wenye mamlaka watimize wajibu wao. Sisi Wakristo tusamehe, tusijibu uovu, tudumishe amani na upendo katika Taifa letu.






No comments:

Post a Comment