WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Monday, November 12, 2012

TUNAJIFUNZA NINI KIPINDI HIKI CHA CHAGUZI ZA VIONGOZI WA VYAMA NDANI YA TAIFA LETU KUELEKEA UCHAGUZI WA 2015?


NIONAVYO MIMI:


BADO TUNAHITAJI BUSARA ZAIDI KUTOKA KWA VIONGOZI WALIOKABIDHIWA DHAMANA KATIKA MAAMUZI YATAKAYO SAIDIA KUJENGA UCHUMI IMARA KWA FAIDA YA TAIFA KWA JUMLA;
Tukumbuke kuwa:

· 
  •  “Siasa si mchezo mchafu, ila wachezaji wake ndiyo wachafu.”

     
  •     Ni kweli kuwa  Siasa hutafasiriwa kuwa ni fikra, busara na mipango ya kuendesha nchi au ya kujinufaisha wao wenyewe?  



  •   Confucius aliwahi sema kuwa  ‘Utajiri na vyeo ndivyo vitu ambavyo kila bianadamu anavitamani; lakini ikiwa njia ya kuvipata ni kwa kwenda kinyume na misingi yake, anapaswa ajiepushe navyo.’


    
  •   Rudolph Giuliani aliwahi sema kuwa ‘Kiongozi huchaguliwa kwa kuwa yeyote anayemuweka pale huwa anaamini maamuzi, tabia na uwezo wa maarifa yake – siyo ujuzi wa kufuata maoni. Ni wajibu wa kiongozi kuchukua hatua kufuatana na sifa hizo.’

  
  •  “kiongozi ajiulize ni vipi atalitumikia Taifa na si Taifa kumtumikia yeye Kiongozi Umashuhuri na uzuri wa Kiongozi unatokana na hekima, busara, uchapakazi, ufanisi, ufuatiliaji, uimara, uungwana, uwajibikaji na unyenyekevu wake. Ama fikra endelevu na upeo wa kuongoza ni muhimu na si kauli tamu za kuwafurahisha viongozi wengine”

      
  •  Tamaa ya kujilimbikizia mali huo ni udhaifu wa mwanadamu ambao hapaswi kuupa nafasi iwapo unazingatia uadilifu wa uongozi


Demokrasia kama falsafa ya Plato ambayo inahusiana na uendeshaji wa shughuli za kisiasa inalenga zaidi katika  utumishi kwa umma na uendeshaji wa jamii na taifa. Wananchi wote hawawezi ongoza nchi kwa mara moja; Katika msingi huu wananchi kutokana na wingi wao waliridhika itakuwa sio rahisi kwa wao wote kukutana, kufanya maamuzi na kuyasimamia moja kwa moja maamuzi hayo yanayowahusu wao kama jamii; dhana ya kuwachagua viongozi wachache huzaliwa kwa chimbuko hili na kuruhusiwa kuunda serikali.


Tatizo kubwa tulilonalo kama Taifa ni ufinyu wa viongozi bora na utashi binafsi wa wachache walio katika nyanja za uongozi kwa kukosa sifa muhimu kwa viongozi. Kwani inatupasa kutambua kuwa uongozi si lelemama, ni kipaji na ni kazi ngumu. Lakini ridhaa hiyo haitolewi hivi hivi tu, inaambatana na amana, kwamba waongozi watatekeleza dhamana  na wajibu  wao kwa makubaliano na maelewano ya kufuata barabara na kuheshimu ipasavyo kanuni na maadili fulani yanayoitambulisha na kuiongoza jamii husika.


Uongozi ni kujitolea na kuweka matwakwa na maslahi ya wengine kuwa mstari wa mbele na si matakwa binafsi na kujinufaisha. Marehemu John Kennedy rais wa Marekani alitoa kauli moja maarufu iliyosema kuwa. Tuchague viongozi si kwa kuangalia vyama au sura, bali tuangalie uwezo wao wa kuongoza, kuhamasisha na kufanya kazi. Tupime kauli zao na matokeo ya kazi zao kama wanavyojinadi.


