WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Sunday, November 4, 2012

Lowassa aenda Ujerumani kwa matibabu



Monduli
ALIYEKUWA Waziri Mkuu katika Serikali ya Awamu ya Nne, Edward Lowassa yupo nchini Ujerumani kwa matibabu na uchunguzi wa kiafya.

Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli jana hakuwapo katika uzinduzi wa mradi wa Barabara ya Minjingu hadi Arusha na shule jimboni kwake, uliofanywa na Rais Jakaya Kikwete aliye ziarani mkoani Arusha.

Kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Jowika Kasunga na baadaye kusambazwa kwa waandishi wa habari, Lowassa alieleza kusikitishwa kutokuwapo jimboni kwake wakati huo ambao Rais Kikwete anatembelea jimbo lake.


Lowassa alisema kuwa, hali hiyo imetokana na kuwa safarini kwa ajili matibabu lakini akasema anaamini mambo yataenda vizuri si kwa ziara hiyo ya Rais Kikwete bali hata vikao vya juu vya CCM vinavyotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Katika taarifa hiyo, alimsifu  Rais Kikwete kuwa, kutokana na kutekeleza vizuri na kwa uadilifu Ilani za uchaguzi za CCM, wiki mbili zijazo wanaCCM watakwenda Dodoma kuidhihirishia dunia  na Watanzania wenye shaka kwamba wanamwamini na kuuthamini uongozi wake.

Katika maelezo hayo, Lowassa alieleza tatizo linalomsumbua kuwa ni macho, lakini pia atatumia nafasi hiyo kuchunguza afya yake.

Aidha, alimshukuru Rais Kikwete kwa kuzindua miradi hiyo akisema inadhihirisha mambo mawili makubwa aliyoyafanya kwa kiwango cha juu chini ya uongozi wake akiwa Rais wa Tanzania.

“Mosi, chini ya uongozi wako shule nyingi zaidi zimejengwa kuliko awamu zote zilizotangulia. Pili, kilomita za barabara za lami zilizoongezeka wakati wa awamu yako ni ndefu kuliko wakati mwingine wowote,” alisema Lowassa na kuongeza:

“Kwa hakika umetekeleza vizuri, kikamilifu na kwa uadilifu Ilani za uchaguzi za CCM, mwaka 2005 na 2010. Sisi wanachama wa CCM na wananchi wa Monduli ni mashahidi wa jambo hili. Tunaamini ndivyo ilivyo kwa nchi nzima.”

Mwishoni mwa wiki ijayo CCM itafanya uchaguzi mkuu wa uchaguzi ngazi ya taifa kuanzia mwenyekiti wa chama na viongozi wengine, ili kukamilisha kupanga safu mpya ya uongozi kwa ajili  ya uchaguzi mkuu wa 2015.

CCM ipo katika uchaguzi wa ndani wa chama hicho ambapo tayari jumuiya zake za Wazazi, Vijana na Wanawake zimekamilisha chaguzi hizo, huku kambi ya Lowassa ikitajwa kuibuka kidedea kwa kunyakua nafasi mbalimbali zilizowaniwa, kuanzia ngazi za wilaya hadi jumuiya za chama kitaifa.

Katika uchaguzi wa UWT, Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Taifa, Sophia Simba ambaye alitetea nafasi yake na Makamu wake, Asha Bakari Makame wanatajwa kuwa wafuasi wa Lowassa, huku wajumbe sita kati ya wanane  waliochaguliwa kuwakilisha jumuiya hiyo katika Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho, wakiwa waumini wa kambi hiyo.
 
Wajumbe sita kati ya wanane walioshinda nafasi za ujumbe wa NEC kupitia jumuiya hiyo  wanatajwa kuwa wafuasi wa Lowassa,  huku mmoja akitajwa kuwa hana kundi lolote huku mwingine akitajwa kumuunga mkono aliyekuwa mgombea wa uenyekiti wa UWT na Mbunge wa Same Mashariki, Anne Killango Malecela.

Kwa upande wa UVCCM, Mbunge wa Donge, Sadifa Juma Khamisi ambaye alichaguliwa kuwa Mwenyekiti kwa kura 483 na makamu wake, Mboni Muhita pia wanatajwa kuwa wafuasi wa kambi ya Lowassa.

Waliotwaa ujumbe wa NEC na ujumbe wa Baraza Kuu la Umoja huo, pia wanatajwa kuwa waumini wa kambi hiyo.

Hata hivyo, katika uchaguzi wa Jumuiya ya Wazazi uliokuwa wa funga dimba la mfululizo wa chaguzi za chama hicho tawala kuanzia ngazi za shina tangu Aprili, waliokuwa wagombea wa nafasi ya uenyekiti, John Barongo na Abdallah Bulembo kwa nyakati tofauti walikanusha kuwa na masilahi na makundi huku Martha Mlata akikataa kuzungumzia uchaguzi huo.

Rais Kikwete
Akizungumza katika hafla hiyo, Kikwete alisema kwamba ni lazima barabara zote ziwekwe matuta ili kuzuia ajali za barabarani, akieleza kuwa mara nyingi baada ya ujenzi wa barabara, kinachofuatia ni vifo vinavyotokana na tabia ya madereva wakorofi.
Mwananchi

No comments:

Post a Comment