WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Thursday, December 22, 2011

JE SHERIA ZETU ZINATEKELEZEKA?


MAJANGA YANAYOENDELEA KUTOKEA KATIKA TAIFA LETU; JE SHERIA ZETU NI KWELI ZINAFANYA KAZI KAMA MSUMENO?


Hivi karibuni katika siku za kuhesabu  jiji la Dar Es Salaam, limekumbwa na mafuriko ambayo yamesababisha vifo,  upotevu wa mali na ukosefu wa makazi kwa nduzu zetu watanzania waliokuwa wananaishai  katika  maeneo haya  waliyokumbwa na mafuriko; kwa tafsiri nyingine waliokuwa wanaishi sehemu za mabondeni au sehemu ambazo maji yalijaa kutokana au na “ water level” kufikia kikomo au maji kushindwa kuendelea  na safari yake kwani hayana sehemu ya kwenda kwenda kutoka na mfumo mbovu au ulio chakaa au uliokosa mwelekea wa kisanyasi katika kuyafanya maji hayo kuendelea kutambaa kwenda baharini au sehemu nyingene ambayo ni salalma kwa maji hayo kwenda.  

Kutokana na mafuriko haya kuwa makubwa katika historia ya jiji la Dar es salaam idadi ya vifo inaweza kuongezeka kadiri siku zinavyoendelea kusonga mbele;



Kama waandishi na wataalamu wengi walivyowahi kusema kuwa” miundo mbinu hafifu imetajwa kuwa chanzo kikubwa cha mafuriko katika jiji la dar es salaam na maeneo mengine nchini ambayo nayo kwa sasa yamekumbwa na mafuriko makubw aikiwemo mikoa ya mwanza na mbeya”



Mafuriko haya kwa upande mwingine ya athari kubwa sana kwani inafahamika kuwa jiji la Dar ndilo  ambalo ni kitovu kikuu cha biashara na uchumi kwa nchi; Mvua hizo zimesababisha usumbufu mkubwa sana katika swala nzima la usafir wa wananchi wa jiji hilo kutoka kuna moja kwenda kona nyingine;

Katika kipindi hiki cha kutapatapa kwa wahusika katika kushughulikia swala hili hoja tofautitofauti zitaendelea kuzungumzwa kama hizi;

·        “Tulishatangaza watu wahame mabondeni jamani, lakini bado wanaendelea kukaa tu huko na haya ndio matatizo yenyewe”

·        Gazeti la HabariLeo katika moja ya vichwa vyake lilenadika kuwa “Tusisubiri kupata hasara tuhame wenyewe mabondeni”

·        “Jamani mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, Serikali ifanye nini ili ionekane inawajali watu wake?

·        Ikiwa watu hawa walishaelezwa wazi kuwa eneo hilo si maalumu kwa makazi, ni bonde na si salama hivyo wahame lakini bado wanaendelea kukaa na maafa yanapotokea lawama zinatupiwa serikali, hii si haki jamani”. 

·        “Inapotolewa tahadhari ya watu wanaoishi maeneo ya hatari kama hayo kuhama pia napo inasubiriwa Serikali iwatoe kwa nguvu? Mvua inaponyesha na maji wanaona yanaongezeka na kuzidi kujaa bado napo inasubiri Serikali iwaambie maji yanawafika viunoni ondokeni jamani! “

·        “Mimi nadhani kila mtu anatakiwa asimame katika nafasi yake, mwananchim wanasiasa na serikali kila mtu atimize wajibu wake kwa maslahi ya Taifa si maslahi binafsi.”

Hizi ni baadhi tu ya hoja kuhusiana na hali halisi ya tukio na nini kifanyike katika kufanikisha swala nzima ka kusimamia na kuwasaidia watanzania wenzetu ambao wamekumbwa na mkasa huu, sio tu kwa sasa na hata baadae;


Mimi najiuliza maswali mengi ambayo mengi kati yake sijeweza kupata majibu ya moja kwa moja kwa haraka; Najaribu kutafakari tukio hili kwa leo na matukio mengine ambayo yanafanana na haya na ambayo yanaendelea kulisababishia taifa hasara ya kubwa wa kupoteza nguvu watu kuleta hasara kubwa kwa Taifa letu kiuchumi na kulirudisha Taifa nyuma kimaendeleo na hasara ambayo tunaweza kabisa kuikabili hata kwa asilimia 80%;

·        Je ni kweli kuwa sheria zetu zimetungwa ili kumsaidia mtanzania bila kuogopa kwa manufaa na masilahi ya Taifa?

