WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Tuesday, May 21, 2013

Simba yaifunika Yanga

Dar es Salaam.Licha ya kufanikiwa kutwaa taji, Yanga imeshindwa kufikia rekodi ya watani zao Simba waliyoweka msimu uliopita iliponyakua ubingwa kwa kujikusanyia pointi 62.
Yanga mwishoni mwa wiki iliizabua Simba mabao 2 - 0, na kutangazwa mabingwa wapya wa msimu wa 2012-2013 ikiwa na jumla ya pointi 60, ambazo sawa na tofauti ya pointi mbili.
Katika upachikaji mabao, Yanga imetoshana nguvu na mtani wake Simba, ambayo msimu wa 2011-12 ilitumbukiza wavuni mabao 47, idadi iliyofikiwa pia na Yanga msimu huu.
Katika ulinzi, Yanga imeshidwa kupiku rekodi ya Simba ambayo mpaka ina kamilisha msimu wa iliruhusu mabao 12 pekee wakati Yanga imemaliza msimu huu imefungwa mabao 14.
Pia, msimu wa 2011-12, Yanga ilihitimisha msimu ikiwa imetunguliwa mabao 30, tofauti na Simba ambayo licha ya kumaliza nafasi ya tatu msimu uliomalizika
ilibwagizwa mabao 23.
Katika hatua nyingine, ukata wa mabao ulionekana kuuvamia msimu wa 2012-13 uliofikia tamati Mei 18, ambapo mabao 370 pekee yaliyotinga nyavuni.
Idadi hiyo ni pungufu ya mabao 40 ambayo yalishuhudiwa yakitinga nyavuni msimu wa 2011- 2012, ambao jumla ya mabao 410 yalitazamwa yakigusa nyavu.Text inakuja hapa.

source: mwananchi

No comments:

Post a Comment