·
NINI MAONI YAKO kuhusu uongozi wake?
·
JE NI KIONGOZI AMBAYE
AMEANDIKA HISTORIA KAMA ILIVYOKUWA KWA BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE
NYERERE?
·
UONGOZI WAKE TUNAWEZA KUUELEZA
VIPI NI HASI AU CHANYA?
Dr. Jakaya Mrisho Kikwete
ndio rais wa awamu ya nne wa serikali ya Muungano wa Tanzania. Kwa maneno
rahisi sana Kikwete ndiye nahodha wa
meli ya taifa ambaye amepewa mamlaka ya kuhakikisha kuwa analivusha na
kulifikisha salama katika nchi ya ahadi ambayo imejaa maziwa na asali.
Rais kama kiongozi wa juu
wa serikali anatakiwa kuwa na mbinu mbadala kuhakikisha kuwa ana sera ambazo
zitamsadia yeye na chama chake kuhakikisha kuwa anasimamia utekelezaji sera zake
kwa manufaa ya wananchi wote bila ubaguzi.
Rais anatakiwa kuwa ni mtu
ambaye anajua kuwa taifa linakwenda wapi na litafika lini pale ambapo wananchi wanataka kufikia kwa ustawi
wa maisha yao; Katika kufanya hivyo, Rais anatakiwa kutoa maagizo, kuyafuatilia
na pale ambapo mambo hayaendi ipasavyo na kuwawajibishawatendaji wake.
Rais wetu anatakiwa kuwa na
nadharia ya “uchumi” hata kama hana shahada ya uchumi lakini kupitia washauri
wake ambao wanatakiwa wamweleze ABC ya uchumi wa ulimwengu. Afahamu nini
madhara ya mfumuko wa uchumi ili
wananchi wanapolalamika maisha magumu aweze kuwaelewesha na kuwapa majibu ya
kuwaeleza nini kinachoendelea.
Rais wetu aweze kuona na kuuchukia
mfumo na utawala wa watendaji wake wanaoendekeza ufisadi; tunajua kuwa ufisadi unawaumiza na kuwanyanyasa wananchi kwa
kuwacheleweshea maendeleo ya Taifa letu;
Je Dr, Jakaya Mrisho Kikwete
anaweza kujivunia mafanikio gani katika kipindi hiki kuelekea miaka 50 ya uhuru
wetu?
· Ameleta mageuzi makubwa katika mfumo wa elimu hakuna
mtoto wa Tanzania anayeshindwa kuingia sekondari kama ameshinda mtihani kwa
sababu sasa nafasi zinatosheleza mahitaji kwa Kuongeza majengo ya shule
za msingi na sekondari na vyuo vikuu?
· Amefanikiwa kuwapa wanawake nafasi za
uongozi ikiwemo nafasi ya Spika wa
kwanza mwanamke Mheshimiwa Ana Makinda?
· Amewezesha kuwaruhusu wananchi kuzungumzia
kero za za muungano hata kusaidia
kuondoa kero ya kulipa kodi VAT mara mbili?
·
Amefanikiwa kuwaeleza viongozi wa dini
waache biashara wa dawa za kulevya wakiwemo kwa kufanya hivyo wanaleta mfano
mbaya kwa jamii wanayoifundisha kuhusu maadili mema ambayo Mwenyezi Mungu
anawataka wawafundishe waumini wao?
· Amefanikiwa kuongeza idadi ya wanawake
katika uongozi kuanzia ngazi mbali mbali za uongozi serikalini?
· amefanikiwa kulifanya Taifa liwe na
Kiongozi wa kwanza Mwanamke kama Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dr Rose
Asha Migiro?
· Amendelea kuboresha KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA
· KWA UPANDE WA VYUO VIKUU amefanikiwa kuongeza idadi ya Wanafunzi
wanaojiunga na vyuo vikuu vilivyopo nchini Tanzania waliongezeka kwa Kuweza kujenga chuo kikuu cha Dodoma chenye uwezo wa
kuchukua wanafunzi 40,000 kwa mwaka?
· Serikali yake imefanikiwa kuongeza Idadi ya vyuo vikuu
imeongezeka kutoka vyuo vikuu kutoka 23 had zaidi ya 31
·
Aliingia madarakani kwa kishindo kwa
asilimia karibia 80.23 ya kura zote, hiyo ikiwa ni asilimia kubwa toka uchaguzi
wa vyama vingi uanze hapa nchini mwaka 1995.
·
Ameendelea kuruhusu uhuru wa habari kwa kiasi kikubwa na kuongoza
nchi chini ya utawala bora na kufuata haki za binadamu. Katika uongozi
wake ameendeleza mapambano dhidi ya rushwa kwa kuruhusu viongozi waandamizi wa
serikali kushitakiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka.
CHANGAMOTO
AMBAZO ZIKO MBELE YAKE;
MFUMUKO WA BEI
Maisha bora kwa kila mtanzania bado imekuwa ni ndoto kwani umasikini bado umeshika kasi kwani maisha ya mtanzania yakiwa yanaendelea kupanda kutokana na mfumuko wa bei yakimgusa mwananchi wa kawaida kabisa na kuporomoka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania.
