WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Saturday, March 16, 2013

Yanga 1:0 Ruvu Shooting; Mtibwa 1:1 Coastal Union


Picture

Yanga vs Ruvu Shootings katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam (picha: Sufiani Mafoto blog)
Timu ya Yanga leo imeifunga timu ya Ruvu Shooting goli 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya VodaCom uliochezwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam. Goli hilo lilifungwa na Hamisi Kiiza “Diego” kunako dakika ya 48 ya mchezo na hivyo kuipa Yanga jumla ya pointi 48 katika ligi hiyo.

Katika mechi nyingine ya ligi hiyo iliyochezwa kwenye kiwanja cha Manungu mkoani Morogoro, timu za Mtibwa Sugar na Coastal Union zimetoshana nguvu kwa kutoka sare ya kufungana 1-1 na hivyo kufikisha pointi 32 kila moja.

Coastal Union walipata goli lao katika dakika kwanza tu ya kipindi kupitia kwa Ibrahim Twaha “Messi”, goli ambalo lilidumu kipindi kizima cha kwanza. Mtibwa Sugar walisawazisha katika kipindi cha pili.

Hadi kufikia sasa, Azam FC inashikilia nafasi ya pili wakati Simba SC ipo katika nafasi ya tatu


No comments:

Post a Comment