WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Sunday, March 31, 2013

UCHAGUZI WA RAIS KATIKA JAMUHURI YA WATU WA KENYA 2013; UMEKWISHA NA UHURU KENYATTA NI RAIS MTEULE KUAPISHWA April 9 2013





  • NI KWELI KUWA SIASA NI MCHEZO MCHAFU?

  • KAMA NCHI JIRANI TUMEJIFUNZA NINI?

Siasa ni mfumo ambao unahusisha zaidi uongozi wa watu kwa kufuata kanuni, sheria, sera, uwajibikaji, uwazi na ugawaji wa rasilimali sawa kwa wananchi wake hasa  katika kuwaleta maendeleo  wadau wakuu kwa maneno mengine wanahisa wakuu ambao  ni wananchi.

Kwa msingi wa utashi huu, wananchi wanakichagua kikundi cha watu au chama ambacho wanawaamini na kuwapa uwezo wa kuunda serikali ili iwaongoze kwa niaba yao.  Kwa hivyo hakuna nchi yeyote hapa duniani ambayo haina serikali. Tofauti inayoweza kujitokeza ni namna serikali hiyo inavyoundwa katika misingi ipi? Na inatekeleza vipi kanuni na taratibu zake? Je kuna uwazi katika shughuli zake? Viongozi wanabebe dhamana ya watu katika utendaji wao na wawajibikaje kwa wananchi ambao ndio waliowaweka ofisini; na viongozi wanatakiwa wawajibike na kuwaletea maendeleo wananchi wao.

Siasa kama siasa sio mchezo mchafu; siasa inageuka kuwa mchezo mchafu pale tu serilali au chama cha upinzani  ambavyo vimekabidhiwa dhamana na wananchi  vinaanza kwenda kinyume na utaratibu na kanuni sahihi,  na kuto fuata   maadili ya uongozi (code of conduct) ndipo tafsiri ya siasa inaanza kugeuka na kuwa mchezo mchafu. 

Misingi ya siasa chafu imechochewa sana na mwanasalsafa Machiavelli  ambaye aliandika katika maandishi yeke kuhusu viongozi na madaraka; kitabu chake kinawanufaisha sana viongozi katika kuimarisha  nafasi zao za uongozi, amewafundisha viongozi namna ya kuwa waongo (liar), wakatili, wanafiki,  kuwa na uchu wa mali, na hata ikibidi kuua ili kupata madaraka na kuudumisha adhima yao ya kuendelea kunyonya na kujitajirisha. mwongozo huu wa Machiavelli unatumiwa sana na watawala wa mabavu (dictators), kutoka nchi mbalimbali ambao waliongoza au wanaongoza nchi zao kwa manufaa binafsi na sio kuwaletea maendeleo wananchi bali huwajengea hofu na kuwasababishia wananchi wao maisha magumu. Tumewaona  watawala kama; Idd Amin Dada, Mabuto, na kadhalika. Katika mlengo huu hakuna kuwajibishana, kinachofanyika hapa wananchi wanatiwa tu kufuata na  kusikiliza na kutii tuKila kiti ambacho wananfanya na wanatakiwa kuwa watiifu kama usipotia au kama ukikidhana kimawzo na viongozi hao unaishia pabaya tumeona vifo na maisha magumu ya baadhi ya wananchi, ambao waliishia kuishi ughaibuni.
 

Uchafu wa siasa ni pale tunapoilinganisha siasa kama wapiganaji katika mchezo wa mieleka ule ambao hauna kanuni yeyote ili ushinde, unaweza kumchezee au kumpiga au kumwangusha mpinzani wako kwa namna yeyote ile uwezayo ili mradi tu wewe uwe mshindi; hapa hakuna  kanuni yeyote inayohitajika refarii yuko pale kutangaza mshindi tu kwani hana kanuni yeyote ambayo anafuata; hapo ndipo tafsiri ya mchezo mchafu inapoanza.je nini kazi ya wanasheria wetu? Utetezi au uonevu? Tatizo la mchezo huu ukiuanza huwezi kuuacha. Ushauri kama huuwezi kamwe usiucheze waache wanaouweza waucheze,  watu wenye kiburi na wasiojali utu hata mara moja. Na ukiamua kuucheza kamwe usiuache au usiwasaliti wenzako ukifanya hivyo safari yako yakuendelea kufurahia maisha ya siasa yataishia kaburini.

