WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere

Wednesday, May 1, 2013

MEI MOSI UWANJA WA AMANI ZANZIBAR

Seif-Ali-Iddi 3ce7f
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewataka vijana wa Zanzibar wabadilike na kujenga Utamaduni wa Ujasiriamali na wawe tayari kujiajiri kupitia vyama vya ushirika vya uzalishaji mali pamoja na kuanzishsa SACCOS ili kupata mitaji yenye unafuu.

Balozi Seif ameeleza hayo katika kilele cha maadhimisho ya sherehe za Wafanyakazi Duniani (Mei mosi) zilizofanyika katika Kiwanja cha Amaan na kuwashirikisha Wafanyakazi wa Mawizara, Maidara na Mashirika ya Serikali pamoja na taasisi binafsi baada ya kuyapokea maadamano ya wafanyakazi hao.

Amesema pamoja na Serikali kuchukua juhudi kubwa ya kupunguza tatizao la ukosefu wa ajira kutoka asilimia saba mwaka 2007 hadi asilimia nne mwaka 2010 bado tatizo la ajira ni changamoto kubwa Zanzibar kama lilivyo nchi nyingi Duniani.

Hata hivyo Makamu wa pili wa Rais ameahidi kwamba Serikali itaendelea kufanya kila juhudi kupunguza ukosefu wa ajira nchini ili vijana waweze kuishi kwa amani.

"La muhimu vijana wetu waache tabia ya kuchagua kazi. Kazi ni kazi mradi inakupatia riziki yako kwa njia ya halali, " amesisitiza Balozi Seif Ali Iddi.

Ameviagiza Vyama vya Wafanyakazi kusaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana kwa njia ya kutoa elimu itakayowasaidia kukabiliana na ushindani wa soko la ajira la sekta binafsi katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki

Amesema uzoefu unaonyesha kwamba vijana wengi wamekosa Utamaduni wa kufanyakazi katika sekta binafsi, matokeo yake huacha kazi baada ya kipindi kifupi cha kuajiriwa na nafasi zao kuchukuliwa na vijana kutoka nchi jirani.

Makamu wa pili wa Rais pia amevitaka vyuo vikuu nchini kuangalia mahitaji ya ajira yaliyokuwepo nchini kwa kuandaa mitaala na mafunzo yatakayowasaidia vijana kuajiriwa kwa urahisi.

"Vyuo vyetu vikuu nchini navyo vinanafasi kubwa ya kusaidia kupunguza tatizo la ajira kwa kuandaa mitaala yao ya kufundishia na mafunzo mengine kwa mujibu wa mahitaji yaliyopo kama vinavyofanya vvyuo vikuu vyengine vingi Duniani, " alifahamisha Makamu wa pili wa Rais.
Blozi Seif amewahakikishia wafanyakazi kwamba Serikali itaendelea kuchukua hatua mbali mbali za kuboresha maslahi yao ili kuhakikisha yanalingana na kazi wanazofanya na kwa upande wao amewataka kufanya kazi kwa bidii na maarifa ili kukuza tija huku wakijua kwamba haki na wajibu ni watoto pacha.

Akizungumza katika maadhimisho hayo Mwakilishi wa Shirika la kazi duniani (ILO) Bibi Hopholang Phororo ameishauri Serikali kuendelea kuwajengea wafanyakazi mazingira bora ya kazi ikiwemo kulinda afya na haki zao.

Ameahidi kuwa Shirika hilo liko tayari kuendelea kuunga mkono katika kusaidia juhudi za Serikali ili kuhakikisha wafanyakazi wako salama wakiwa kazini.
Katibu Mkuu wa ZATUC Maalim Khamis Mwinyi Muhammed ameelezea kuridhishwa na mafanikio makubwa katika awamu ya saba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwa karibu sana na Shirikisho hilo na kutekeleza kanuni na sheria za kazi.
Hata hivyo Maalim Khamis ameeleza masikitiko ya wafanyakazi wa Zanzibar kwa kutopandishwa viwango vya mishahara yao mwaka uliopita licha ya uchumi kuelezwa kuwa umekua.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBARMakamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewataka vijana wa Zanzibar wabadilike na kujenga Utamaduni wa Ujasiriamali na wawe tayari kujiajiri kupitia vyama vya ushirika vya uzalishaji mali pamoja na kuanzishsa SACCOS ili kupata mitaji yenye unafuu.

