WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Tuesday, June 18, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT GHARIB BILAL AWAJULIA HALI MAJERUHI WA BOMU LA ARUSHA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia hali, Gabriel Kivuyo (52) aliyelazwa Hospitali ya Rufaa Selian, baada ya kujeruhiwa na mlipuko wa bomu katika mkutano wa Chadema, mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Arusha. Makamu wa Rais, jana Juni 17, alifanya ziara ya kuwatembelea kuwajulia hali majeruhi wa mlipuko huo waliolazwa katika hospitali za Mount Meru, Selian na Mtakatifu Elizabeth.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia hali, mtoto aliyetambuliwa kwa jina moja la Fahad (7) aliyelazwa katika chumba cha watu mahututi Hospitali ya Rufaa Selian, baada ya kujeruhiwa na mlipuko wa bomu katika mkutano wa Chadema, mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Arusha. Makamu wa Rais, jana Juni 17, alifanya ziara ya kuwatembelea kuwajulia hali majeruhi wa mlipuko huo waliolazwa katika hospitali za Mount Meru, Selian na Mtakatifu Elizabeth.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa picha ya X-Ray, ya mmoja kati ya majeruhi waliolazwa kwenye Hospitali ya Mount Meru, Joseph Anthony, mkazi wa Karoleni, baada ya kujeruhiwa katika mlipuko wa bomu lililotokea wiki iliyopita katika mkutano wa Chadema eneo la Soweto jijini Arusha. Imeelezwa kuwa hadi jana Juni 17, 2013, wakati makamu alipowatembelea majeruhi hao watu watatu waliliripotiwa kufariki dunia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia hali, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Majengo A, Sarah John (45) aliyelazwa Hospitali ya Mtakatifu Elizabeth, baada ya kujeruhiwa na mlipuko wa bomu katika mkutano wa Chadema, mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Arusha. Makamu wa Rais, jana Juni 17, alifanya ziara ya kuwatembelea kuwajulia hali majeruhi wa mlipuko huo waliolazwa katika hospitali za Mount Meru, Selian na Mtakatifu Elizabeth.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na wananchi wa jijini Arusha waliokusanyika nje ya Hospitali ya Mount Meru jana, wakati Makamu alipokuwa na ziara ya kuwatembelea kuwajulia hali majeruhi wa mlipuko wa Bomu uliotokea wiki iliyopita katika mkutano wa Chadema jijini Arusha, ambapo jumla ya watu 70 walijeruhiwa na watatu walifariki dunia. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mwilongo. 
 
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

No comments:

Post a Comment