·
Je Ni kweli kuwa vijana ndio nguzo na
uhai wa chama chochote kiwacho?
·
Je ni kweli kuwa Vijana wanafaa kutumikia taifa lao kwa ajili
ya nguvu walizo nazo zaidi hata kama hawana elimu ya kutosha ya
uongozi?
· Je vijana wanaelewa matatizo ya vijana
wenzao na wataweza kuwasaidia haraka katika kujinasua katika atope zito la
maisha magumu pindi wapatapo nafasi ya uongozi?
· Hivi sasa wazee ndio chimbuko la
matatizo ndani ya vyetu vya siasa?
·
wazee kwa wakati huu wamechoka kuongoza chama kwa umri wao na
mawazo yao mgando?
·
wazee hawaoni wala hawasikii hoja zote
vizuri;
·
wazee ni wazito kufanya maamuzi;
·
wazee wana huruma kupita kiasi
· Ni kweli kuwa vijana hawana uwezo
kuongoza siasa za nchi zetu?
· ni kweli kuwa vijana hawana hekima ya
kutosha katika kufanya maamuzi makubwa ya kitaifa.
· vijana wana nmatatizo bado ya kuongelea
integrity (uadilifu) wa utendaji wa vyama vyao kwani wengi bado wamejiegemeza
kwa kundi fulani;
· Ni kweli kuwa vijana wote wanaoingizwa katika shughuli za siasa na kushiriki katika ngazi za maamuzi, lazima
wawe na back-up ya nguvu kabisa ya wazee.
Prof. Issa Shivji aliwahi
kusema katika moja ya mijadala ya vijana kuwa yeye ni kijana kutokana na kuwa upeo wake wa kufikiri
bado una nguvu na hutenda kazi zaidi ya ambavyo vijana kwa mujibu wa umri wao
wangeweza kufanya. Tafsiri hii ya Prof. Shivji inakuja na maswali mengi ya kujiuliza, je
ujana tuuangalie katika upeo gani? Wa umri au katka uwezo wa kuamua mambo? Kwa
upande wa Prof Shivji yeye anaangalia zaidi katika upande wa maamuzi; hata kama
umri wako ni mkubwa lakini bado uwezo wake wa kufikiri na kufanya maamuzi ni mkubwa; kwa tafsiri hii ya Shivji basi Mzee
wetu Kingunge Kombale Mwiru kama bado anao upeo mzuri wa maamuz ni kijana;
Kwa tafsiri yangu mimi
nafikiri bado Umri uchukuliwe kama ni kigezo kikubwa cha ujana; ujana pamoja na udogo wa umri vile vile
unahusisha ukakamavu, uwajibikaji wa muda mrefu hata kufikiri vizuri kwa
ufasasaha kwa hiyo bado umri ni kigezo muhimu;
Kwa nini vijana wengi
hutumika sana wakati wa kampeni au shughuli zote zinazohitaji utendaji imara wa
muda mrefu? Kwa nini wazee wasiwe mstari wa mbele katika kampeni? Kuna tofauti
kubwa kati ya mwenye umri wa miaka 45 na 70 katika kila Nyanja. Pamoja na hoja kuwa ujana sio umri, ujana ama
kijana ni upeo wa fikra pevu. Upeo wa fikra pevu ndio unaotofautisha maendeleo ndani
ya nchi.
Upeo wa fikra pevu ndio
utakao wafanya vijana kuwa “nguvu ya mabadiliko”. Bongo za vijana ndio chachu
ya mabadiliko, na ndio chemchem ya fikra mpya na mbadala zinazotarajiwa kulitoa
Taifa katika usingizi mzito wa kifikra kwa kuwa umri wao wa ujana.
Hata katika hali ya sasa
ya maendeleo ya teknologia luninga, internet n.k vijana wanapata taarifa
haraka, za kina na bila kuchujwa. Jambo hili limewafungua vijana kuelewa zaidi
haki zao, kutambua matamanio yao na kuanza kuona kuwa na wao wanaweza kufanya
vitu vinavyofanyika sehemu nyingine duniani.
