WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Saturday, June 22, 2013

Neno La Leo; Ishara Za Dhoruba Kuu Linalokuja...

10 ce5c4
Ndugu zangu,
BAHARINI ishara za Dhoruba Kuu ama ' Zildhirai' linalokuja ni mawimbi madogo madogo yanayotangulia wimbi kuu, kisha huja dhoruba. Zildhirai.

NCHI Yetu inapitia sasa kwenye kipindi kigumu sana kuwahi kutokea katika historia yake.

Kila ninaposhika magazeti na hata kuangalia runinga na kusikiliza redio, naiona hatari kubwa sana kwa taifa letu. Naziona ishara za Zildhirai inayokuja. Ni dhoruba. Na dhoruba ikitua haitatuacha salama kama taifa. Kuna kusambaratika.

Ndugu zangu,

Tuna uwezo wa kulizuia wimbi hili lisije kuleta maangamizi kwa nchi yetu. Ni wakati wa kutanguliza hekima na busara za hali ya juu. Sioni kwanini mpaka leo hii viongozi wa dini, siasa na Serikali hawajakaa kwenye chumba kimoja kujadiliana kama Watanzania. Kuona, na kwa kutanguliza maslahi ya Nchi Yetu na vizazi vyake, ni kwa namna gani tutatoka kwenye tope hili. Maana, kama taifa tuko, katika hali ya kunasa topeni. Na hatuwezi kumsubiri Mwalimu arudi aje atunasue.

Kwa mimi ninayeamini katika Ujamaa na Kujitegemea,( Social Democrat) naiona sababu kubwa ya mkanganyiko uliopo sasa na wenye kuzaa hofu ya dhoruba kuu ni kukosekana kwa kiasi kikubwa kwa usawa kwenye jamii.

Kwa jamii kuwa na kiwango kikubwa cha kukosekana kwa usawa ni sawa na mtu kuvaa viatu vya kubana. Vinaumiza miguu unavyotembea navyo. Na viatu kubana ina tafsiri ya taifa kushindwa kutambua rasilimali watu zilizopo na kuzisaidia ili ziweze kuinuka na kuchangia kwenye ustawi wa taifa. Kuwaacha wachache wakineemeka na wengi wakitaabika.

Kwenye jamii yoyote iwayo, pengo la wenye nacho na wasio nacho likipungua, basi, hupelekea kwenye uwepo wa jamii yenye watu wenye unafuu katika maisha. Hupelekea kupunguza hasira za wasio nacho. Hivyo, hupelekea jamii ambayo viatu vyao havitawabana sana na kuwasababishia maumivu makali wanapotembea.

Na kwenye ubongo wa mwanadamu kuna kitu kinaitwa Oxytocin. Hizo ni hormones ambazo huathiri mahusiano yetu kijamii. Na huathiri kwenye imani zetu kwa wanadamu wenzetu.

Kwamba , yumkini, moja ya sababu zinazopelekea mikanganyiko katika jamii ni kukosekana kwa imani. Kukosekana kwa imani miongoni mwetu. Kwamba hatuaminiani. Na kukosekana kwa imani kwa jamii dhidi ya mamlaka.

Na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon alipata kusema; kuwa tatizo kubwa Africa sio budget deficits za Serikali, kwa maana ya kupungua kwa bajeti, bali, Trust deficits- Kupungua kwa Imani.

Naam, kufikiri ni kazi, lakini itakuwaje, kama taifa, tukiacha kazi ya kufikiri?
Maggid Mjengwa,
Iringa

No comments:

Post a Comment