WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Tuesday, June 4, 2013

Mwili wa Mwanamiziki Mashuhuri Nchini Marehemu Albert Mangwea Aliyefariki Nchini Afrika ya Kusini Wawasili Nchini Leo

  Mwili wa Marehemu Albert Mangwea uliowasili mchana huu kutokea nchini Afrika ya Kusini.
Wadau mbalimbali
 Wadau mbali mbali wakiwa wamekusanyika kwa wingi kwenye uwanja wa Ndege Julius Nyerere kwa ajili ya kuupokea Mwili wa Marehemu Albert Mangwea uliowasili mchana huu kutokea nchini Afrika ya Kusini.
Baadhi ya mashabiki na wasanii waliojitokeza kuupokea mwili wa marehemu Albert Mangwea aliyekuwa mwanamuziki wa kizazi kipya. R.I.P Ngwea.
 Ilikuwa ngumu kuzuia hisia...
 Sehemu ya Wananchi na wapenzi wa Mwanamuziki Marehemu Albert Mangwea wakisukuma gari lilobeba mwili ake muda mfupi baada ya kuwasili jijini Dar es salaam ukitokea afrika ya kusini
 Rafiki kipenzi wa Marehemu Albert Mangwea,Jay Mo akihojiwa na vyombo vya habari uwanjani hapa.
 Prof. Jay nae alipata wasaha wa kuongea na vyombo vya habari juu ya Msanii mwenzao Albert Mangwea alietangulia Mbele ya haki.
Wadau kibao wapo uwanjani hapa hivi sasa tayari kwa kuupokea Mwili wa Marehemu Mangwea.KWA PICHA ZAIDIBOFYA HAPA    AU  BOFYA HAPA NA HAPA
 
source: haki ngowi

No comments:

Post a Comment