WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Thursday, May 9, 2013

Necta wagoma kufuta matokeo IV,watishia kujiuzuru

ndalichako 46eb4

Katibu Mtendaji wa Necta Joyce Ndalichako

WAKATI Serikali ikitangaza kufuta matokeo ya mtihani wa kidato cha nne, Mwenyekiti wa Baraza la Mitihani la Taifa-NECTA ambaye pia ni Makamu Mkuuwa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Prof.Rwekaza Mukandala amesema hayuko tayari kubadili matokeo ya Kidato cha Nne.Chanzo cha karibu cha Prof.Mukandala kinadai kuwa mara baada ya kutolewa taarifa ya Serikali inayotaka 'kuboreshwa' kwa matokeo hayo,Prof.Mukandala ameonesha kukataa amri hiyo hadi sasa. 'Sisi tulipitisha matokeo hayo mbele yao na kwa idhini yao.Iweje leo Baraza libadili matokeo?.Tunafanya hivi kwa faida ya nani na kwa ustawi wa elimu ya wapi?' alinukuliwa akihoji Prof.Mukandala. Habari za kuaminika zinadai kuwa Prof.Mukandala pamoja na Katibu Mtendaji Dr.Joyce Ndalichako wanajiandaa kuachia ngazi kama Serikali itasimamia uamuzi wake huo.
 
Naye Naibu Waziri wa Elimu na Ufundi Philipo Mulugo alipotafutwa kwenye simu yake ya mkononi kuzungumzia suala hilo iliita bila ya kupokelewa na baadaye akatuma ujumbe mfupi  akisema, "Sorry I'm busy call back later", alisema Mulugo kupitia simu yake ya mkononi
 
source: Mjengwa blog

No comments:

Post a Comment