Je siasa zetu zinalenga wapi tunaoutaratibu ambao tunaweza kumwajibisha hata kiongozi wa juu wa    nchi anapokiuka maadili ya uongozi? mkumbuke Nixon na “Watergate scandal” kwa kosa lolote lile ambalo alifanya akiwa kama kiongozi mkuu wan nchi alikiuka maadili ya uongozi kulingana na taratibu za serikali ya Marekani kilichofuata ni kumpigia kura ya kutomwamini na kumwondoa ofisini kama Raisi; alikwenda kwenye ziara kama Raisi wa Marekani ndani ya "Airforce One" lakini alirudi nyumbani kama raia wa kawaida kwa kutumia ndege ya kawaida ya abiria.

                                                                 
Siasa sio mchezo mchafu kwa watu ambao ni wanyeneyekevu na wenye huruma ya kuwahurumia wanyonge, watu wanaomwogopa Mungu, na daima sio wala rushwa, siasa kama kazi ni sawa na kazi nyingine zinazotakiwa kufuata taaratibu, tukumbuke kuwa iwapo mtu mwenye haki anaongoza nchi kila mtu atafurahia matunda na maziwa yatokanayo na rasilimali ya nchi hiyo, lakini iwapo nchi itaongozwa na mtu mwovu, fisadi wanyonge wataumia sana na wenye nacho wataongezewa. Na hapo tutakendelea na kilio cha kila siku kwanini sisi ni masikini katika nchi hii iliyojaa maziwa na asali na wakati huo huo inawatajirisha watu au inchi nyingine?

Tukumbuke kwa wale ambao wamesoma kitabu cha sharkespear  nini alikifanya Macbeth kwa kusababisha umwagaji wa damu ambao ulikuwa hauna sababu kwa sababu tu ya  siasa  za ubinafsi na hatimaye kutekeleza mwonekano wa siasa kuwa mchezo mchafu ambao mwisho wa siku ulimgeukia mwenyewe na kuuwawa. Tatizo la uchafu wa siasa pengine huanzia kwa serikali kuona kuwa ofisi zao ndio biashara yao hivyo hata ile mishahara ambayo wamewekewa kisheria haiwatoshi na huanza kujiingiza katiak rushwa, mikataba mibovu ambayo inawapa masilahi wao binafsi, na kuwaongezea nguvu ya kipesa na uwezo wa kuongoza kwa masilahi ya watu wachache.

Siasa sio mchezo mchafu kwa watu ambao ni wanyeneyekevu na wenye huruma ya kuwahurumia wanyonge, watu wanaomwogopa Mungu, na daima sio wala rushwa, siasa kama kazi ni sawa na kazi nyingine zinazotakiwa kufuata taaratibu, tukumbuke kuwa iwapo mtu mwenye haki anaongoza nchi kila mtu atafurahia matunda na maziwa yatokanayo na rasilimali ya nchi hiyo, lakini iwapo nchi itaongozwa na mtu mwovu, fisadi wanyonge wataumia sana na wenye nacho wataongezewa. Na hapo tutakendelea na kilio cha kila siku kwanini sisi ni masikini katika nchi hii iliyojaa maziwa na asali na wakati huo huo inawatajirisha watu au inchi nyingine?

