WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Monday, May 13, 2013

Lady Jaydee apokea rasmi hati ya mashtaka


ladyjaydee 23390

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Judith Wambura Mbibo a.k.a Lady Jaydee muda si mrefu amepokea hati yake ya mashtaka kutoka katika mahakama ya Kinondoni ambapo ameshtakiwa na Mkurugenzi wa vipindi wa Clouds FM baada ya kuwa na kutofautiana kwa muda.

Jaydee ambaye alikuwa Baraza la Sanaa ambapo alikuwa akiongea katika jukwaa la wasanii, alipata ujumbe wa kuitwa mahakamani na alipofika alikabidhiwa hati hiyo ambayo mwenyewe alikataa kusema makosa aliyoorodheshewa, na kusema kwamba anataka kwanza awasiliane na mwanasheria wake.

Kikubwa ambacho aliweza kusema kwa waandishi waliokuwa wameongozana naye ni kwamba, kesi itaanza kuunguruma tar 27 mahakamani hapo.
Kati ya vielelezo alivyopewa na mahakama ambavyo alivionesha kwa baadhi ya waandishi ni pamoja na nakala za magazeti na nakala za Post za blog yake pamoja na tweets!

source: mjengwa blog

No comments:

Post a Comment