WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Sunday, November 11, 2012

NINI KINAENDELEA DODOMA NA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA KITAIFA WA CCM



kikao cha NEC kimepitisha  jina la Ndugu. Phillip Mangula Kuwa mgombea wa 
  Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara
kikao cha NEC kimepitisha  jina la  Rais wa Zanzibar Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk Ali Shein nae mapendekezwa kuendelea kutetea nafasi hiyo
kikao cha NEC kimepitisha kwa kishindo jina la  Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwa mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti CCM Taifa.
  Nape Nnauye ,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Kizota Usiku wa Leo
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi,Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akivishwa skafu na Chipukizi wa CCM alipowasili Makao Makuu ya CCM Dodoma jana
 Rais jakaya Kikwete akifungua rasmi kikao cha kamati kuu leo Dodoma.
 Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifungua kikao cha Halmashauri kuu ya CCM Taifa mjini Dodoma usiku wa kuamkia leo.Wengine katika picha kutoka kushoto ni Rais Mstaafu awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa,Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar(SMZ) Dkt.Ali Mohamed Shein,Rais Mstaafu wa Zanzibar Amani Abeid Karume, Katibu Mkuu wa CCM Dkt.Wilson Mukama na kulia ni Makamu mwenyekiti CCM Bara Ndugu Pius Msekwa.Ajenda kuu ya kikao hicho ni maandalizi ya mkutano Mkuu wa CCM utakaoanza kesho
 Mwenyekiti wa CCM Taifa,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifungua mkutano wa Halmshauri Kuu ya CCM Taifa mjini Usiku wa kuamkia leo Dodoma 
  Wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Halmshauri hiyo uliofanyika katika ukumbi wa White House leo usiku mjini Dodoma.
  Nape Nnauye ,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akipiga gitaa kwa ustadi kabla ya ufunguzi wa kikao cha Kamati Kuu na NEC,jana Dodoma katika Makao Makuu ya Chama.
---
Halmashauri Kuu ya Taifa ya CHAMA CHA MAPINDUZI  CCM iliyokaa kikao chake jana tarehe 10 November 2012, imependekeza Ndugu. Phillip Mangula kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara huku Rais wa Zanzibar Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk Ali Shein , akipendekeza kuwa mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar.

Nape Nnauye ,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Kizota,amesema majina hayo yatapigiwa kura na wajumbe wa mkutano mkuu siku ya jumanne.Hata hivyo ndugu Nape, amewaambia waandishi wa habari kuwa kikao cha NEC kimepitisha kwa kishindo jina la Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwa mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti CCM Taifa.

Pia kikao cha NEC kimefanya Mabadiliko kidogo ambapo leo wajumbe wa NEC nafasi kumi bara,na kumi Zanzibar watapigiwa kura leo tarehe 11 Novemba badala ya kesho, na matokeo yatatangazwa mara baada ya uchaguzi kumalizika.Wajumbe wote wa mkutano kutoka mikoa yote wameshawasili.

Wakati huo huo Rais Jakaya Kikwete kabla ya kufungua mkutano mkuu ataweka jiwe la msingi la Makao Makuu mapya ya CCM eneo la Makulu.

SOURCE: Haki Ngowi blog

No comments:

Post a Comment