WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Thursday, November 1, 2012

MWENYEKITI MPYA WA JUMUIYA YA WAZAZI APATIKANA



Abdallah Majura Bulembo
 
Picture: Abdallah Majura Bulembo

Refa wa zamani wa soka aliyewahi pia kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Mara, Abdallah Majura Bulembo, ameibuka kidedea na kuwa Mwenyekiti Mpya wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM Taifa baada ya kuzoa kura nyingi na kuwaacha mbali wapinzani wake John Barongo na Martha Mlacha (Mbunge wa Viti Maalum CCM).

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo jana, msimamizi wa uchaguzi huo uliofanyika mjini Dodoma, Steven Wassira, alisema Bulembo ameshinda baada ya kuzoa kura 680 atashika wadhifa huo kwa kipindi kijacho cha miaka minne.

Alisema kuwa Martha Mlata alipata kura 190 na hivyo kumaliza katika nafasi ya pili huku  John Barongo akiambulia kura 42 tu na hivyo kuwa nyuma ya Bulembo na Mlata.

Akizungumza baada ya kutangazwa kuibuka mshindi na kutangazwa rasmi kuwa mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Bulembo aliyekuwa akishangiliwa ukumbini mfululizo aliwashukuru wajumbe kwa kumpa ushindi wa kishindo, lakini akawaasa baadhi ya watu walioshindwa kwenye uchaguzi huo kukubaliana na matokeo ili kuendelea kukijenga chama chao.

"Miaka minne iliyopita nilisimama pia mbele yenu hna kuwaomba kura, lakini nikashindwa kwa vile kura hazikutosha... hata hivyo niliwashukuru sana na kuahidi kurudi. Leo nimetimiza wajibu huo. Lakini nasikitika kuona wenzangu ambao hawakusimama hapa," alisema Bulembo.

"Kura zao hazikutosha, hawakusaini, wamekimbia, wanaanzisha ajenda mpya... nawakumbusha kuwa katika Chama cha Mapinduzi (CCM) kuna kushinda na kushindwa. Wakubali matokeo kama mimi nilivyofanya miaka minne iliyopita," alisema Bulembo ambaye katika uchaguzi uliopita alishika nafasi ya pili baada ya kuzidiwa kura na Balozi Athumani Juma Mhina (sasa Marehemu) aliyetwaa nafasi hiyo.

Wengine waliofanya vizuri katika uchaguzi huo ni pamoja na Pandu Silima na Haji waliotwaa nafasi za ujumbe wa NEC-CCM kutokea Zanzibar huku wagombea wengine watatu wakiwamo Mussa Azzan Zungu, Jasson Rweikiza na Adam Malima wakitwaa nafasi ya ujumbe wa NEC-CCM kutokea Tanzania Bara.

Mbali na kuwahi kuwa refa na Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Mara (MRFA), Bulembo pia aliwahi kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).


Source: http://www.wavuti.com

No comments:

Post a Comment