Katika nchi zetu ambazo umasikini umekidhiri, tatizo la kukosekana kwa ajira, kupeana kazi na vyeo kwa kufuata undugu na urafiki na sio sifa za elimu, kuwanunua watu kwa kuwapa zawadi wakati wa kampeni na hatimaye wakati wa upigaji wa kura, kwa misingi hiyo sio rahisi baada ya uchaguzi kwa wananchi kuwawajibisha viongozi wao. Siasa taalumu nzuri sana na muhimu kwa jamii ikiwa itawapata viungozi wazuri na waungwana ambao wamewaeka wananchi mbele ya maendeleo yao, lakini siasa ikiwapata viongozi wabovu wala rushwa nchi imekwisha na wanyonge hawana chao ndipo hapo siasa inapokuwa ni mchezo mchafu. Kwa msingi huu ni kuwa siasa sio mchezo mchafu ni mchafu tu ikipata watu wala rushwa  na sio waaminifu, walafi wa madaraka,
 
Ni mchezo mchafu tu kama utaratibu wote wa uchaguzi haukwenda vizuri na matokeo yake baada ya hapo ni chuki binafsi baina ya vyama na hiyo mwisho wa siku itamaanisha kuwa chama tawala na  chama cha upinzani ni maadui na hakuna wa umuhimu wa chama kingine kuwapo, vyama vya siasa katika nchi vinaweza kuiongoza kwa kupokezana ni kama huko Marekani wakati wananchi wanapoona kuwa nchi iko amani yao ina mashaka wanakipigia chama cha Republican lakini wakiona uchumi wao unayumba wanakipigia chama cha Democratic;

Tukumbuke maneno ya Raisi JF Kennedy wa Marekani alivyosema” hakuna mtu ambaye atanishawishi mimi kufanya kitu ambacho nafikiri sio kwa masilahi ya nchi yangu, kama wewe au mtu mwingine anafikiri kuwa ndiye, basi huyo ni Mwendawazimu” Hii ndio tofauti ya kiongozi ambaye kwake siasa ni mchezo mzuri kwa masilahi ya wananchi wake na taifa lake, ambaye ni mkweli mwadilifu na ambaye anaweza kutoa maamuzi mazito kwa faida ya nchi yake;

 LAKINI pale tunapokosa maadili ya uiongozi tunakaribisha sana  urafiki, undugu na kugeuza ofisi zetu ambazo zimewekwa kwa masilahi ya Taifa kuwa sehemu za biashara na kuwakaribisha zaidi wenye fedha kututawala kwa kutoa mwongozo nini kifanyike hapo ndipo tunabadilisha tafsiri sahii ya siasa kuwa mchezo mchafu. Pengine bora hata kiongozi ambaye ni mbabe wa maendeleo ya taifa ambaye anapinga uzembe na hana rafiki wala ndugu ndugu yake ni maendeleo ya nchi yake. Je tunao viongozi wa namna hii hasa barani Afrika. tumkumbuke Mzee wetu, Mandela Nyerere na wengine wa namna kama yao.


Uchaguzi wa Jamuhuri ya watu wa Kenya ambao ulifanyika  March 3 2013 tunamshukuru Mungu umeisha salama ambapo mgombea wa urais wa Muungano wa Jubilee Bwana Uhuru Kenyatta amefanikiwa kuwashinda wagombea wenzake nane akiwiwamo mshindani wake wa karibu na waziri Mkuu ambaye amemaliza kipindi chake bwana Raila Odinga.

Kama wanahabari wengi walivyoandika kuwa umekwenda vizuri pamoja na kasoro ambazo zimejitokeza lakini demokrasia imeheshimiwa na wananchi wameyapokea matokea wakiwa na nia mpya ya kuijenga Kenya mpya. Pengine uchaguzi wa mwaka 2007 ambao ulishia na machafuko na mauaji ya wananchi ambao hawana hatia tayari limekuwa ni somo nzuri na wananchi hawataki kurudi tena huko.

