WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Friday, May 17, 2013

Poulsen awaita Barthez, Chanongo Stars


 
Kocha mkuu wa Taifa Stars, Mdenmark Kim Poulsen
Benchi la ufundi la timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars), linaloongozwa na kocha Mdenmark Kim Poulsen limetaja kikosi cha wachezaji 26 watakaoingia kambini kujiwinda kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco itakayochezwa Juni 8 mwaka huu jijini Marrakech, Morocco.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Poulsen alisema kuwa katika kikosi chake ameita wachezaji wapya sita ingawa baadhi yao wamewahi kuchezea timu hiyo, huku akiacha wengine watatu aliokuwa nao kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Morocco ambayo Taifa Stars ilishinda mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Taifa Machi 24 mwaka huu.

Wapya aliowaita katika kikosi hicho kitakachoingia kambini jijini Dar es Salaam Jumatatu ni Ally Mustafa 'Barthez' (Yanga), Vicent Barnabas (Mtibwa), Juma Luzio (Mtibwa), Haruna Chanongo (Simba), Mudhathiri Yahya (Azam) na Zahoro Pazi (JKT Ruvu) wakati wachezaji aliowaacha ni Shabani Nditi (Mtibwa), Nassoro Masoud 'Chollo' (Simba) na Issa Rashid (Mtibwa).

Kikosi kamili cha Taifa Stars ambacho kabla ya kwenda Morocco kitapita jijini Addis Ababa, Ethiopia kucheza mechi ya kirafiki Juni 2 mwaka huu dhidi ya Sudan ni kama ifuatavyo;
Makipa ni nahodha Juma Kaseja (Simba), Aishi Manula (Azam), Barthez (Yanga) na Mwadini Ally (Azam). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub 'Cannavaro' (Yanga), Shomari Kapombe (Simba), Vicent Barnabas (Mtibwa Sugar) na Waziri Salum (Azam).

Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd 'Chuji' (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Khamis Mcha (Azam), Mwinyi Kazimoto (Simba), Yahya (Azam) na Salum Abubakar 'Sure Boy' (Azam).

Washambuliaji ni John Bocco 'Adebayor' (Azam), Luzio (Mtibwa Sugar), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Mrisho Ngasa (Simba), Simon Msuva (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC) na Pazi (JKT Ruvu).

Aidha, kocha huyo alisema kikosi kitakachoingia kambini kitakuwa na wachezaji 24 ambapo Samatta na Ulimwengu watajiunga na timu jijini Marrakech, lakini wachezaji atakaondoka nao Dar es Salaam kwenda Addis Ababa ni 22 ambapo ataacha kipa mmoja na mchezaji mmoja wa ndani baada ya mchujo.

Awali TFF ilikuwa imeitafutia Taifa Stars mechi ya kirafiki Juni 1 mwaka huu dhidi ya Algeria, Libya au Misri, lakini baadaye Algeria ikasema itacheza na Togo, wakati Misri ilitaka mechi hiyo ichezwe Juni 4 jijini Cairo, jambo ambalo lisingewezekana kwa Stars kwani ina mechi ya mashindano Juni 8 mwaka huu.

Kwa upande wa Libya mechi hiyo ilikubaliwa ichezwe Tunis, Tunisia, Juni 2 mwaka huu. Lakini baadaye Libya ikataka mechi hiyo ichezewe jijini Tripoli ambapo TFF ilikataa kutokana na sababu za kiusalama.

Katika hatua nyingine, Osiah alisema kuwa Poulsen ameingia nao mkataba wa miaka miwili kuendelea kuinoa Stars baada ya mkataba wake wa mwanzo kumalizika Machi 15 mwaka huu.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment