WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Saturday, June 15, 2013

Bomu lalipuka kwenye mkutano wa CHADEMA, Soweto, Arusha

 
 
Watu wawili wanahofiwa kupoteza maisha na wengine wengi kujeruhiwa kutokana na mlipuko wa bomu lililolipuka kwenye mkutano wa CHADEMA katika eneo la Soweto, kata ya Kaloleni jijini Arusha, wakati wa kufunga kampeni za uchaguzi wa madiwani katika maeneo ya jiji hilo.

Waliojeruhiwa wamekimbizwa katika hospitali za Seliani na Mount Meru ambapo baadhi ya watu wamejitolea vyombo binafsi vya usafiri na wengine wanashirikiana na Madaktari na Wauguzi wa hospitali hizo kutoa huduma ya kwanza.

Kamanda wa polisi mkoani humo, Liberatus Sabas yupo katika moja ya hospitali hizo.

Bomu hilo linaelezwa kuwa lilipuka kwenye mkusanyiko wa watu meta chache kutoka jukwa kuu, mwendo wa saa kumi na mbili kasoro robo jioni wakati mkutano huo ulipokuwa umekwisha na shughuli ya kukusanya michango ikiendelea.

Viongozi wa juu wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Godbless Lema walikuwepo na wameendelea kuwepo kwenye eneo hilo.

Polisi wapo katika eneo hilo wakijitahidi kutuliza ghasia lakini inasemekana upo upinzani mkubwa kutoka kwa wananchi wanaojaribu kuwafukuza, hali iliyowalazimu kupiga mabomu ya machozi na kukamata watu kadhaa wakiwemo viongozi wa CHADEMA. Mwandishi mmoja wa habari anaripotiwa kunyang’anywa kamera yake baada kwa kupiga picha, hata baada ya kujitambulisha.

Watu wenye hasira wanaripotiwa kuyashambulia na kulipasua kioo gari la kutoa huduma ya kwanza (ambulance) la hopitali ya Mt. Meru lenye namba STK 8493, kwa kuwa lilichelewa kufika kuwaokoa majeruhi.

ILANI: Baadhi ya picha zilizopachikwa hapo huenda zikagusa  hisia ya mtizamaji, tafadhali ikiwa huwezi kuvumilia kuona damu usibofye tarakimu zilizopo hapo chini kufungua picha zinazofuatia.
 

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

No comments:

Post a Comment