·        Sheria zimetungwa na zinafanya kazi kwa ubutu zikiishia tu katika maneno zaidi na sio utekelezaji wake?

·        Je ni kweli sheria zetu ni kama msumeno kwa maana zinatakiwa kukata mbele na nyuma na kwamba hazitakiwi kuchagua  pa kukata?

·        Je kama sheria kweli ni msumeno mbona Taifa linaendelea kushuhudia majanga yakitokea ambayo ni udhaifu wa utekelezaji wa sheria hizo?

Namkumbuka Dr. Magufuri alivyosimamia watedaji walioshindwa kufanya kazi yao inavyotakiwa kwa kujenga ofisi ya Tanroads katika hifadhi ya barabara; alisimama kidedea na kuhakikisha kuwa jingo hilo linabomolewa, na lilibomolewa; kama taifa lazima tukubali kuwa sheria  lazima iheshimiwe;

·        Je wananchi ambao wanaishi katika mabonde ambayo sio salama kwa makazi yao hasa wakati wa maafa au mafuriko kama haya, waliruhusiwa na nani?


Kama serikali ambayo ndo iriwarusuhukupitia watendaji wake kwa sababu moja au nyingine basi pamoja na maafa haya makubwa hakuna sababu ya kuwalaamu wananchi, ni jukumu la serikali kuhakikisha kuwa inawasaidia katika kuhakikisha kuwa wanakuwa salama na baada ya tatizo kutoweka maji kwisha inawajibika kuwatengenezea makao yao vizuri katika maeneo ili waweze kuendelea na maisha yao ya kila siku;

Lakini kama wananchi  na wathirika wa mafuriko haya  wanaisha katika maeneo haya kinyume cha sheria na agizo la serikali, na walivamia tu makazi haya  basi ni wajibu wa serikali kuhakikisha kuwa Watanzania wezetu wanatafutiwa mahali salama pa kuishi na sio kuwaruhusu kuendelea kuishi katika maeneo haya ambayo sio salama hata kiafya;

·     Kwa nini tuendelee kumsikitikia Mwenyezi Mungu kwa uzembe wetu?

Siku zote sheria ni msumeno, hukata mbele na nyuma. Hivyo ni jukumu la sheria kulinda unapokuwa katika mwelekeo sahii  na kuhukumu unapoikiuka. Kwa matazamo huu niauliza tena hapa kama nilivyowahi kuuliza huko nyuma Je Msimamo wa Dr. Magufuli katika kusimamia sheria ambazo zimepindwa na watendaji wenginine ni sahihi?  Je taifa linahitaji watendaji kama Dr. Magufuli na Prof. Tibaijuka katika kuleta usawa mbele ya sheria na katika utendaji kazi wao kulingana na katiba na sheria za nchi?
Prof. Tibaijuka katika harakati zake za kusimamia sheria amekuwa akisema na kusisitiza kuwa;

·        “Tumeshatoa tangazo kwa wahusika juu ya kuhama maeneo hayo, sheria zimetungwa na kupitishwa na Bunge ili zifuatwe, hivyo jukumu letu ni kuzifuata”.

  “…Kuzitekeleza ni wajibu, safari hii tutafanya kazi bila kumwangalia mtu usoni, sheria zitafuatwa kwa wale waliojenga kinyume na sheria na maeneo ambayo si rasmi wakae chonjo,”

Nakumbuka kuwa Profesa Anna Tibaijuka, amewataka wakazi wa eneo la Jangwaji na wanaoishi eneo la Bonde la Msimbazi Dar es Salaam, wahame katika eneo hilo kabla Serikali haijawachukulia hatua.

