WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Saturday, May 25, 2013

Maalim Seif afungua kongamano la pili la kitaifa la maridhiano

 

 Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akihutubia katika ufunguzi wa kongamano la pili la Maridhiano lilolofanyika hoteli ya Bwawani.
 Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akihutubia katika ufunguzi wa kongamano la pili la Maridhiano lilolofanyika hoteli ya Bwawani.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano Mzee Hassan Nassor Moyo akizungumza katika kongamano la pili la Maridhiano lilolofanyika hoteli ya Bwawani.
 Mjumbe wa Kamati ya Maridhiano Ismail Jussa Ladhu, akizungumza katika kongamano la pili la Maridhiano lilolofanyika hoteli ya Bwawani.
 Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano Hassan Nassor Moyo (kushoto) na Mjumbe wa kamati hiyo Ismail Jussa Ladhu, wakibadilishana mawazo kabla ya ufunguzi wa kongamano la maridhiano lililofanyika hoteli ya bwawani.
Baadhi ya washiriki wa kongamano la pili la maridhiano Zanzibar lililofanyika hoteli ya Bwawani, wakisikiliza hotuba ya Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad, katika ufunguzi wa kongamano hilo. (Picha, Salmin Said, OMKR)
 
Na Hassan Hamad, OMKR
 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, amesema dhamira ya msingi ya ukombozi wa Zanzibar kupitia Mapinduzi ya Januari 12, 1964, ni Zanzibar kuweza kujitawala yenyewe na kuwa na mamlaka kamili.
 
Maalim Seif ameeleza hayo katika ukumbi wa salama hoteli ya Bwawani, wakati akifungua kongamano la pili la kitaifa linalohusu Maridhiano ya Wazanzibari.
 
Amesema dhamira hiyo ya Mapinduzi ilianza kukiukwa baada ya kutiwa saini kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao uliipunguzia Zanzibar mamlaka yake.
 
Amesema wakati Wazanzibari wanapodai kuwa na mamlaka kamili wanatetea haki na maslahi ya nchi yao, na kwamba hakuna sababu ya kubezwa wala kupuuzwa.
Amefahamisha kuwa akiwa ni kiongozi wa Zanzibar, atasimamia na kutetea mawazo ya wazanzibari waliowengi katika kupata haki zao za msingi ndani na nje ya Zanzibar.
 
Akifafanua zaidi kuhusu msimamo wake amesema hiyo haina maana kuwa Wazanzibari hawataki Muungano, bali wanataka kuwepo kwa Tanzanyika na Zanzibar zenye mamlaka kamili, halafu kuwepo na muungano wa mkataba, ili kila nchi iweze kuendesha mambo yake kwa uhuru.

“Kuwa na mamlaka kamili sio kwa maslahi ya watu wachache bali kwa watu wote, ni kama mvua, yaani inaponyesha mimea yote inanawirika”, alifafanua Maalim Seif na kuongeza,
 
“Tunataka kurejesha heshima ya nchi yetu, tuwe na sera na Wizara yetu ya mambo ya nje, bendera yetu ipepee nchi za kigeni, Umoja wa Mataifa na Jumuiya nyengine za Kimataifa zikiwemo Jumuiya ya Madola, Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Afrika Mashariki”.
 
Amewataka wanakongamano hao kuwaongoza wajumbe wa mabaraza ya katiba katika kutetea maoni na maslahi ya Zanzibar.
 
Akizungumzia kuhusu mafanikio ya maridhiano amesema yamerejesha umoja wa wazanzibari na kuondosha uhasama na chuki miongoni kwa wananchi.
 
Ameipongeza kamati ya maridhiano chini ya Mwenyekiti wake Mzee Hassan Nassor Moyo kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kuyaendeleza maridhiano hayo na umoja wa wazanzibari.
 
Nae Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano ambaye ni mwanasiasa mkongwe wa Zanzibar Mzee Hassan Nassor Moyo amesema maridhiano hayo yaliyoasisiwa na Rais Mstaafu wa Zanzibar dkt. Amani Abeid Karume na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad, yameondoa fitna na chuki zilizodumu kwa muda mrefu miongoni mwa wananchi.
 
Amesema kamati yake inaisubiri kwa hamu kubwa rasimu ya Katiba mpya itakayotolewa, ili waweze kuichambua kuona kama imezingatia maoni ya wananchi na maslahi ya Zanzibar.
 
Akiwasilisha mapendekezo ya kamati hiyo Mzee Moyo amesema kila nchi katika Muungano inapaswa kuwa na uraia wake, sera yake ya mambo ya nje na Muungano uwe na JINA la “Muungano wa Jamhuri za Tanzania” au “United Republics of Tanzania”.

