BADO TUNAHITAJI BUSARA
ZAIDI KATIKA MAAMUZI YETU KULINGANA NA HALI YETU YA UCHUMI;
- ·“Siasa si mchezo mchafu, ila wachezaji wake ndiyo wachafu.”
- · Je bunge letu linapofanya maaumuzi ya liko kwenye dhana ya “wao” na “sisi”
- Ni kweli kuwa Siasa hutafasiriwa kuwa ni fikra, busara na mipango ya kuendesha nchi au ya kujinufaisha wao wenyewe?
- · Litakuwa ni jambo la kuheshimiwa kwa viongozi wetu kama Waheshimiwa Wabunge wetu watakuwa wakweli na wenye Uzalendo wa kweli ndani ya mioyo kwa faida ya wananchi wao.
· Confucius aliwahi sema kuwa ‘Utajiri
na vyeo ndivyo vitu ambavyo kila bianadamu anavitamani; lakini ikiwa njia ya
kuvipata ni kwa kwenda kinyume na misingi yake, anapaswa ajiepushe navyo.’
· Rudolph Giuliani aliwahi
sema kuwa ‘Kiongozi huchaguliwa kwa
kuwa yeyote anayemuweka pale huwa anaamini maamuzi, tabia na uwezo wa maarifa
yake – siyo ujuzi wa kufuata maoni. Ni wajibu wa kiongozi kuchukua hatua
kufuatana na sifa hizo.’
·
“kiongozi ajiulize ni vipi
atalitumikia Taifa na si Taifa kumtumikia yeye Kiongozi Umashuhuri na uzuri wa
Kiongozi unatokana na hekima, busara, uchapakazi, ufanisi, ufuatiliaji, uimara,
uungwana, uwajibikaji na unyenyekevu wake. Ama fikra endelevu na upeo wa
kuongoza ni muhimu na si kauli tamu za kuwafurahisha viongozi wengine”
· Tamaa ya kujilimbikizia mali
huo ni udhaifu wa mwanadamu ambao hapaswi kuupa nafasi iwapo unazingatia
uadilifu wa uongozi
Demokrasia kama falsafa ya
Plato ambayo inahusiana na uendeshaji wa shughuli za kisiasa inalenga zaidi
katika utumishi kwa umma na uendeshaji
wa jamii na taifa. Wananchi wote hawawezi ongoza nchi kwa mara moja; Katika
msingi huu wananchi kutokana na wingi wao waliridhika itakuwa sio rahisi kwa
wao wote kukutana, kufanya maamuzi na kuyasimamia moja kwa moja maamuzi hayo
yanayowahusu wao kama jamii; dhana ya kuwachagua viongozi wachache huzaliwa kwa
chimbuko hili na kuruhusiwa kuunda serikali.
Tatizo kubwa tulilonalo
kama Taifa ni ufinyu wa viongozi bora na utashi binafsi wa wachache walio
katika nyanja za uongozi kwa kukosa sifa muhimu kwa viongozi. Kwani inatupasa kutambua
kuwa uongozi si lelemama, ni kipaji na ni kazi ngumu. Lakini ridhaa hiyo
haitolewi hivi hivi tu, inaambatana na amana, kwamba waongozi watatekeleza
dhamana na wajibu wao kwa makubaliano na maelewano ya kufuata
barabara na kuheshimu ipasavyo kanuni na maadili fulani yanayoitambulisha
na kuiongoza jamii husika.
Kwa kauli zinazotofautiana
na misimamo inayotofautiana kuhusu ongezeko la Posho za waheshimiwa Wabunge
hivi karibuni, tunapo yakidirifu maisha
ya kila siku ya wanasiasa ataiona siasa imejikita katika kukimbilia na
kupigania nafasi, fursa na ushawishi kwa malengo ya kujilimbikizia utajiri
binafsi kwa wengi ; ikumbukwe kuwa kiongozi muadilifu hakubali kufuata au kutoa maamuzi bila kufanya ukadirifu wa
hoja na hali husika. Uongozi ni kujitolea na kuweka matwakwa na maslahi ya
wengine kuwa mstari wa mbele na si matakwa binafsi na kujinufaisha. Marehemu
John Kennedy rais wa Marekani alitoa kauli moja maarufu iliyosema kuwa. Tuchague
viongozi si kwa kuangalia vyama au sura, bali tuangalie uwezo wao wa kuongoza,
kuhamasisha na kufanya kazi. Tupime kauli zao na matokeo ya kazi zao kama
wanavyojinadi.
