WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Tuesday, June 4, 2013

Uchambuzi Wa Rasimu; Tano Zangu Kwenye 50 Pasenti Ya Urais!


9 49808

Ndugu zangu,
Naanza kushiriki kuichambua rasimu ya KATIBAkwa kuangalia kipengelea Uchaguzi wa Rais.
Naam, Katiba ya Nchi inatakiwa pia kuchangia kwenye kuondoa hofu zilizopo kwenye jamii husika. Kwa Nchi Yetu, moja ya hofu hizo ni UDINI.
Nawapa alama 5 ambazo ni za juu kabisa( Kwa Kipimo Changu) Wajumbe wa Tume Ya Katiba. Ni  kwa kutanguliza busara na hekima na kutuletea muarobaini wa Udini hapa nchini kwetu.
TUME imefanya kitu kikubwa sana kwa kupendekeza kuwa Mgombea Urais atangazwe mshindi anapopata asilimia 50 ya kura zote, hiyo kiufundi itakuwa 50 plus 1.
Tafsiri yake?
 Huo ni muarobaini wa udini na hata siasa za ukanda. Maana, hili la udini kwa kiasi kikubwa limechagizwa na wanasiasa. Na sasa, ili mwanasiasa au chama cha siasa kiweze kuungwa mkono na zaidi ya asilimia 50 ya Watanzania itabidi  kijinadi kwa masuala ya kuwasaidia Watanzania bila kujali tofauti za dini zao au hata kanda zao.
Maana, kwa nchi yetu, Mungu ameijalia kwa kutokuwa na dini yenye waumini wanaofikia asilimia 40ya Watanzania wote. Bado kuna wasio Wakristo wala Waislamu.
Hivyo, ili mgombea Urais aweze kufikia asilimia 50, atahitaji kuungwa mkono na hata wasio wa dini yake. Na akianza kuhubiri udini , basi, huyo ajihesabu kuwa atabaki kuwa ’ Rais’ wa Watanzania wa dini yake!
Kwa mara nyingine, pokea 5  zangu,  Tume ya Warioba kwa kuliona hili! ( Soma hapo chini nilichoandika kwenye moja ya makala zangu kwenye safu ya Mraba wa Maggid, Raia Mwema)
Maggid Mjengwa,
Iringa.
0754 678 252
Nilipata kuandika;
”Utaratibu huo unaua ukabila na kujenga vema misingi ya Utaifa. Hata kama itachukua muda kufika mbali zaidi katika hilo lakini Wakenya wameanza kuondokana na ukabila kwenye siasa zao, kwa kupitia Katiba.
Kwa mantiki hiyo hiyo, Watanzania tungeweza kabisa kuondokana na siasa za udini kwa kuweka, kwenye Katiba yetu ijayo sharti la mgombea Urais kushinda kwa asilimia 50+1 ( Asilimia 50 jumlisha kura 1). Hilo lingewafanya wanasiasa wetu wenye kuwania Urais na vyama vyao pia ‘ Kutia akili’.
Maana ingekuwa na tafsiri moja kuu; kuwa mgombea na chama chenye kuendekeza udini kisingekuwa na nafasi ya kutoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wala nafasi ya kushika dola. Maana, hakuna dini hapa Tanzania yenye idadi ya waumini wanaovuka asilimia 50 ya jumla ya Watanzania.
Kwa maana, hiyo, muarobaini wa kumalizana na udini uko kwenye Katiba ijayo, kama tuna nia ya dhati ya kutoka hapa tulipo. Vinginevyo, udini huu tunaosema kuwa ni tatizo tutakuwa tunaulea wenyewe.
Hata tatizo la siasa za ukanda nalo litapotea, maana, hakutakuwa na mgombea au chama kitakachoweza kushinda na kutoa Urais kwa kuegemea kura za kikanda. Hakuna kanda itakayovuka peke yake asilimia 50 ya kura zote. Chama na mgombea kitahitaji kuungwa mkono na wapiga kura wa kanda hata zilizo nje ya anakotoka mgombea Urais.
Vinginevyo, kama alivyotamka Uhuru Kenyatta kwenye hotuba yake nzuri iliyojaa utaifa hivi majuzi, kuwa katika uchaguzi waliofanya, kila kura ilikuwa ina umuhimu. Hivyo, kila kabila lilikuwa na umuhimu. Na Uhuru Kenyatta akaweka wazi anachotaka Serikali yake kwa kushirikiana na Wakenya kufanya ili kuitoa Kenya hapo ilipo na kwenda mbele.
Kenyatta alimalizia na maneno matatu; Forward, Foward. Foward!- Kusonga mbele!
Ndio, Wakenya wameamua; KENYA KWANZA!
And really, The Kenyans are coming, Big Time!”- Maggid Mjengwa, Raia Mwema.

No comments:

Post a Comment