Kama wadau wakuu wa siasa wananchi wameamua kuheshimu matokeo kwa faida ya Taifa.Tuchukue fursa hii pia kuwapongeza Wakenya kwa kufanikisha uchaguzi mkuu kwa amani na utulivu. Ni imani yetu kwamba utulivu huo utadumishwa pasipo kuathiriwa na hila zinazohusisha uhasama wa aina yoyote ile.Baada ya maamuzi ya Mahakama kuu kuhusu Pingamizi ambayo Mheshimiwa Odinga aliweka na Mahakama kutupilia mbali pingamizi hiyo na MAHAKAMA KUU YAAMUA UHURU NDIYE MSHINDI HALALI

“Mahakama ya Juu imefikia uamuzi kwa kauli moja kuhusu masuala manne yaliyoibuliwa kwenye kesi za uchaguzi. Uchaguzi ulifanyika kwa njia huru na ya haki na kwa kufuata Katiba na Sheria,” alisema Jaji Mutunga kabla ya kutangaza kuwa Uhuru Kenyatta na William Ruto walichaguliwa kwa njia huru na ya haki kuwa Rais na Naibu Rais mtawalia.

“Kesi za Raila na AFRiCOG zimetupwa. Kila mtu ajilipie gharama. Uamuzi wa kina utatolewa katika muda wa wiki mbili.”

Hebu tuangalie kauli mbalimbali kufuatia uamuzi wa mahakama:

“Mahakama imetekeleza jukumu lake. Jukumu sasa ni kwa raia, viongozi wao, mashirika ya kijamii na wanahabari kuhakikisha umoja wa Kenya unadumu,” alisema Jaji Mutunga.
WAZIRI MKuu Raila Odinga amekubali kushindwa baada ya Mahakama ya Juu kutupilia mbali kesi yake kupinga kupinga kuchaguliwa kwa Uhuru Kenyatta. Bw Odinga amemtakia Rais Mteule kila la heri.

“Hatua yangu ya kwenda mahakamani ilikuwa ishara ya imani yangu katika Mahakama. Haikuwa ni ya kisasi.  Tulijaribu kadiri ya uwezo wetu. Mawakili wetu wakiongozwa na Oraro walikusanya na kuwasilisha ushahidi mwingi.”

“Tunasikitika kwamba Mahakama ilikataa ushahidi kwa msingi kuwa uliwasilishwa kuchelewa au mahakama haikuwa na muda. Mwishowe, Wakenya walipoteza nafasi ya kujua nini kilitendeka.”

“Mimi na Kalonzo hatuna majuto kwa kuwasilisha kesi kortini. Ni matumaini yangu kwamba serikali ijayo itaheshimu Katiba na kuitekeleza. Namtakia Rais Mteule Uhuru Kenyatta na kundi lake kila la kheri. Pia, maseneta wabunge, wawakilishi wa wanawake na magavana ufanisi. Tusigawanywe na mtukio haya. Natoa wito kwa Wakenya na wafuasi wangu wakumbuke maneno ya Wimbo wa Taifa – “Haki iwe ngao na mlinzi.’”


 Sasa ni wakati wa kuijenga Kenya mpya kwa kuzika yote yaliyopita ambayo yalileta mtikisiko kama vile ukabila uliosababisha maafa kama ilivyokuwa uchaguzi Mkuu mwaka 2007. Hakika Wakenya wameonyesha ukomavu kisiasa na ndiyo maana uchaguzi huu umefanyika kwa amani na utulivu wa hali ya juu. Bravo Kenya, bravo Wakenya.
Kama alivyowahi kusema mheshimia James
Mbatia kuwa Uchaguzi wa Kenya ni mfano wa kuigwa kutokana na namna Wananchi walivyohamasika kushiriki katika zoezi la kupiga kura huku Tume ya Uchaguzi nchini humo ikionekana kujipanga ipasavyo kwa ajili ya zoezi hilo.


Tunawatakia Ndugu zetu wa Jamhuri ya watu wa Kenya kila la kheri katika kendelea kulinda demokrasia na kuhakikisha kuwa vurugu zilizotokea mwaka 2007 hazijirudii tena.  Uongozi wako Uhuru kama Rais wa awamu ya nne ukizingatia maadili ya uongozi bora utawaletea faraja wakenya wote bila kujali tofauti zao za kabila au dini.

God Bless Kenya

No comments:

Post a Comment