Serikali ni watu, inaundwa
na watu tuliowachagua na tunawapa watu hawa na Serikali mamlaka makubwa ya
kutuongoza, kupanga na kulinda Taifa na Katiba yetu. Dhamana hii imefanywa kwa
kuaminiana kuwa Serikali itafanya kazi kwa manufaa ya Wananchi wake na kwa
matakwa na utashi wa Wananchi wake.
Maaumuzi ya ongezeko la
Posho kama kweli yamepata Baraka zote za serikali basi tujue wazi kuwa uamuzi
huu haujezingatia mazingira ya Taifa letu, na uwezo wetu wa kifedha kwa wakati
huu. Maaumuzi ya Bunge na kwa wabunge kuridhia kupokea posho hizo kunawafanya
wananchi wajiulize maswali mengi
· Kuna amani gani na
utulivu gani katika nchi yetu wakati mioyo yetu sisi kama wananchi imevimba kwa
kujaa hasira za ubinafsi?
· Je mwananchi wana nafasi
gani katika kuiendesha nchi hii? Wasubiri kuongozwa tu. Mawazo ya wabunge ndiyo maoni yao?
Mheshimiwa Rais, busara
yako inahitajika sasa kuliko wakati mwingine wowote kwa kuangalia hali halisi
ya maisha ya mwananchi wa kawaida na mateso ya hali ngumu inayomzunguka,
pengine ile aliyoisema Mheshimiwa Spika wa Bunge letu kuhusu hali ngumu ya
maisha ya wabunge wetu sio kitu. busara yako Mheshimiwa Rais inahitajika sasa
kuliko wakati mwingine wowote ili kudumisha amani na utulivu wa kweli
Kama ilivyo kwa umoja wa
kitaifa, kiongozi muadilifu pia hufanya kila bidii kuhakikisha amani na utulivu
wa kweli katika nchi vinapatikana. Amani na utulivu ni chachu ya wananchi kwa
kushirikiana na Serikali yao kujiletea maendeleo. Maendeleo hayaji mahala penye
magomvi na hasama. Lakini na amani na utulivu pia haviji mahala pasipo na haki
na uadilifu. Uvunjifu wa amani na utulivu wa nchi hupelekea hasara ya maisha na
mali ya watu na hayo hayawi malengo ya uongozi muadilifu katika nchi
Uadilifu wa uongozi unadai
kuheshimu nguvu ya hoja na fikra bora na hayo yanaweza kupatikana tu iwapo nchi
inaongozwa kwa misingi ya kidemokrasia. Hivyo, katika kutoa uongozi sahihi, kwa
kuzingatia maslahi bora ya nchi na watu wake, haki, uadilifu, umoja, amani na
utulivu, hapana budi kwa kiongozi kuiamini, kuiheshimu na kuifuata barabara
misingi ya kidemokrasia.
Bado binadamu si mkamilifu
na kwa vyovyote vile hufikia mahala akafanya maamuzi ambayo si sahihi hata kama
yalifanywa kwa nia njema na kwa kuzingatia taarifa zilizopatikana wakati
maamuzi hayo yanafanywa. Hayo yanaeleweka na kiongozi muadilifu anapaswa
kuyakubali na kuliomba radhi Taifa. Hiki ndiyo kilele na kigezo kikuu cha
uadilifu wa uongozi katika siasa. Kukubali kubeba dhamana kwa madhara
yaliyotokana na maamuzi yako au yaliyofanywa kwa jina lako.
Maamuzi ya kiongozi wa
kisiasa huathiri taifa zima, busara na hekima huzaa maamuzi yanayotokana na
tafakuri ya kina, yanayozingatia hali halisi ya mambo na maslahi na manufaa ya
muda mrefu. Kiongozi muadilifu anatakiwa ayaone haya na ayazigatie kwa kila
hatua anayochukua. Kama viongozi wetu wa bunge wakikiri kuwa walikurupuka
katika kufanya maamuzi hayo bila kuyafanyia kazi vizuri heshima na uwajibikaji
wa kuliendesha bunge letu itarudi. Tukubali tu kuwa njia ya kusonga mbele ni
kukubali kutofautiana katika fikra lakini tubaki kuwa wamoja.
Mheshimiwa Spika ni ukweli
ambao haufichiki kuwa kwa sasa wananchi ndio wenye maisha magumu kuliko wabunge
unaowatetea.
No comments:
Post a Comment