·
Tatizo la mfumo wetu ni
huu kwamba wazee hawa wako kwenye umri wa kustaafu lakini hawawapi vijana
nafasi kwa visingizio uzoefu;
·
vijana hawana uzoefu, mtu
atapataje uzoefu asipopata pa kuapitia huo uzoefu?
Kwa nini wazee wasianze
kuandaa utaratibu wa kuwaandaa vijana kupata uzoefu mapema kwa kuwaandaa katika fani za uongozi kupitia elimu
na taaluma itakayowawezesha kumudu changamoto zakiuungozi bila unafiki. Pale ambapo
wazee huamua kutowasaidia vijana kupata uzoefu na kuwaacha Kujiingiza katika siasa bila elimu ya kutosha
ni sawa na kujiingiza katika jambo ‘kichwakichwa’.
Nimekuwa nikijiuliza mara
kwa mara. Kwanini viongozi wa kisiasa hawaoni haja ya kuwaendeleza kielimu
vijana wanaowasafishia njia ya ushindi wao? Kwanini vijana wanabebeshwa mizogo
mizito ambayo haina maslahi kwao wakati wa kampeni kwa kisingizio cha kuwa ni
mkereketwa wa chama husika;
· Nafikiri kwa upepo huu vijana wanatakiwa
kujitambua kuwa wao ndio kundi lenye watu wenye nguvu na kutumia nguvu hizo ziwe na
manufaa kwa jamii.
Hebu tumwangalie mheshimiwa Zitto Kabwe toka CHADEMA kijana
msomi, mahiri wa kuzungumza na mwenye nguvu za hoja na mpigaji hodari kwa ajiri
ya wananchi na maendeleo yao ndani ya Tanzania;
Ni ukweli mtupu kuwa
vijana ni nguzo muhimu katika taifa letu. Hakika vijana wanaona na wanafikiri.
Vijana hawa ambao wengi ni wasomi wa
hali ya Juu na hata wale wa kawaida wana uwezo wa kuchambua baina ya kauli tupu
na utendaji wa kauli hizo. Vijana kama mheshimiwa Zitto
Kabwe; Mheshimiwa Halima Mdee, Marehemu Amina Chifupa, Nape Mnauye, Benno Malisa, mheshimiwa Godbless
Lema, mheshimiwa January Makamba,James Mbatia, Mheshimiwa David Kafulia
na wengine wengi; Naamini, endapo kweli tukiwa tunatambua nguvu, thamani na
mchango wa vijana kama uliotolewa katika kipindi cha chaguzi zetu nchini, tunaweza kuthubutu kimaendeleo kwa kuwapa
nafasi za uongozi na wazee washuke katika basi la uongozi na sasa iwe zamu yao
kulisukuma kutoka nje na sio ndani ;
HEBU TUWAPE NAFASI YA UONGOZI NA TUONE MAFANIKIO YAO
NUKUU ZA MWALIMU NYERERE
KUHUSU KANSA YA UONGOZI TANZANIA:
·
“Viongozi wetu hivi sasa wanaogopa kutumia
nguvu za hoja ili kufikia maamuzi muhimu. Kwa sasa wanatumia hila zaidi
kuliko hoja; vitisho kwao ni mbinu rahisi zaidi kuliko adha ya kutumia akili na
kupata hoja safi ya kumjibu mpinzani katika mjadala “Viongozi hawa wakipewa
nafasi watatumia hoja ya nguvu tu; hawatakuwa na haja ya kutumia akili.
Kichini chini baadhi yao tayari wameanza kutumia hoja ya vitisho.
·
“Kama tukiacha utamaduni wa woga ukazagaa,
tutakuwa tunakaribisha udikteta. Uhuru hauji wala haudumishwi bila kuwa tayari
kulipa gharama zake; na vitu vyote vyenye thamani kubwa, gharama yake ni kubwa.
No comments:
Post a Comment