WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Thursday, March 7, 2013

Kutoka Ikulu Zanzibar:Taswira za Ziara ya Rais wa Zanzibar Dr Ali Shein Mkoa wa Mjini Magharibi

 Pichani Ujenzi Skuli ya Sekondari ya Wilaya huko Mpendae Mjini Zanzibar ukiendelea katika Mkoa wa Mjini Magharibi ,ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alitembelea ujenzi huo akiwa katika ziara ya Mkoa huo iliyoanza jana
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na wafanyakazi katika  Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi alipofanya ziara ya Mkoa huo iliyoanza jana
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Viongozi wa Vikosi vya Ulinzi alipowasili katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi akiwa katika ziara ya Mkoa huo iliyoanza jana
Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akionesha zawadi aliyopewa na  Mkuu wa  Mkoa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis,(katikati) alipofika Ofisini kwake akiwa katika ziara ya Mkoa huo iliyoanza jana ,(kushoto) Mkuu wa
Wilaya Mjini Abdi Mahmoud Mzee
 Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo ya Ujenzi kutoka kwa  Mhandisi wa Ujenzi  wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Iddi Khatib,alipotembelea kukagua Ujenzi wa Skuli ya Sekondari ya Wilaya huko Mpendae Mjini Zanzibar,akiwa katika ziara ya mkoa Mjini Magharibui iliyoanza jana.
 Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji (ZAWA) DK.Mustafa Ali Garu,alipofika Chumbuni Kuangalia mradi uchimbaji wa  kisima cha Maji katika eneo hilo akiwa katika ziara ya Mkoa wa Mjini Magharibi iliyoanza jana
 Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akibadilishana mawazo na Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Hassan Ali Mbarouk,(wa pili kushoto) wakati alipotembelea kituo kipya cha Umeme huko Welezo alipokuwa katika ziara ya Mkoa wa Mjini Magharibi iliyoanza jana
 Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Hassan Ali Mbarouk,(kulia) akitoa maelezo kwa Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,wakati alipotembelea kituo kipya cha Umeme huko Welezo alipokuwa katika ziara ya Mkoa wa Mjini
Magharibi iliyoanza jana
Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na wananchi na wazee wa Chumbuni  Wilaya ya Mjini Mkoa Mjini Magharibi, alipofungua kituo cha Mafunzo ya Kazi za Amali,akiwa katika ziara Mkoa huo,(kulia) Naibu waziri wa Ulinzi Perera Ame Silima,na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Abadala Mwinyi Khamis,na (kushoto)Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Mwinyihaji Makame
 
Baadhi ya Viongozi na watendaji wa Idara mbali mbali za Ofisi za Serikali wakiwa katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi,katika mkutano na Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa katika ziara ya Mkoa huo iliyoanza jana.
 
Picha Zote na Ramadhan Othman,Ikulu-Zanzibar

No comments:

Post a Comment