WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Tuesday, November 13, 2012

JK apita kwa asilimia 99.92: Mangula, Shein mia kwa mia




CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) jana kilikamilisha safu yake ya uongozi kwa kuwapitisha kwa kishindo viongozi wa ngazi za juu wa Chama hicho katika uchaguzi ambao ulionekana kuwa na nidhamu kutokana na kutokuwa na uharibifu wa kura.


Katika uchaguzi wa safu za juu za Chama hicho, Mwenyekiti, Makamu wa Mwenyekiti Zanzibar na Bara wajumbe wa mkutano huo walitekeleza ombi la Yusuph Makamba la kumchagua kwa kishindo Jakaya Kikwete kuongoza CCM .

Akitangaza matokeo hayo Spika wa Bunge la Tanzania ambaye ndiye alikuwa msimamizi,Anne Makinda alisema kwamba Mwenyekiti  alipata ushindi wa kura 2,395 sawa na asilimia 99.92 huku kura mbili zikisema hapana.


Makamu Mwenyekiti Zanzibar Dk Ali Shein alipata kura 2,397 wakati makamu wa Bara Phillip Mangula naye alipata idadi hizo za kura huku kukiwa hakuna kura zilizoharibika wala kusema hapana kwa viongozi hao wawili.
Awali kabla ya kutamka ushindi wa viongozi wa juu, walitamkwa wajumbe 20 wa viti vya Bara na Zanzibar




No comments:

Post a Comment