WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Thursday, May 30, 2013

Kiiza asisitiza mamilioni Yanga


Hamis Kiiza
Wakati uongozi wa klabu ya Yanga umesema kwamba mshambuliaji wao wa kimataifa, Hamis Kiiza, amekalia kuti kavu kwa sababu klabu haina kiasi cha fedha ambacho amekitaja ili apewe mkataba mpya, Mganda huyo ameshikilia msimamo wake huo.
Kiiza ameutaka uongozi wa Yanga umpe Dola za Marekani 50,000 (Sh. milioni 80) kwa ajili ya kusaini mkataba mpya na pia umpe mshahara wa Dola za Marekani 3,000 (Sh. milioni 4.8) kila mwezi.

Kiongozi mmoja wa juu wa Yanga (jina tunalihifadhi) alisema kuwa endapo Kiiza ataendelea kuwa na msimamo huo, nafasi yake itachukuliwa kiulaini na kipa Mghana, Yaw Berko na kiungo Mnyarwanda, Kabange Twite.

"Licha ya mazungumzo na kumweleza msimamo wetu, alibaki na msimamo wake na hadi alipoamua kwenda kwao, alituandikia barua akieleza kwamba atakuwa tayari kusajili kwa Dola za Marekani 45,000 na si chini ya hapo,".

Kiongozi huyo aliongeza kuwa Kiiza anatakiwa akubali kushusha kiwango cha fedha cha usajili ili asajiliwe la sivyo nafasi yake itachukuliwa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Abdallah Binkleb, aliliambia gazeti hili kuwa kamati yake bado iko katika mazungumzo na wachezaji hao watatu na itakapofikia mwisho itawasajili wawili.

Binkleb alisema kwamba kamati yake inafanya maamuzi ya kumsajili mchezaji baada ya kuridhishwa na kiwango cha mchezaji husika na kuridhiwa na vipengele vitakavyokuwapo ndani ya mkataba.

Alisema pia wanataka kumaliza zoezi la usajili wiki hii ili mapema wiki ijayo programu ya mazoezi ya timu yao ianze kwa ajili mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame).

Yanga ndiyo mabingwa watetezi wa mashindano hayo ambayo mwaka huu yatafanyika kuanzia Juni 18 hadi Julai 2 huko Sudan.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment