WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Friday, June 7, 2013

Rasimu ya Katiba Mpya yaleta hofu

Dodoma na Dar es Salaam. Baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani wamedai kuwa muungano unaweza kuvunjika kutokana na pendekezo la kuundwa kwa Serikali tatu lililotolewa kwenye rasimu ya Katiba Mpya na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.Akizungumzia suala hilo, Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani na Mbunge wa Iramba Mashariki, Tundu Lissu alisema Tume ya Nyalali na Kisanga ziliona matatizo katika kuunda Serikali tatu kwa kuwa zinaua Muungano, lakini kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya Jaji Joseph Warioba, imeuua Muungano.
“Pamoja na kwamba Wazanzibari wengi wamefurahia rasimu ya Katiba kwa kuipa mamlaka Zanzibar na Tanganyika, lakini watambue kuwa itafika hatua na wao watabaguana tu baadaye. “Labda isipite, lakini hili la Serikali tatu likipita, wapo watakaoanza chokochoko kama hizi, Wapemba nao watakuja kudai Jamhuri yao. Watatengana Wapemba na Waunguja ni yaleyale aliyoyaona Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere,” alisema Lissu.
Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Bariadi Mashariki, John Cheyo alihofia kuwepo kwa Serikali tatu, ambapo alibainisha kuwa kama pendekezo hilo litapita, basi Katiba Mpya iwe moja kwa Tanganyika na Zanzibar na mambo muhimu yaingizwe kwenye Katiba ya Shirikisho na iwe katiba moja badala ya kuanza kusaka Katiba Tanganyika na Zanzibar kwa kuwa mambo mengi ni yaleyale kama itaanza kutafutiwa maoni mengine.
Cheyo aliyewahi kuwania urais kupitia Chama cha UDP, 1995 na 2000 pia alisema kamwe mgombea binafsi wa urais hawezi kushinda nafasi hiyo japokuwa inapangwa kuingizwa kwenye Katiba Mpya. “Kuwepo ndani ya chama kunatengeneza mazingira mengi. unawekewa mazingira ya ushindi, watu wengi wanakuunga mkono kwa sauti moja, sasa ukiwa peke yako, ni kazi kweli kweli pamoja na kwamba itawekwa kwenye mpango, lakini mtu hawezi kushinda,” alisema Cheyo.
Naye Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mabere Marando alikosoa Rasimu ya Katiba Mpya ibara ya 187, ambayo inampa Rais mamlaka ya kuteua mkurugenzi wa tume ya uchaguzi na mkurugenzi wa usajili wa vyama vya siasa.
Akizungumza jana ofisini kwake Dar es Salaam, Marando ambaye pia ni wakili maarufu nchini alisema kuwa Rais ana hadhi kubwa. Hivyo ni vyema kama rasimu hiyo ingependekeza wakurugenzi hao wachaguliwe na wajumbe wa tume husika ambao wao wanateuliwa na Rais.
“Kuna kiwango cha nafasi za utendaji ambazo Rais anapaswa kuteua, lakini kwa nafasi hizi za wakurugenzi hawa ambao ni watendaji, wajumbe walipaswa kupewa jukumu la kuwachagua kwa kuwaajiri. Pia watumishi wengine wanaotumikia Tume ya Uchaguzi wanapaswa kuwa waajiriwa,” alisema Marando.

Katika rasimu hiyo Ibara ya 187 kifungu cha 5 inazungumzia kuwa uteuzi wa mkurugenzi wa uchaguzi na msajili wa vyama vya siasa utafanywa na Rais baada ya kuthibitishwa na Bunge na kifungu cha 6 kinaeleza kuwa katika kutekeleza majukumu yao, mkurugenzi wa uchaguzi na msajili wa vyama vya siasa watawajibika kwa Tume Huru ya Uchaguzi.
 Tume ya Warioba iliweka hadharani Rasimu ya Katiba Mpya, ikibainisha maeneo mbalimbali ya kufanyia marekebisho kutokana na mawazo ya watu wa kada mbalimbali.
source: Mwananchi
 • Lisu mbona huuleweki? SERIKALI TATU NI SERA YA CHADEMA. Ina maana mliweka sera huku mkijua kwamba ina madhara? Wacheni unafik ZANZIBAR ilikuwepo kabla ya Tanganyika na itaendelea kuwepo nje ya muungano. MUSIME WAZI KWAMBA HIYO BI HOFU YA WATANGANYIKA NABII WAO. MTAANZA KUBAGUWANA