7 comments:

 1. ndugu yangu sharif nakupongee kwa kuwa mkweli lakini sisi hatutaki muungano wowote ule , hata mkataba hatutaki kwani humo pia kutakuwa na ujanja ujanja , bora kila mtu achukue nchi yake , tushirikiane tu kama vile tunavyoshirikiana na kenya uganda nk , ingawa ushirikiano wetu unaweza kuwa zaidi ya huo wa east africa , lakini mambo ya mikataba hatutaki kabisa kabisa
  ReplyDelete
 2. Usitusemee, sisi wengine tunauhitaji kama uhai. Tunajua kuwa bila Muungano ni gomvi tu hapa Zanzibar.
  ReplyDelete
 3. mtwara wameanza udini mbeya nani achinje kukatana mapanga kwa siasa zote hizi hutokea tanganyika
  ReplyDelete
 4. wazanzibar walikuwepo na tulikuwepo na tupo kabla ya tanganyika,watanganyka husema wazanzibar wakitoka nje ya muungano watagawana unguja na upemba,hizi ni hisia dhaifu za nyrere,tanganyika inakabiliwa na udini sababu wakristo wanawalemea waisilam na kuwadhulumu kupitia mfumo kristo,kuchinja nyama sensa hiini mifanohai,necta ,siasa chafuchaguzi za diwanitu wanachinjana na kukatana mapanga siasa chafu utekaji na kungowa watukucha ,mwangosi ,sikwambii mtwara hatanyinyi tanganyika haitokuwa salama zanzibar matokeo ya fujo na ubaguzi ni siasa za tanganyika kupitia ccm ukitaka kujuwa hili kuzamakwa spice ilender wazanzibar wa unguja na pemba walivyoguwsa na msiba lakini kuzama kwa skajit watu walikuwa wakisema wakati inatokea huko itakuwa watananyika wengi tu kuliko sisi wazanzibar watu kifo skajit hakikuhit sana
  ReplyDelete
 5. tunacho kidai sisi sio kuuvunja mungano bali ni muungano wausawa huku kila nchi ikiwa namamlaka yake kamili kitaifa na kimataifa kisha tukashirikiana kwa makubaliano maalumya kiuchumi na kijamii
  ReplyDelete
 6. @ano 6.15 , si tatizo waitishe kura ya maoni tuone nani mkweli. Kwa kuongezea tu mapinduzi hayakuletwa ili wazanzibari wajitawale , isipokuwa ilikuwa ni njama ya mwl nyerere kutaka kuitawala zanzibar kwa njia ya muungano huo ndio ukweli na ndio maana mpaka leo ukizungumzia muungano inakuwa kama nongwa kwa watanganyika, lakini msisahau kuwa ndugu zetu pia watanganyika wanataka nchi yao iwe peke yao huu muungano ushawatosha hata wao.Wala si kweli kama bila muungano tutagombana hizi ni fitna zisizo na msingi zimepandikizwa na wachache wenye faida na muungano.@ ano 8.24 udini umeletwa na Mwl Nyerere ndie alipandikiza mbegu za udini , ukiangalia katika kila sekta zote muhimu iliwapa jamaa zake, na mpaka leo hii , angalia wizara zote , jeshi , polisi, akina tra , elimu, uhamiaji , kila mahali hata afya mfano mdogo angalia muhimbili bodi yake ina akina nani , waajiriwa wengi ni akina nani? wamebakia kuwadanganya kwa kupiga picha watu wanaovaa hijabu ktk sherehe mbalimbali ili waonekane kuwa kuna ka usawa , kuwapa ukubwa akina alhajat ktk sensa , akina mwema , akina jaji mkuu , akina bilali huu ni unafiki mtupu. Kama mwongo angalia hata kazi ambazo hazitaki akili nyingi kama za kukusanya parking fee hapa dar es salaam ni akina nani wamepewa kazi hizo? wakishasoma haya niliyoandika , watachofanya watawavalisha vihijabu baadhi yao ili waonekane kuna ka usawa . Uhuru wa zanzibar ni lazima upatikane kwa uwezo wa mola hakuna chenye mwanzo ila huwa na mwisho msisahau , umefika wakati uvunjwwe muungano kwa amani na upendo ili tubakie kushirikiana , kuliko kuvunjika kwa umwagaji damu na kuacha chuki na madhila.
  ReplyDelete
 7. nakushangaa sharifu hamadi vipi unasema wizara ya mambo ya nje tu , sisi wananchi wako tunataka kila wizara iwe peke yetu isiungane na chochote kile , labda wizara ya kilimo na afya . Wizara nyengine zote zisiwepo kwenye muungano , tuwe na kila kitu chetu wenyewe , kuanzia jeshi la wanachi , polisi, magereza , uhamiaji , elimu , usafiri , nishati , ardhi, mambo ya ndani, kwa kifupi hatutaki muungano kwenye lolote lile , tushirikiane tu katika nyanja zitazokubalika, msemaji hapo anonymus 8.45 ana mtazamo wa mbali maneno ya kuzingatia japokuwa Rais Nyerere amefariki lakini athari zake zinaonekana mpaka leo hii
source:ZanziNews blog

No comments:

Post a Comment