WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Sunday, June 16, 2013

Neno La Leo; ” Hell Is The Other People!”- Jehanam Ni Wale Wengine!

9 9f578

Ndugu zangu,
Mwanafalsafa Jean- Paul Sartre anasema; “ Hell is the other people” – Kwamba jehanam ni wale wengine. Anataka pia tukubaliane, kuwa pepo yaweza kuwa ni wale wengine.

Na hakika, tofauti ya mwanadamu na mnyama iko kwenye kufikiri. Mnyama anaongozwa na hisia, lakini mwanadamu anapaswa aongozwe na kufikiri. Ndio maana ng’ombe anaweza kumpanda mama yake. Ni hisia tu zitakazoongoza tendo lake.

Hivyo, mwanadamu kwenye mambo ya msingi hapaswi
kabisa kuongozwa na hisia ikiwamo ushabiki. Anapaswa kufikiri. Na zaidi kufikiri kwa bidii.
Vinginevyo, ni ukweli, kuwa kijamii, mwanadamu anaweza kuwa kiumbe anayeishi kwenye mahusiano ya kirafiki na kiadui na wenzake. Na katika hilo la uadui, wanadamu, kama ilivyo kwa wanyama, wanaweza kushindania na hata kugombania vingi; iwe fedha, mashamba, wanawake na hata kivuli cha mti.

Ndio, unaweza kabisa kuwakuta wanadamu wawili wanagombania kivuli cha mti, kwamba nani mwenye haki ya kukaa kivulini. Na wanaweza kugombana mpaka akatokea mwendawazimu atakayekuja kuukata na huo mti wenyewe. Na wanadamu hao watabaki wakitazamana juani.

Mara nyingi, migogoro husababishwa na kugombania kisichotosha. Hivyo, lililo la msingi ni kutambua, kuwa wanadamu tunategemeana. Kwamba panapo kushindania jambo, mwanadamu, tofauti na mnyama, anapaswa kufikiri sana. Atangulize kwanza hekima na busara.

Na kwenye mgogoro wowote ule, mwanadamu ayape mazungumzo nafasi ya pekee katika kufikia muafaka, na si vurugu au mapigano. Kwenye mgogoro, na kwenye kuitafuta amani, panakosekana mazungumzo, basi,  ina maana ya uwepo wa mazingira ya kuvunjika kwa amani.

Na wanadamu sisi tumekuwa wepesi sana wa kunyosheana vidole na hata kuhukumiana pasipo kudadisi ili kuujua ukweli.

Na hapa nawaletea leo kisa cha wanandoa waliokaa miaka mingi bila kupata mtoto. Wakaamua wamfuge paka nyumbani. Naye paka huyo wakampenda sana kama mtoto wa kumzaa. Paka naye aliwapenda sana bwana na bibi nyumbani.

Ikatokea mke yule akapata mimba na hata kuzaa salama mtoto. Ikawa kama miujiza. Furaha nyumbani ikaongezeka.

Siku moja bwana na bibi walimwacha mtoto wao amelala kitandani. Nao wakaenda zao kuwasabahi jamaa na marafiki.

Walipokaribia nyumba yao wakati wakirudi nyumbani wakshtuka sana. Walimwona paka wao nje ya mlango akiwa na kipande cha nyama mdomoni. Sura yake ilitapakaa damu pia.

Wote wawili wakachukua miche ya kutwangia nafaka.  Kwa hasira wakamtwanga paka yule kichwani. Alikufa papo hapo.

Walipoingia chumbani wakamkuta mtoto wao amelala salama kitandani. Kando kuna nyoka mkubwa aina ya chatu. Nyoka  amekufa baada ya kujeruhiwa kwenye mapambano na paka.

Hell is the other people!- Jehanam ni wale wengine, lakini, pepo yaweza pia kuwa ni wale wengine.
Ni Neno La Leo.
Maggid,
Iringa

No comments:

Post a Comment