JE MWENGE WA UHURU BADO
UMEENDELEA KUTIMIZA ADHIMA YAKE KATIKA KIPINDI HIKI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA
TAIFA LETU?
Mwenge huo uliwashwa Siku ya uhuru wa Tanganyika Desemba 9, 1961,
Baba wa Taifa aliwasha Mwenge na baadaye ukapelekwa kwenye kilele cha mlima
Kilimanjaro
Je mwenge huu ulikuwa na
maana gani kwa Taifa?
· kwa ufupi, ulikuwa ni alama ya uhuru wetu kuona
mapungufu yetu sisi wenyewe katika ujenzi wa Taifa letu
· Falsafa hiyo inalenga kuwaunganisha Watanzania, unatumika
kukemea waovu, unatumiwa na serikali kupitisha ujumbe na kuzindua miradi ya
maendeleo inayoleta matumaini kwa Watanzania
· mwenge ulikutumika kuhimiza uzalendo, kuhimiza uwajibikaji,
kueneza ujumbe juu ya athari za rushwa, ukimwi, uzembe na kadhalika;
· Mwenge ni ishara ya mshikamano wa udugu wa kitaifa
· Mwenge ametumika kama chombo cha kuchochea maendeleo
kupitia kauli mbio yake amabyo imekuwa ikitolewa kila mwaka na tukizingatia kuwa mwenge unafika katika kila kona ya nchi yetu.
MIAKA 50 YA UHURU JE MALENGO YA MWENGE WA UHURU YAMEONYESHA
MAFANIKIO?
· Mwenge umekuwa ukitukumbusha kuhusu kuthamini uhuru wetu
kama taifa ambalo tunatakiwa kusimama imara kwa kuzingatia misingi ya imani upendo, amani
na utulivu.
·
Mwenge pamoja na tofauti zetu za makabila, dini na vyama
vya siasa sisi kama Watanzania katika kipindi hiki cha miaka 50 bado
tunahimizwa kusimama kama Taifa moja na
kuhakikisha kuwa Taifa letu haliyumbishwi na
watendaji wabovu, wazembe, wala Rushwa, Mafisadi na wanaoeneza chuki za
kuligawa Taifa kwa njia yeyote ile iwe ni Dini, Ukabila au Vyama vya siasa.
· Katika kusherekea Mwenge wa Uhuru falfasa ya Mwenge
inatakiwa ibaki imara ila utekelezaji wake unatakiwa kubadilika kulingana na
hali halisi ya vyama vingi, upana wa
demokrasia, na uzembe wa uwajibikaji;
· Sheria inatakiwa iendelee kufuatwa na wale wote wanaovunja sheria wachukuliwe hatua kali bila kujali nafasi zao kwa kufanya hivyo tutafanikiwa kurejea nuru yake ile ile tukapousimika tena tarehe 9 december 2011, kilele katika Mlima Kilimanjaro;
· Mwenge kwa sasa uwamulike ; wabadhirifu, wazembe maofisini,
wala rushwa magendo uwajibikaji ni dhana
ambayo kwa sasa kama Taifa tunaihitaji sana
· Mheshimiwa Rais wa Awamu ya Nne Dr. Jakaya Mrisho Kikwete
sisi kama watanzania tutaendelea kukuhimiza wewe kama Rais wa nchi pamoja na
Makamu wa Rais na Waziri Mkuu kuwapigania watanzania katika kufikia nchi ahadi
ambayo itakuwa na falfasa ya maisha Bora kwa kila mtu yanawezekana kama
serikali itafanikiwa kushinda vita dhidi ya mafisadi na wahujumu wa maendeleo
ya wananchi wa Tanzania kupitia kodi zetu;
· Kodi zetu na Misaada kutoka kwa wafadhili itumike kwa
masilahi ya Wananchi na sio watu wachache ambao wanatumia nguvu kubwa katika
kuhujumu;
SISI KAMA WATANZANIA TUNA
SABABU,
NIA,
NA UWEZO,
WA KUPAMBANA NA WAHUJUMU wa AMANI,
MAENDELEO NA UTULIVU AMBAO MWENGE WA UHURU UMEKUWA UKIENEZA KWA MIAKA HAMSINI (50) SASA;
TAZAMA RAMANI kweli TANZANIA ni NCHI NZURI.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
No comments:
Post a Comment