Balozi Seif ameeleza hayo katika kilele cha maadhimisho ya sherehe za Wafanyakazi Duniani (Mei mosi) zilizofanyika katika Kiwanja cha Amaan na kuwashirikisha Wafanyakazi wa Mawizara, Maidara na Mashirika ya Serikali pamoja na taasisi binafsi baada ya kuyapokea maadamano ya wafanyakazi hao.

Amesema pamoja na Serikali kuchukua juhudi kubwa ya kupunguza tatizao la ukosefu wa ajira kutoka asilimia saba mwaka 2007 hadi asilimia nne mwaka 2010 bado tatizo la ajira ni changamoto kubwa Zanzibar kama lilivyo nchi nyingi Duniani.

Hata hivyo Makamu wa pili wa Rais ameahidi kwamba Serikali itaendelea kufanya kila juhudi kupunguza ukosefu wa ajira nchini ili vijana waweze kuishi kwa amani.

"La muhimu vijana wetu waache tabia ya kuchagua kazi. Kazi ni kazi mradi inakupatia riziki yako kwa njia ya halali, " amesisitiza Balozi Seif Ali Iddi.

Ameviagiza Vyama vya Wafanyakazi kusaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana kwa njia ya kutoa elimu itakayowasaidia kukabiliana na ushindani wa soko la ajira la sekta binafsi katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki

Amesema uzoefu unaonyesha kwamba vijana wengi wamekosa Utamaduni wa kufanyakazi katika sekta binafsi, matokeo yake huacha kazi baada ya kipindi kifupi cha kuajiriwa na nafasi zao kuchukuliwa na vijana kutoka nchi jirani.

Makamu wa pili wa Rais pia amevitaka vyuo vikuu nchini kuangalia mahitaji ya ajira yaliyokuwepo nchini kwa kuandaa mitaala na mafunzo yatakayowasaidia vijana kuajiriwa kwa urahisi.

"Vyuo vyetu vikuu nchini navyo vinanafasi kubwa ya kusaidia kupunguza tatizo la ajira kwa kuandaa mitaala yao ya kufundishia na mafunzo mengine kwa mujibu wa mahitaji yaliyopo kama vinavyofanya vvyuo vikuu vyengine vingi Duniani, " alifahamisha Makamu wa pili wa Rais.

Blozi Seif amewahakikishia wafanyakazi kwamba Serikali itaendelea kuchukua hatua mbali mbali za kuboresha maslahi yao ili kuhakikisha yanalingana na kazi wanazofanya na kwa upande wao amewataka kufanya kazi kwa bidii na maarifa ili kukuza tija huku wakijua kwamba haki na wajibu ni watoto pacha.

Akizungumza katika maadhimisho hayo Mwakilishi wa Shirika la kazi duniani (ILO) Bibi Hopholang Phororo ameishauri Serikali kuendelea kuwajengea wafanyakazi mazingira bora ya kazi ikiwemo kulinda afya na haki zao.

Ameahidi kuwa Shirika hilo liko tayari kuendelea kuunga mkono katika kusaidia juhudi za Serikali ili kuhakikisha wafanyakazi wako salama wakiwa kazini.
Katibu Mkuu wa ZATUC Maalim Khamis Mwinyi Muhammed ameelezea kuridhishwa na mafanikio makubwa katika awamu ya saba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwa karibu sana na Shirikisho hilo na kutekeleza kanuni na sheria za kazi.
Hata hivyo Maalim Khamis ameeleza masikitiko ya wafanyakazi wa Zanzibar kwa kutopandishwa viwango vya mishahara yao mwaka uliopita licha ya uchumi kuelezwa kuwa umekua.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

No comments:

Post a Comment