·        “Wananchi wengi hawazijui sheria za kumiliki maeneo, ndiyo maana wengi wao wanaishi sehemu zisizo halali kwa makosa, na ndiyo maana mnaona wengine wanaishi Jangwani ingawa siyo eneo la makazi bali ni eneo maalum kwa ajili ya kuegeshwa magari.

WATAALAMU WETU WA MIPANGO MIJI BADO WANAENDELEA KULALA USINGIZI MNONO? 

Leo tunavyoendelea kushuhudia  maafa haya makubwa ya mafuriko ambayo yamesababisha maafa makubwa kwa taifa letu; je chimbuko lake nini?

Nafikiri wataalamu wa Mipango Miji  wataendelea kulaumiwa kwa sababu wao ndio waliochangia maeneo ya wazi kuvamiwa na watu bila kufuata utaratibu na kanuni za kisheria kama hawakuhusika mara moja. Kwani hata kama wananchi walivamia maeneo hayo walikuwa wanawaona na kwa nini waliamua kuwaacha waendelee kujenga na kulindikana:

Nafikiri pamoja na utaalamu wao  wameshindwa kuwaelimisha na elimu katika jamii kuhusu umiliki wa maeneo na pia hawatoa ramani zinazoonyesha maeneo ya wazi amabyo hayaruhusiwi kwa makazi.

JE WANANCHI WANAMCHANGO GANI KATIKA TATIZO HILI NA MATATIZO YANAYOFANANA?

Kama alivyosema Prof.Tibaijuka “Tumegundua wananchi wengi wanaofanya udanganyifu katika maeneo wanatumia ramani za kukopi, kitu ambacho ni udanganyifu, wanafanya hivi katika kuwaibia wananchi,”

Wananchi wakati mwingine hatujali na tunavuja sheria kusudi kwa kujua kuwa watendaji wetu wasimamizia wa sheria si wawajibikaji na wameshindwa kuthubutu katika kusimamia sheria hizo;
Wananchi wakati mwingine tumekuwa wabishi lakini tatizo likitokea kama hili majuto yanarudi kwetu na sio kwao; athari zinabaki kwa mwananchi na serikali inaendelea kuwa na utamu tu wa maneno;

Kiburi na ukorofi na urahisi wa mambo utagharimu sana maisha yetu na vizazi vyetu wananchi tunatakiwa kufuata sheria zaidi na sio kulazimisha kukaa katika sehemu ambazo zimetafitiwa sio salama kwa makazi ya kudumu ya binadamu;
Kwa kweeli sheria inatakiwa kuwa msumeno ambao unaweza kutukata pande zote mbili kuruka; na sheria kamwe isiwe jambia kuwa anayeathirika na jambia ni Yule tu anayekamata kwenye makali;

vita  ya kusimamia utekelezaji wa kweli wa sheria wahusika wanatakiwa kuwa wawajibikaji wa kweli kwani jamii imevurugwa na nguvu ya fedhakatika usimamizi wake. Hivyo, uwezekano wa kukwamishwa, kusalitiwa au kuingizwa mkenge na mafisadi kupitia kwa baadhi ya watumishi wa wizara husika wataendelea kukwazwa katika kusimamia  sheria na kanuni za kulinusuru Taifa na majanga kama haya.
   
wasimamizi wa sheria tunaendelea kuwashauri wasiogope kujitoa  muhanga iwapo watalazimika kufanya hivyo, kwani huo ndiyo utakuwa  mchango wao katika kuleta ukombozi katika ustawi wa jamii yetu  na kwa usimamizi wao ambao utakuwa umetukuka basi itakuwa rahisi sana kwa wananchi kwa umoja wetu kuunga  mkono  jitihada hizi kwa faida yetu na Taifa letu. Siasa itusaidie kuimarisha na kutekeleza sheria na tusitumie mwanya wa siasa kuogopa kusema ukweli kwa kuogopa kukosa kuchaguliwa kwa kusimamia ukweli ambao pengine utawaudhi wananchi, na kuliletea hasara taifa kama tunavyoendelea kushuhudia sasa;

No comments:

Post a Comment