  • Avatar

   ghibuu  18 hours ago

   Tundu lissu wacha unafikiri, wapemba kama watadai kujitenda watakuja kwenye serikali ya mapinduzi ya zanzibar na sio tanganyika sasa wewe unakuuma nini ? Hio ni haki yao kama raia,ndio democracy.
   Mbona nyi watanganyika munapenda kutia tia sumu ? Tunachotaka wazanzibari zanzibar yenye mamlaka kamili, na wala hatujafurahia rasimu hii, musione kimya tuko katika uchambuzi wa kujenga hoja.
   Rasimu hii amependekeza warioba kuunda serikali tatu, ya muungano ndo yenye mamlaka kamili, na maoni ya wazanzibari kupuuzwa tena ya walio wengi waliopendekeza muungano wa mkataba.
   Kwani sio ajabu kuvunjika muungano, sisi sio wa kwanza ambao tutakao kuwa tumevunja muungano, tumechoka na ukoloni, lets people talk and decide .

   • Avatar

    john  21 hours ago

    Wakati mwingine huwezi kujua exactly wanasiasa wetu wanataka kitu gani.Hakuna katiba ambayo inaweza kukithi kwa asilimia 100 wishes za kila mtu. Tume ya kukusanya maoni ilibidi ku- strike balance ( it is a give and take process)

    Tume imefanya kazi kubwa;

    Suala la raisi- itakuwa meaningless kuwa na executive president ambaye hatakuwa na powers. Raisi lazima awe na nguvu kiasi. haiwezekani raisi awe kila kitu lazima ategemee bunge au tume fulani. This is not ideal

    • Avatar


     john
     Bora wananchi wanamisimamo kuliko viongozi wa siasa na siasa yao, chadema ndio walikuwa wkaipigania serikali tatu, hata kama mktaba wao wako radhi alimuradi kwamba tanganyika inarudi, na wao ndio walikuwa wakisema kwamba zanzibar ni mzigo, sasa wananchi wametoa maoni juu ya katiba mpya na hasa zanzibar ambao wametoa hoja nzito juu ya muundo wa muungano, na wakapendekeza wengi wengi kutaka muungano wa mkataba.
     Warioba kwa maelezo yake, anasema kwamba walio pendekeza muungano wa mkataba ni wengi sana na hoja nzito, lakini kama yeye warioba amependekeza serikali tatu ,tena ya kikatiba, ina maana kazi yote imefanywa bure ? Maoni ya wazanzibari yame puuzwa, tumepoteza fedha za watoa jasho na rasilimali zetu bure ?
     Inasikitisha leo eti viongozi wamekuwa wakitoa sumu kama vile vyerere eti tutbaguana wapemba na waunguja, mbona hamusemi mutabaguana nyinyi kimiko na kikanda na ukabila ? Angalia mtwara vurugu, amngalia arusha vurugu, hao wote wanapigania nini ? Wanapigania maslahi yao kama wananchi kwa vile serikali imeshindwa kuwatekelezea.
     Sasa kama zanzibar vile vile itajitenga, na serikali hii ikaamuwa kuwatenga kimaendeleo wapemba, basi wanahaki kujitenga kama wataamua na kuweka hoja kwa serikali ya zanzibar , na pia kama watapeleka maombi yao UN. Tunachotaka wazanzibari mamlaka kamili ya nchi yetu, tuachiwe na matatizo yetu ya kijamii tuyamalize upemba na unguja, haiwahusu.

   No comments:

   Post a Comment