MIGOMO MASHULENI
Kushindwa kutoa jibu lenye
matumaini ambalo linapingana na nia ya kila mtoto au kijana ambaye amefaulu
kuendelea na shule Migomo ya vyuo vikuu inaendelea kutikisa serikali yake kwa
kushindwa kuwapatia mikopo wahitaji dhidi ya kufaulu na lupata sifa za kujiunga
na vyuo vikuu. Nafikiri tatizo hapa sio uwezo ni kushindwa kwa bodi kubuni
mbinu mbadala wa kukidhi malengo ya Rais elimu kwa kila mtu ambaye anasifa.
sheria ya mkopo kuwa kila
atakayekidhi vigezo vya mkopo ikiwa na maana ya kupata usajili wa chuo na
kuhakikisha kuwa hana uwezo wa kujisomesha, atapatiwa mkopo. Hii inapigana na
maisha bora kwa kila mtanzania tukizingatia kuwa elimu ndio zawadi pekee kwa
vijana wa taifa hili; Baba wa Taifa aliliona hili ndio maana sisi wengi tuko
katika nafasi mbalimbali leo kwa kujitoa muhanga kwake kuhakikisha vijana wa
kitanzania wa wakati wake wanapata elimu wakiwa na sifa zinazotakawa na shule.
Serikali kushindwa
kulifanyia kazi swala hili litakuwa linapingana na nia yake njema ya kuanzisha
kwa shule za sekondari za kata, itakuwa ni ukosekanaji wa vision kwa nini
uanzishe shule nyingi za sekondari wakati huna uwezo wa kuwasaidia kutimiza
ndto zao za elimu ya juu tukizingatia kuwa shule hizo za kata wanafunzi wengi
wanasoma Shule hizi nyingi hazina walimu wala vifaa, mwanafunzi anayepata
daraja la tatu au la pili katika shule za aina hii anao uwezo mkubwa wa
kujifunza kuliko wanafunzi wengi wanaosoma katika shule za ambazo zinafaulisha
vizuri.
Taifa limeendelea kukabiliwa
na changamaoto nyingi kama ajali za barabarani, ajali za meli ambazo
zimechangia vifo vya watanzania wengi: je Rais wetu msimamo wake ni upi katika
vifo hivi vinavyoendelea kutokea? Je sheria zetu ni “ double standar”?
Tatizo la ukosefu wa
wataalam na madawa katika hospitali zetu na zahanati hasa kwa wananchi
wanaoishi vijijini bado safari ni ndefu, je tutawezaje kutatua tatizo hili? Je tutawamotisha
vipi wahusika ili wawe tayari kukaa akatika mazingira magumu ili kuwatolea
huduma watanzania walio wengi?
Pamoja na ujenzi wa shule
nyingi za sekondari za kata tatizo ambao taifa bado inakabiliana nalo ni ubora
wa shule hizo, ukosefu wa wataalam na vifaa vya kiada na makazi bora ya walimu; Hili tutalitatua vipi?
TATIZO LA UKOSEKANAJI WA
MAADILI MIONGONI MWA WATENDAJI WA SERIKALI;
Changamoto kubwa nyingine
ni hasa uzalendo na uwajibikaji wa viongozi walio chini yake ukitia shaka
machoni mwate kama Baba wa Taifa alikuwa anasema kuwa "ili tuendelee
tunahitaji watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora" Siasa safi ya
uwajibikaji, sio siasa ya kulindana hata pale wanaposhindwa kuwajibika. Uongozi
bora utumishi na uadilifu kama rais Kikwete alivyowahi sema kuwa Sheria ya sasa
inawachunguza viongozi pekee, lakini pia tunataka na watumishi wa umma ambao
sio viongozi waanze kumulikwa kwa kuwa wengi wanamilki mali nyingi
tofauti na vipato vyao halali
JE KIKWETE AMEANDIKA
HISTORIA GANI PAMOJA NA MAPUNGUFU YA UONGOZI WAKE;
· Kusaidia
kumaliza mpasuko wa kisiasa Zanzibar na kufanikisha uundwaji wa serikali ya
Umoja wa Kitaifa
·
Kuanzisha
mchakato na kusainiwa kwa sheria ya kuandikwa kwa katiba mpya ya serikali ya
muungano wa Tanzania
·
Kusherekea
miaka 50 ya uhuru wa Taifa letu katika hali ya amani na utulivu
Tusherekee kwa pamoja
popote ulipo miaka hii 50 ya uhuru wa Taifa letu na kuzidi kumwomba Mwenyezi
Mungu kuendelea kuvumiliana pale tunapotofautiana katika mazingira yeyote yale na tuendelee kukumbuka wosia wa Baba wa Taifa alitukumbusha kuwa “Tusipopambana vikali na rushwa, wananchi
watakosa imani na Serikali yao. Ni lazima tupigane na adui rushwa kwa
nguvu sawa na zile tunazozitumia katika kupingana na adui wakati wa vita”.
No comments:
Post a Comment