WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Tuesday, May 21, 2013

Neno La Leo: Tukichoka Kuhubiri Amani, Tujiandae Na Kazi Ya Kuchimbiana Makaburi..

a6 63d34
 
 
Ndugu zangu,
 
Naiona hatari kubwa nyingine inakuja mbele yetu. Ni haya makundi mawili; MaBodaboda na MaMachinga. Hofu yangu kuna wanasiasa wachache wanaowaona vijana hawa, katika matatizo yao ya kiuchumi, kuwa ni mtaji wa kisiasa. Na kimsingi wanawageuza kuwa ' Shuka za Kisiasa'. Na hapa ni wanasiasa wa vyama vyote.
 
Hatari yake?
Viongozi wasipokuwa makini, wakaacha kutanguliza busara na hekima kwenye kauli zao, basi, hofu ya kauli kupelekea machafuko na kuvunjika kwa amani itabaki kuwepo.
Maana, hawa MaBodadoba na MaMachinga, pamoja na kuwa wengi wao ni vijana wema kabisa, na ambao, kwenye mahangaiko yao, kama wagonjwa, wanamsikiliza kila anayekuja na kauli za kuwapa matumaini, hata kama ni ya muda mfupi,  na hata kama ni kwa kuvunja sheria. 
 
Na kwa vile Elimu ya Uraia iko chini sana katika jamii yetu, hata kwa miongoni mwa viongozi wetu, basi, ndio maana naiona hatari hii kubwa inayokuja mbele yetu. Kwamba MaBodaboda na MaMachinga wakiendelea kutumiwa kama ' Shuka za Wanasiasa', basi, yumkini, huko tuendako Watanzania tujiandae na kazi ya kuchimbiana makaburi. Maana, siku zote, maovu huzaa maovu. MBodaboda au Mmachinga mmoja akiuawa, kuna mia watakaokuja kutaka kulipiza kisasi. Na Polisi mmoja akiuawa, kuna operesheni ya kipolisi itakayofuata. Na polisi wetu hawa ni vijana hawa hawa ambao wengine wameponea chupuchupu kuwamo  kwenye makundi haya ya MaBodaboda na MaMachinga, lakini sasa, tumewapa pia silaha za moto wabebe.
 
Naam, tukichoka kuhubiri Amani, Upendo Na Mshikamano, basi, tujiandae na kazi ya kuchimbiana makaburi.
Maggid
 Iringa,
0754 678 252

No comments:

Post a Comment