WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Sunday, November 4, 2012

Simba yaacha bahari Dar kushangaa bwawa la Mindu, ilipogutuka, ishalishwa pingili mbili za Miwa! Kwisha khabari yake! Yanga waleee...


Picture
Mechi ya Yanga vs Azam (picha: Bin Zubeiry blog)
Kutoka mjini Morogoro Simba ya jijini Dar es Salaam leo imejikuta ikiangukia pua baada ya kuchapwa bao 2-0 na Mtibwa Sugar, mchezo litawaliwa na rabsha za mara kwa mara kutoka kwa mashabiki wa Simba waliokuwa na hasira wakidai mwamuzi Judith Gamba, alikuwa hawatendei haki.
Mtibwa ilijipatia bao dakika ya 34, kwa bao lililofungwa na Mohamed Mkopi baada ya Kipa Juma Kaseja kutema shuti kali la Vicent Barnabas.

Dakika ya 87, mshambuliaji mahiri Hussein Javu, aliipatia Mtibwa bao la pili, baada ya Kaseja kufanya mbwembwe langoni mwake.

Baada ya mchezo kumalizika, Kaseja aliangua kilio uwanjani huku mashabiki wakimzonga. Wachezaji wa Simba waligoma kupanda basi lao, ambako baadhi ya viongozi wao walifanya kazi ya ziada kuwabembeleza, ambako walikubali kwa shingo upande, lakini baada ya muda Mrisho Ngasa alishuka akiwa kabadilisha nguo kuondoka kivyake huku akisindikizwa na mashabiki lukuki.
Picture
Mshambuliaji wa Klabu ya Simba Emmanuel Okwi katikati akitafuta mbinu ya kuwatoka wachezaji wa Mtibwa Sugar, Jamali Simba kulia na Hussein Ramadhani kushoto wakati wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro. (picha: Juma Mtanda blog)
Mabao kutoka kwa straika wa kimataifa wa Burundi, Didier Kavumbagu na straika wa Uganda, Hamis Kiiza yaliipandisha Yanga kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuibuka na ushindi 'mtamu' wa mabao 2-0 dhidi ya Azam kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam huku mahasimu wao wa jadi, Simba wakipata kipigo cha ugenini cha 2-0 kutoka kwa Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro leo.

Katika mechi ya Taifa, Yanga walionyesha soka safi kuanzia mwanzo wa mechi hadi mwisho, wakigongeana pasi za kuvutia na kutawala mno katika eneo la katikati ya dimba lililokuwa chini ya himaya ya kiungo wao wa kimataifa kutoka Rwanda, Haruna Niyonzima 'Fabregas'.

Kavumbagu aliifungia Yanga bao la utangulizi katika kipindi cha kwanza na Kiiza alifunga goli la pili lkatika kipindi cha pili ambacho Azam walijikuta wakiusaka mpira kwa tochi kutokana na 'gonga' za kusisimua za Yanga; zikiwamo zilizozaa bao la Kiiza baada ya Fabregas, Kiiza na Chuji kupigiana 'one-two' kabla mfungaji kukwamisha mpira wavuni.

Kwa matokeo ya mechii za leo, Yanga imekamata usukani rasmi ikiwa na pointi 26 huku Simba ikibaki na pointi zake 23 wote wakiwa na michezo 12 huku Azam ikiwa nafasi ya tatu kwa pointi 21 huku Mtibwa ikifikisha pointi 13.

Yanga: Ally Mustafa Barthez, Mbuyi Twite, Oscar Joshua, Naroub Cannavaro, Kelvin Yondani, Athuman Idd, Simon Msuva, Frank Domayo, Didier Kavumbagu, Hamis Kiiza na Haruna Niyonzima.

Azam: Mwadini Ali, Erasto Nyoni, Ibrahim Shikanda, Aggrey Morris, Said Morad, Kipre Balou, Salum Abubakar, Jabir Aziz, John Boko, Kipre Tchetche, Hamis Mcha ‘Viali’.

Habari via Habari Mseto blog na Straika Mkali blog
Picture
Mwamuzi Judith Gamba akirushiwa chupa za maji na mashabiki wa Simba wakati akitoka uwanjani baada ya dakika 45 kumalizika.
Picture
Polisi wamemkwida "Tanganyika jeki" mshabiki wa Simba aliyehusika na vurugu za kumshambulia mwamuzi wa mchezo huo.
Picture
Mwamuzi wa kati Judith Gamba kutoka Arusha (mwenye mpira) akiwaongoza wachezaji wa klabu ya Mtibwa Sugar Manungu Turiani na Simba katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara uwanja wa Jamhuri Morogoro. (picha: Juma Mtanda blog)
Source: http://www.wavuti.com

No comments:

Post a Comment