WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Tuesday, May 7, 2013

Rais Tec: wakristo ongezeni kasi ya sala

bishop b489d

Na Gustav Chahe, Iringa              
 
RAIS wa Baraza la Maakofu Tanzania (TEC) Mhashamu askofu Tarcisius Ngalalekumtwa amewataka waamini wakristo kutokuwa na moyo wa kuhamaki kutokana na kitendo kilipuliwa Kanisa Katoliki huko Arusha.
 
Amesema kama ilivyoutamaduni wa Kikristo, yanapotukia matukio ya kusikitisha kama hayo silaha iliyo kubwa ni sala kumuomba Mungu atoe jibu kwa wanaohusika na mateso kama hayo.

“Kasi ya sala iendelee, ili Mungu wetu wa Amani ajenge fikira za upendo na haki katika mioyo yetu” alisema.
 
Amesema waamini wasikate tamaa na kuacha kusali kwa kuwa Mungu ndiye mwenye jibu na atatoa majibu kadiri atakavyo kwa wale wote wanaowatesa wenzao kwa sababu zao binafsi.
 
Hata hivyo alisema licha ya kuwa kila mtu amepokea kwa mshituko na maumivu makubwa, roho za watu zinazoteswa na wengine Mungu atazifariji na kuziponya lakini mtesaji atapata majibu yake.
 
Alisema waliopoteza maisha katika mlipuko huo Mungu atawarehemu na kuwafariji majeruhi wote.
 
“Waliopoteza maisha wapokee Rehema ya Mungu na waliojeruhiwa wafarijiwe na uwezo wa Mungu” alisema.
 
Hali kadhalika amesema upendo na haki ni zawadi kutoka kwa Mungu na hivyo, anayedhurumu wengine zawadi hiyo atapata pigo kubwa.
 
Aidha amesema wakati uliopo sasa ni wakutafakari na kumkabidhi Mungu yale yote yanayowasumbua wanadamu na kuongeza nguvu ya sala ili majibu ya Mungu yapatikane kwao.
 
“Tulieni na kufanya tafakari kasha mwambie Mungu hayo yote ayafanyie kazi kwa uweza wake. Sisi binadamu tunategemea nguvu kutoka kwake” alisema

No comments:

Post a Comment