WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Wednesday, November 14, 2012

SAFU MPYA YA SEKRETARIETI YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CHAMA CHA MAPINDUZI



Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) kimekutana katika Ukumbi wa mikutano wa Makao Makuu ya chama, maarufu kama Whitehouse mjini Dodoma,leo tarehe 14th Nov 2012.
Nafasi ya Katibu Mkuu, alimpendekeza Mhe. Abdulrahaman kinana.

Kikao hicho kitajadili juu ya kuunda na kupitisha majina yaliyopendekezwa  na Mwenyekiti wa ChaCha Mapinduzi Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, ya wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama ya Taifa (CC) pamoja na uundaji wa sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa. Ambapo Mwenyekiti wa Chama kwa mujibu wa Kanuni na Katiba ya Chama Cha Mapinduzi, anayo fursa ya kuteua wajumbe kumi(10) wa Halmashauri kuu ya Taifa, ambapo  Mwenyekiti aliwateua wajumbe wanne(4) na akabakiza nafasi nyingine sita (6) miongoni mwa wajumbe hao ni Mhe. Asha-rose Migiro, Mhe. Zakhia Meghji, Mhe. Nape nnauye na  Mhe. Abdulrahaman Kinana.


Katibu wa Siasa na Mahusiano ya Kimataifa, Asha-rose Migiro.

Baada ya uteuzi huo Mwenyekiti pia alipendekeza majina ya Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa, ambapo alipendekeza majina yafuatayo;

1.     Nafasi ya Katibu Mkuu, alimpendekeza Mhe. Abdulrahaman kinana.
2.     Nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Zanzibar,  Mhe. Vuai Ali Vuai.
3.     Nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Bara, Mhe. Lameck Madelu Nchemba.
4.     Katibu wa Oganaizesheni ni Ndugu Mohamed Seif Khatibu.
5.     Katibu wa Siasa na Mahusiano ya Kimataifa, Asha-rose Migiro.
6.     Katibu wa Uchumi na Fedha, Zakhia A. Meghji 
7.     Itikadi na Uenezi: Ndugu Nape Moses Nnauye


  
Itikadi na Uenezi: Ndugu Nape Moses Nnauye

Baada ya mapendekezo hayo, Halmashauri Kuu ya Taifa ilipitisha majina hayo na kuyakubali kuwa hao waliopendekezwa ndio hasa wanaofaa kuwa wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa.
 
 Katibu wa Uchumi na Fedha, Zakhia A. Meghji.

Pia, Mwenyekiti akawashukuru wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa waliopita na pia kuwataka wajumbe wapya kuchapa kazi, na kuwataka kujenga mustakabali wa Chama, Uimara na Umadhubuti kwa kufanya kazi kwa kushirikiana na kusaidiana.

Nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Bara, Mhe. Lameck Madelu Nchemba.


Katibu wa Oganaizesheni ni Ndugu Mohamed Seif Khatibu.


Nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Zanzibar,  Mhe. Vuai Ali Vuai.

No comments:

Post a Comment