Mheshimiwa Rais, busara yako inahitajika sasa kuliko wakati mwingine wowote hasa katika kipindi hiki cha kuchagua wawakilishi na viongozi mbalimbali ndani ya chama chako; tuwapate viongozi ambao watakuwa tayari kuangalia hali halisi ya maisha ya mwananchi wa kawaida na mateso ya hali ngumu inayomzunguka; Busara yako Mheshimiwa Rais inahitajika sasa kuliko wakati mwingine wowote ili kudumisha amani na utulivu wa kweli na kujenga msingi mzuri wa viongozi wa uchaguzi wa 2015 kama CCM itapata ridhaa ya kuongoza Taifa letu.


Kama ilivyo kwa umoja wa kitaifa, kiongozi muadilifu pia hufanya kila bidii kuhakikisha amani na utulivu wa kweli katika nchi vinapatikana. Amani na utulivu ni chachu ya wananchi kwa kushirikiana na Serikali yao kujiletea maendeleo. Maendeleo hayaji mahala penye magomvi na uhasama. Lakini na amani na utulivu pia haviji mahala pasipo na haki na uadilifu. Uvunjifu wa amani na utulivu wa nchi hupelekea hasara ya maisha na mali ya watu na hayo hayawi malengo ya uongozi wenye misingi ya uadilifu katika nchi.


Uadilifu wa uongozi unadai kuheshimu nguvu ya hoja na fikra bora na hayo yanaweza kupatikana tu iwapo nchi inaongozwa kwa misingi ya kidemokrasia. Hivyo, katika kutoa uongozi sahihi, kwa kuzingatia maslahi bora ya nchi na watu wake, haki, uadilifu, umoja, amani na utulivu, hapana budi kwa kiongozi kuiamini, kuiheshimu na kuifuata barabara misingi ya kidemokrasia.

Bado binadamu si mkamilifu na kwa vyovyote vile hufikia mahala akafanya maamuzi ambayo si sahihi hata kama yalifanywa kwa nia njema na kwa kuzingatia taarifa zilizopatikana wakati maamuzi hayo yanafanywa. Hayo yanaeleweka na yakitokea,  kiongozi muadilifu anapaswa kuyakubali na kuliomba radhi Taifa. Hiki ndiyo kilele na kigezo kikuu cha uadilifu wa uongozi katika siasa. Kukubali kubeba dhamana kwa madhara yaliyotokana na maamuzi yako au yaliyofanywa kwa jina lako.



Maamuzi ya kiongozi wa kisiasa huathiri taifa zima, busara na hekima huzaa maamuzi yanayotokana na tafakuri ya kina, yanayozingatia hali halisi ya mambo na maslahi na manufaa ya muda mrefu. Kiongozi muadilifu anatakiwa ayaone haya na ayazigatie kwa kila hatua anayochukua. kitu kikubwa ambacho kitatokea katika harakati za uchaguzi ni kutofautiana;. Tukubali tu kuwa njia ya kusonga mbele ni kukubali kutofautiana katika fikra ambazo zitatokana na kampeni za uchaguzi husika lakini mwishowa uchaguzi inatupasa kubaki kuwa wamoja.


  
Viongozi ambao wanachaguliwa katika vipindi hivi vya chaguzi za vyama wawe ni msingi wa kweli wa uadilifu ili waweze kutuletea Kiongozi mzuri ambaye tutamkabidhi jahazi letu kuelekea kwenye maisha bora ya kila mtanzania; kama wananchi tumeshachoka na ubabaishaji wa viongozi wapenda rushwa, na wasiojali masilahi ya Taifa letu.

Leo tunashuhudia chaguzi za ndani za CCM, tunasubiri pia chaguzi za vyama vingine kama CUF; Chadema na vingine ambavyo vitajifunza katika mapungufu ya CCM na wao kufanya vizuri zaidi.


MUNGU IBARIKI TANZANIA

No comments:

Post a Comment